Mbwa jamii ya Rottweiller waua mwangalizi wao Dar

Maana wezi wenyewe hawaji kilichobaki ni kuwapeleka kusaka kenge na sungura bobi wetu

enzi zile kanidakia sungura sana kule milimani kiding'a,ila tukrudi nyumbani linazubaa zubaaa tu
Huwa kina bobi tunawatumia kama alarm, ila sio ulinzi. Akibweka tu, unatoka nje kuchungulia

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Mimi nafuga kwa mapenzi najiona fahari kuzungukwa na mbwa, vile tu breed nyingi hazipatikani kirahisi, kwa sasa na GS 1 na Rott 5, am dog lover
 
natafuta mbwa aina ya KANGAL hawa kiturkey naweza pata wapi, hawa ndo mbwa bora kwangu, si pitbull wala rott wanakaa kwa huyo mjuba,
 
Mkuu anakutishia na wakati una miaka nao 8 kama unavyobainisha
Anyway mkuu unashauri mbwa gani wa kufuga ambaye sio mkali sana kama huyo RW
German shepherd ni mkali lakini mtiifu sana na anafundishika kirahisi, anapokea order mapema na hasau. Rott shida yake kubwa ni mgumu kufundishika na kigeugeu anaka kukumbushwa Mara kwa mara
 
Sisi tunapambana na hawa wetu wa kienyeji, wanakula dagaa unawachanganyia na pumba za mahindi na wanakulinda poa kabisa.
Chakula siyo issue, issue ni kufundisha na kuendana na tabia zake, wakwangu wanakula chakula chochote,
 
hujanijibu, namuulizia KANGAL, kwa hapa tz naweza mpata wapi?
Mzee baba Mimi siwezi kujua labda Nenda wizara ya mifugo, Uzi wangu nimeongelea rott, huyo unayeuliza sijawahi muona. Mimi nina rott 4 na GS mmoja
 
Ikiwa nitapata muda nitafanya hivo, kwa kijibu pia swali lako ikiwa unaanza kufuga mbwa kwa Mara ya kwanza na kushauri uanze na mbwa mdogo kabisa ili upate kujua tabia zao. Lakini hata ukirithi mbwa mkubwa haina shida kwani mbwa anatabia ya kuishi kwa territory. Hivo anapofika eneo geni atahitaji kuyazoea mazingira na kuwazoea wale wanao mpatia chakula, mfanye mbwa wako azoee familia tote kwa ujumla, asiyependa mbwa hakikisha Nate anazoea,
Kuhusu chakula mzoeshe chakula chochote kinacholiwa na binadamu, wali,ugali, dagaa, Nyama, epuka kumpa nyama au damu mbichi. Unaweza pia mpatia chakula cha dukani Kama pedigree,supa dog nk
 
Mbona uzi unaohusu mbwa wa kizungu na ufugaji upo humu kitambo sana, na umezungumzia vitu vingi sana.

Tena kuna hadi vile vimbwa vya kina Wema Sepetu ambavyo unaweza ukavipiga teke vikaenda kuangukia kwa jirani mtaa wa pili, alaf unaambiwa vinauzwa hela ndefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…