Analyse
JF-Expert Member
- Jan 19, 2014
- 17,637
- 47,413
Yeah, aende vichakani kusaka vicheche na kengeAkasake. [emoji16][emoji16]
Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yeah, aende vichakani kusaka vicheche na kengeAkasake. [emoji16][emoji16]
Huwa kina bobi tunawatumia kama alarm, ila sio ulinzi. Akibweka tu, unatoka nje kuchunguliaMaana wezi wenyewe hawaji kilichobaki ni kuwapeleka kusaka kenge na sungura bobi wetu
enzi zile kanidakia sungura sana kule milimani kiding'a,ila tukrudi nyumbani linazubaa zubaaa tu
Mimi nafuga kwa mapenzi najiona fahari kuzungukwa na mbwa, vile tu breed nyingi hazipatikani kirahisi, kwa sasa na GS 1 na Rott 5, am dog loverTabu yote ya nini nyinyi waafrika.
Mnalinda vitu gani hadi mpate tabu zote hizo,kwani mna benki kwenye manyumba yenu.
Kuna jamaa mmoja naye anafuga mbwa wa staili hiyo sasa kila siku mida ya usiku kuna mlinzi huwa anaenda kumfungulia then asubuhi anamfungia na kuondoka.
Sasa siku hiyo mlinzi hakuja kumfungia asubuhi basi mke wa mwenye nyumba akatoka nje aende kazini La haula wala kuwata alivamiwa na huyo mbwa alimchakata miguu bahati yake mumewe alikuwepo ndani akawahi kumshika na kumfungia vinginevyo angemuua.
Sasa nikajiuliza hiyo adhabu yote ya nini
ngoja tupambane na hawa koko tunawatunga majina eti simba 😂😂😂Hahahahah mbwa ni domestic ila kuna breed sio za kufuga hasa hao Rotweillers na Pitbull. Hawafai kwa jamii zetu za kiswahilini swahilini ambako hakuna nidhamu.
Otherwise jiandae na msiba tena hao pitbull ndio balaa.
natafuta mbwa aina ya KANGAL hawa kiturkey naweza pata wapi, hawa ndo mbwa bora kwangu, si pitbull wala rott wanakaa kwa huyo mjuba,Wana jamvi niwasalimu kwanza, na moja kwa moja niende kwenye mada.
Asubuhi ya leo nimepokea taarifa toka kwa rafiki yangu mmoja aliyeko Dar akitaka kufahamu kwa nini mbwa jamii ya Rottwieler hugeuka na kushambulia wamiliki na kufikia kuwaua. Hii ni kutokana na ukweli kwamba usiku wa kuamkia leo mbwa aina tajwa hapo wamemshambulia mpaka kumuua kijana mtunza bustani ambaye ndo alikuwa akiwatunza na kuwapa chakula.
PAMOJA na kuhitaji kupata ushauri tayari alikuwa ameconclude kuwa Rottweiler siyo mbwa wa kufugwa kitu ambacho mimi na kikataa kutoka na kwamba nimekuwa nikifuga jamii ya mbwa kwa miaka kadhaa, na hata ninapoandika bandiko hili ninao wanne, majike wawili na madume wawili.
JE, NI KWELI KWAMBA ROTTWEILLER NI HATARI SANA?
Jibu ni ndiyo, huyu mbwa anashikilia nafasi ya pili duniani hii ni kwa mjibu wa jarida la K-9 Dog day ya tarehe 26 August 2020, mbwa huyu anaguvu ya kung'ata ( PSI Pound per Square Inch or Pound-force per Square Inch 328 akiwa anakamata nafasi ya 12 dunia. Pamoja na hizo sifa hapo juu mbwa huyu bado kwangu ni mbwa rafiki endapo utakuwa naye karibu na kuonyesha unamjali sana, ( Kifupi ana wivu mnoooo ikiwa ulikuwa umezoea kucheza naye lakini ukabadilika na kuamishia mapenzi kwa kitu kingine kama paka, ng'ombe, mbuzi na hata mtoto Rottweiler anatabia ya kulipa kisasi, hata kama ni wao kwa wao ikiwa wako zaidi ya mmoja na wengine ukawa unawafungia kwenye kennel na mmoja ukamwacha free lazima huyu aliyeko free watamua tu.
