kiboboso
JF-Expert Member
- Sep 17, 2013
- 9,323
- 12,594
Hao ndo mbwa wa kufuga. Sio unafuga matatizo bila kujua.Nawapenda pia German Shepherd
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hao ndo mbwa wa kufuga. Sio unafuga matatizo bila kujua.Nawapenda pia German Shepherd
kwangun siyo issue ninao mwaka kama wa nane wakikaribia kuzeeka naandaa wengine, nawamudu hamna shakaSasa na wewe jiandae mzee!
Sikutishi bali nakupa makavu
Mkuu nadhani kuna kitu hujaelewa ndo maana nikasema ikiwa huwezi hayo masharti usige rott make ni sawa na bunduki ambayo tayari risasi iko chemba haitaki mzaha zaidi ya Ku engage safety pin. Siyo lazima ufage MBDA ambao huwezi kuwahudumia. Funga mbuzi au kondoo. Nimeleta hii mada ili watu wajifunze kwani kuna MTU Jana mida Kama hii alikuwa hai lakini kwa kukosa elimu sasa hivi yuko mochwariNtapata wapi muda wa kuhudumia mara mbilimbili
Hawa jamaa nawaelewa Sana unambii chochote hapa namtafuta mnyama anaitwa Belgium Malinois huyu ndo hatari zaidi, bahati mbaya nchi nyingi zimempiga marufuku
Hawana shida mi nyumbani wana urafiki na kila MTU na wanapenda mno kucheza, kinachonifurahisha mkichelewa kuamka wanakuja kuwaamshaView attachment 1628722
wabongo kwa kuiga vya wazungu,igeni na hiiii Fugeni hii kitu halafu muwekeni Junior akae pembeni wacheze nae.
Tanzania Hao Belgium wapo kweli?Hawa jamaa nawaelewa Sana unambii chochote hapa namtafuta mnyama anaitwa Belgium Malinois huyu ndo hatari zaidi, bahati mbaya nchi nyingi zimempiga marufuku
Hamna labda Kenya unaweza kupata kwa sababu kuna wafugaji wengi ambao ni members wa K9 breeersTanzania Hao Belgium wapo kweli?
Sisi tushazoea mbwa unamlisha dagaa, au unamuacha akasake. Sasa haya ya kulisha mbwa msosi wa supermarket sio yetu.
ambapo kwa puppy wanauzwaje?Hamna labda Kenya unaweza kupata kwa sababu kuna wafugaji wengi ambao ni members wa K9 breeers
Sina uhakika Ila haiwezi chini ya USD 250 kwenda juu. Na huyu ni hatari zaidi kibongo bongo kwani anaweza kuruka fence bila wasiwasi na kuleta madhara njeambapo kwa puppy wanauzwaje?
Wana jamvi niwasalimu kwanza, na moja kwa moja niende kwenye mada.
Asubuhi ya leo nimepokea taarifa toka kwa rafiki yangu mmoja aliyeko Dar akitaka kufahamu kwa nini mbwa jamii ya Rottwieler hugeuka na kushambulia wamiliki na kufikia kuwaua. Hii ni kutokana na ukweli kwamba usiku wa kuamkia leo mbwa aina tajwa hapo wamemshambulia mpaka kumuua kijana mtunza bustani ambaye ndo alikuwa akiwatunza na kuwapa chakula.
PAMOJA na kuhitaji kupata ushauri tayari alikuwa ameconclude kuwa Rottweiler siyo mbwa wa kufugwa kitu ambacho mimi na kikataa kutoka na kwamba nimekuwa nikifuga jamii ya mbwa kwa miaka kadhaa, na hata ninapoandika bandiko hili ninao wanne, majike wawili na madume wawili.
JE, NI KWELI KWAMBA ROTTWEILLER NI HATARI SANA?
Jibu ni ndiyo, huyu mbwa anashikilia nafasi ya pili duniani hii ni kwa mjibu wa jarida la K-9 Dog day ya tarehe 26 August 2020, mbwa huyu anaguvu ya kung'ata ( PSI Pound per Square Inch or Pound-force per Square Inch 328 akiwa anakamata nafasi ya 12 dunia. Pamoja na hizo sifa hapo juu mbwa huyu bado kwangu ni mbwa rafiki endapo utakuwa naye karibu na kuonyesha unamjali sana, ( Kifupi ana wivu mnoooo ikiwa ulikuwa umezoea kucheza naye lakini ukabadilika na kuamishia mapenzi kwa kitu kingine kama paka, ng'ombe, mbuzi na hata mtoto Rottweiler anatabia ya kulipa kisasi, hata kama ni wao kwa wao ikiwa wako zaidi ya mmoja na wengine ukawa unawafungia kwenye kennel na mmoja ukamwacha free lazima huyu aliyeko free watamua tu.