Pia kama hauna muda wa kucheza nao kuwatembeza na kuwaruhusu kufanya mazoezi basi usifuge Rottweiler kwani kitakachofuata ni majonzi. Historia ya mbwa huyu inaenda mbali sana tangu zama za ufalme wa kirumi ambapo walitumika kusaidia wafugaji kuchunga mifugo na kuvuta mikokoteni. Kutokana na kuvuta mikokoteni mara nyingi mbwa hawa walivunjika mikia na ndo maana hata leo hii umekuwa kama utamaduni mara nyingi wamiliki wa hawa mbwa huwakata mikia.
NINI UFANYE KAMA UNAFUGA ROTTWEILER
Asubuhi kabla hujawaingiza bandani hakikisha unapata muda wa kuonana nayo cheza nao kidogo wafanyie groomimng, kisha waingize bandani na ikiwa unatabia ya kuwapa breakfast baada ya breakfast waache nje kwa muda ili wacheze, hakikisha una matoyi ya wao kuchezea kama vitenesi ( Napoongelea vitenesi nina maanisha vile ambavyo ni special kwa mbwa usinunue hivi vya kawaida make watatafuna na kumeza na hii inaweza kupelekea kifo. Nunua mifupa ile ya mpira wape waangaike nayo kwa muda kisha warudishe bandani.
Wafundishe utii kwa zile basic command kama ACHA, NJOO, INGIA NDANI. Tumia lugha hiyo kila siku.
KUWA NA MUDA MAALUM WA KUWAPA CHAKULA
Usiwaache na njaa muda mrefu na endapo umechelewa kuwapa chakula na ikawa tayari ni usiku kabla ya kuwafungulia jaribu kuvaa nguo walizozizoea na usijipulizie manukato. Ikiwa umewafungua banda anza na yule mkorofi zaidi akishatoka nje akiwa peke yake ni rahisi kumkontrol na hatimaye kukutambua tena. Baada ya hapo ndo ufungulie waliobaki. Endapo utawafungulia wote na ni usiku wakaona labda paka na kuanza kumfukuza ukijaribu kuwazuia wasiposikia usijaribu kuwapiga make tayari wana hasira na watakugeuka. Wazungu wanesema respect the power' Rottweiler is a loaded gun if not properly handled. Be Leader and not a boss to the breed.
Usiwaache wakuongoze bali uwaongoze ( These are dogs and they leave in packs ) wewe ndo uwe pack leader na si wao.
Usiache hawa mbwa kuhudumiwa na house boy au garderner muda wote, kama itabidi basi mfundishe namna ya kuishi na hawa mbwa.
NAWAPENDA ROTTWEILER
Kwa sababu najihisi salama zaidi kuliko mbwa mwingine yeyote, kwangu mimi wamewahi kumdhibiti mchawi saa nane usiku, na ikabidi yeye mwenyewe aombe msaada na kuonekana na kila mtu pale nyumbani usku.
UFANYE NINI
UKISHAONA MBWA WAKO WANAMSHAMBULIA MTU NDANI YA COMPOUND USITUMIE FIMBO BALI WAZUIE KWA ORDER YA MDOMO NA IKIWA HAWAKUSIKILIZI TUMIA MPIRA KUWA MWAGIA MAJI.
Nasema hivi kwa sababu huyu aliyeuliwa wamiliki na waajiri wameshindwa kumsaidia hii ni kwa sababu hawajawazoea mbwa, wameita kampuni ya ulinzi nayo ikashindwa kumwokoa mpaka polisi nao hakuweza kumwokoa mpaka walipolazimika kupiga mbwa wote wanne risasi. Lakini ikiwa hii kampuni wangejua namna ya kumwokoa mtu anayeshambuliwa na mbwa ilikuwa watume gari ya fire na siyo mobili crews ambao pamoja na bunduki zao hawakuweza kutoa msaada.
Sisi tunapambana na hawa wetu wa kienyeji, wanakula dagaa unawachanganyia na pumba za mahindi na wanakulinda poa kabisa.Sawa hao kibongo bongo hawafai
German shepherd ni mkali lakini mtiifu sana na anafundishika kirahisi, anapokea order mapema na hasau. Rott shida yake kubwa ni mgumu kufundishika na kigeugeu anaka kukumbushwa Mara kwa maraMkuu anakutishia na wakati una miaka nao 8 kama unavyobainisha
Anyway mkuu unashauri mbwa gani wa kufuga ambaye sio mkali sana kama huyo RW
Chakula siyo issue, issue ni kufundisha na kuendana na tabia zake, wakwangu wanakula chakula chochote,Sisi tunapambana na hawa wetu wa kienyeji, wanakula dagaa unawachanganyia na pumba za mahindi na wanakulinda poa kabisa.
German shephered ndio mbwa intelligent kuliko wote. Huyu ndio ana akili timamu na msikivu.German shepherd ni mkali lakini mtiifu sana na anafundishika kirahisi, anapokea order mapema na hasau. Rott shida yake kubwa ni mgumu kufundishika na kigeugeu anaka kukumbushwa Mara kwa mara
hujanijibu, namuulizia KANGAL, kwa hapa tz naweza mpata wapi?Chakula siyo issue, issue ni kufundisha na kuendana na tabia zake, wakwangu wanakula chakula chochote,
Hiyo ni sahihi kabisa, kuna jamaa alitaka kuniuzia G-Shepherd kwa laki 6 na niongeze laki 2 unusu ya mbwa kufundishwa utii na ukali. Nikaenda nunua wa elfu 70 na anatimiza wajibu wake vizuri kabisa.Chakula siyo issue, issue ni kufundisha na kuendana na tabia zake, wakwangu wanakula chakula chochote,
Hahahahah ufala😂Huwa kina bobi tunawatumia kama alarm, ila sio ulinzi. Akibweka tu, unatoka nje kuchungulia
Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
Mzee baba Mimi siwezi kujua labda Nenda wizara ya mifugo, Uzi wangu nimeongelea rott, huyo unayeuliza sijawahi muona. Mimi nina rott 4 na GS mmojahujanijibu, namuulizia KANGAL, kwa hapa tz naweza mpata wapi?
Ntamuomba msamaha kuna mruzi wake mtamu kinoma yani. 😂Ukichelewa kurudi home lazima akurarue.
Unarudi umevaa magunia alafu unamuomba msamaha 😂Sasa sisi wazee wa kula tungi tukitoka kazini na home mpaka mida ya wangua si watuwaisha ahera siku si zetu
Ikiwa nitapata muda nitafanya hivo, kwa kijibu pia swali lako ikiwa unaanza kufuga mbwa kwa Mara ya kwanza na kushauri uanze na mbwa mdogo kabisa ili upate kujua tabia zao. Lakini hata ukirithi mbwa mkubwa haina shida kwani mbwa anatabia ya kuishi kwa territory. Hivo anapofika eneo geni atahitaji kuyazoea mazingira na kuwazoea wale wanao mpatia chakula, mfanye mbwa wako azoee familia tote kwa ujumla, asiyependa mbwa hakikisha Nate anazoea,Mkuu nimekuelewa. Sasa labda nakuja kwako kununua GS au RW, Mimi ndio mara ya kwanza mbwa ananiona, hua mnafanyaje ili mbwa ambaye ndio anapewa mteja aweze kumzoea Siku hio.
**Mkuu kama hutojali kama utaweza kufungua thread kwa wale ambao tunapenda kufuga mbwa hao, mbinu, lugha za kutumia, vyakula, na mengineyo ya muhimu kwa aina zote za mbwa hao akina GS, RW, PB, nk
Mbona uzi unaohusu mbwa wa kizungu na ufugaji upo humu kitambo sana, na umezungumzia vitu vingi sana.Mkuu nimekuelewa. Sasa labda nakuja kwako kununua GS au RW, Mimi ndio mara ya kwanza mbwa ananiona, hua mnafanyaje ili mbwa ambaye ndio anapewa mteja aweze kumzoea Siku hio.
**Mkuu kama hutojali kama utaweza kufungua thread kwa wale ambao tunapenda kufuga mbwa hao, mbinu, lugha za kutumia, vyakula, na mengineyo ya muhimu kwa aina zote za mbwa hao akina GS, RW, PB, nk