Pia kama hauna muda wa kucheza nao kuwatembeza na kuwaruhusu kufanya mazoezi basi usifuge Rottweiler kwani kitakachofuata ni majonzi. Historia ya mbwa huyu inaenda mbali sana tangu zama za ufalme wa kirumi ambapo walitumika kusaidia wafugaji kuchunga mifugo na kuvuta mikokoteni. Kutokana na kuvuta mikokoteni mara nyingi mbwa hawa walivunjika mikia na ndo maana hata leo hii umekuwa kama utamaduni mara nyingi wamiliki wa hawa mbwa huwakata mikia.
NINI UFANYE KAMA UNAFUGA ROTTWEILER
Asubuhi kabla hujawaingiza bandani hakikisha unapata muda wa kuonana nayo cheza nao kidogo wafanyie groomimng, kisha waingize bandani na ikiwa unatabia ya kuwapa breakfast baada ya breakfast waache nje kwa muda ili wacheze, hakikisha una matoyi ya wao kuchezea kama vitenesi ( Napoongelea vitenesi nina maanisha vile ambavyo ni special kwa mbwa usinunue hivi vya kawaida make watatafuna na kumeza na hii inaweza kupelekea kifo. Nunua mifupa ile ya mpira wape waangaike nayo kwa muda kisha warudishe bandani.
Wafundishe utii kwa zile basic command kama ACHA, NJOO, INGIA NDANI. Tumia lugha hiyo kila siku.
KUWA NA MUDA MAALUM WA KUWAPA CHAKULA
Usiwaache na njaa muda mrefu na endapo umechelewa kuwapa chakula na ikawa tayari ni usiku kabla ya kuwafungulia jaribu kuvaa nguo walizozizoea na usijipulizie manukato. Ikiwa umewafungua banda anza na yule mkorofi zaidi akishatoka nje akiwa peke yake ni rahisi kumkontrol na hatimaye kukutambua tena. Baada ya hapo ndo ufungulie waliobaki. Endapo utawafungulia wote na ni usiku wakaona labda paka na kuanza kumfukuza ukijaribu kuwazuia wasiposikia usijaribu kuwapiga make tayari wana hasira na watakugeuka. Wazungu wanesema respect the power' Rottweiler is a loaded gun if not properly handled. Be Leader and not a boss to the breed.
Usiwaache wakuongoze bali uwaongoze ( These are dogs and they leave in packs ) wewe ndo uwe pack leader na si wao.
Usiache hawa mbwa kuhudumiwa na house boy au garderner muda wote, kama itabidi basi mfundishe namna ya kuishi na hawa mbwa.
NAWAPENDA ROTTWEILER
Kwa sababu najihisi salama zaidi kuliko mbwa mwingine yeyote, kwangu mimi wamewahi kumdhibiti mchawi saa nane usiku, na ikabidi yeye mwenyewe aombe msaada na kuonekana na kila mtu pale nyumbani usku.
UFANYE NINI
UKISHAONA MBWA WAKO WANAMSHAMBULIA MTU NDANI YA COMPOUND USITUMIE FIMBO BALI WAZUIE KWA ORDER YA MDOMO NA IKIWA HAWAKUSIKILIZI TUMIA MPIRA KUWA MWAGIA MAJI.
Nasema hivi kwa sababu huyu aliyeuliwa wamiliki na waajiri wameshindwa kumsaidia hii ni kwa sababu hawajawazoea mbwa, wameita kampuni ya ulinzi nayo ikashindwa kumwokoa mpaka polisi nao hakuweza kumwokoa mpaka walipolazimika kupiga mbwa wote wanne risasi. Lakini ikiwa hii kampuni wangejua namna ya kumwokoa mtu anayeshambuliwa na mbwa ilikuwa watume gari ya fire na siyo mobili crews ambao pamoja na bunduki zao hawakuweza kutoa msaada.
Nimemuonesha uzi huu rafiki yangu mhehe ametoa masikitiko take watu wa mifugo ya kuila lakini wanailealea mpaka inawatafuna wao
Mbwa mwenyewe anaonekana amekaa kishari shari tu.