dvj nasmiletz
JF-Expert Member
- Jul 23, 2018
- 2,079
- 2,254
Huyo ndo marehem??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo ndo marehem??
Sura mbaya na kutisha na hasira kwanini umfuge
Hebu nitumie number za huyo trainer wa mbwaHiyo ni sahihi kabisa, kuna jamaa alitaka kuniuzia G-Shepherd kwa laki 6 na niongeze laki 2 unusu ya mbwa kufundishwa utii na ukali. Nikaenda nunua wa elfu 70 na anatimiza wajibu wake vizuri kabisa.
Ila kwa sasa yuko Mbeya, kuna mwingine pia yuko MorogoroHebu nitumie number za huyo trainer wa mbwa
Hapana kwa kweli kwahyo suraMbwa kwa ajili ya ulinzi ila sharti na ww umlinde
Huko mbali I thought wa DarIla kwa sasa yuko Mbeya, kuna mwingine pia yuko Morogoro
Siko Dar mkuu, mimi ni wa mikoani.Huko mbali I thought wa Dar
OkaySiko Dar mkuu, mimi ni wa mikoani.
Mkuu nafikiri kuna makosa ya kimatumizi maana kwa nijuwavyo hawa jamii hiyo ya mbwa huwa ni walinzi kwenye sehemu ambayo watu wanakuwa hawapo kwa muda huo.kama vile bank au mahali panapohifadhiwa vito vya thamani na huwa wanawekwa baada ya muda wa kazi na kuondolewa kabla ya muda wa kazi na watu maalumu na wenye mava,I maalumu, hawa ni moja ya jamii ya mbwa ambayo ni wakali sana na uwezi wao wa kupokea amri ni mdogo sana wao kazi yao ni kushambulia kilichoko mbele yao.Hii mbegu ni noma haitakagi ujinga, kama mtu hana uelewa wa kuwadhibiti, ni bora ya kukaa nao mbali. Nawafahamu sana.
Msasani kubwa hebu weka contact hapa au pmDar mbn wapo msasani
Pita insta @NattyDogs au https://nattydogs.co.tz/ uone vyuma vya kaziMsasani kubwa hebu weka contact hapa au pm
ThanksPita insta @NattyDog au https://nattydogs.co.tz/ uone vyuma vya kazi
Aisee hiyo picha ya kwanza mbwa yuko siriaz utadhani mshua anakucheki unavyozingua.
Aisee, ndio maana vinauzwa bei,???Mzee vile kazi yake ni kuzama chumvini kma ulikua ujui
Mbwa anabajet kubwa kuliko binadam [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kumuogesha sawa, ilo hata kwakina bobi nalifanya. Ila kumnunulia vitu vya kuchezea? Hell no [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]usisahau kumuogesha
Unafanyaje?, Unawanusisha?Mbwa dawa yake ugolo tu hapo ndipo huwa nawadharau wanaojivunia kufuga mbwa
[emoji23][emoji23][emoji23]Kumuogesha sawa, ilo hata kwakina bobi nalifanya. Ila kumnunulia vitu vya kuchezea? Hell no [emoji23][emoji23]
Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
Kwaiyo mtu ameshambuliwa wameita vikosi vyote ivo na vikafika bado wanamshambulia tu kweli tz hali imebadilika watu wako chap haraka now daysWana jamvi niwasalimu kwanza, na moja kwa moja niende kwenye mada.
Asubuhi ya leo nimepokea taarifa toka kwa rafiki yangu mmoja aliyeko Dar akitaka kufahamu kwa nini mbwa jamii ya Rottwieler hugeuka na kushambulia wamiliki na kufikia kuwaua. Hii ni kutokana na ukweli kwamba usiku wa kuamkia leo mbwa aina tajwa hapo wamemshambulia mpaka kumuua kijana mtunza bustani ambaye ndo alikuwa akiwatunza na kuwapa chakula.
PAMOJA na kuhitaji kupata ushauri tayari alikuwa ameconclude kuwa Rottweiler siyo mbwa wa kufugwa kitu ambacho mimi na kikataa kutoka na kwamba nimekuwa nikifuga jamii ya mbwa kwa miaka kadhaa, na hata ninapoandika bandiko hili ninao wanne, majike wawili na madume wawili.
JE, NI KWELI KWAMBA ROTTWEILLER NI HATARI SANA?
Jibu ni ndiyo, huyu mbwa anashikilia nafasi ya pili duniani hii ni kwa mjibu wa jarida la K-9 Dog day ya tarehe 26 August 2020, mbwa huyu anaguvu ya kung'ata ( PSI Pound per Square Inch or Pound-force per Square Inch 328 akiwa anakamata nafasi ya 12 dunia. Pamoja na hizo sifa hapo juu mbwa huyu bado kwangu ni mbwa rafiki endapo utakuwa naye karibu na kuonyesha unamjali sana, ( Kifupi ana wivu mnoooo ikiwa ulikuwa umezoea kucheza naye lakini ukabadilika na kuamishia mapenzi kwa kitu kingine kama paka, ng'ombe, mbuzi na hata mtoto Rottweiler anatabia ya kulipa kisasi, hata kama ni wao kwa wao ikiwa wako zaidi ya mmoja na wengine ukawa unawafungia kwenye kennel na mmoja ukamwacha free lazima huyu aliyeko free watamua tu.
Pia kama hauna muda wa kucheza nao kuwatembeza na kuwaruhusu kufanya mazoezi basi usifuge Rottweiler kwani kitakachofuata ni majonzi. Historia ya mbwa huyu inaenda mbali sana tangu zama za ufalme wa kirumi ambapo walitumika kusaidia wafugaji kuchunga mifugo na kuvuta mikokoteni. Kutokana na kuvuta mikokoteni mara nyingi mbwa hawa walivunjika mikia na ndo maana hata leo hii umekuwa kama utamaduni mara nyingi wamiliki wa hawa mbwa huwakata mikia.
NINI UFANYE KAMA UNAFUGA ROTTWEILER
Asubuhi kabla hujawaingiza bandani hakikisha unapata muda wa kuonana nayo cheza nao kidogo wafanyie groomimng, kisha waingize bandani na ikiwa unatabia ya kuwapa breakfast baada ya breakfast waache nje kwa muda ili wacheze, hakikisha una matoyi ya wao kuchezea kama vitenesi ( Napoongelea vitenesi nina maanisha vile ambavyo ni special kwa mbwa usinunue hivi vya kawaida make watatafuna na kumeza na hii inaweza kupelekea kifo. Nunua mifupa ile ya mpira wape waangaike nayo kwa muda kisha warudishe bandani.
Wafundishe utii kwa zile basic command kama ACHA, NJOO, INGIA NDANI. Tumia lugha hiyo kila siku.
KUWA NA MUDA MAALUM WA KUWAPA CHAKULA
Usiwaache na njaa muda mrefu na endapo umechelewa kuwapa chakula na ikawa tayari ni usiku kabla ya kuwafungulia jaribu kuvaa nguo walizozizoea na usijipulizie manukato. Ikiwa umewafungua banda anza na yule mkorofi zaidi akishatoka nje akiwa peke yake ni rahisi kumkontrol na hatimaye kukutambua tena. Baada ya hapo ndo ufungulie waliobaki. Endapo utawafungulia wote na ni usiku wakaona labda paka na kuanza kumfukuza ukijaribu kuwazuia wasiposikia usijaribu kuwapiga make tayari wana hasira na watakugeuka. Wazungu wanesema respect the power' Rottweiler is a loaded gun if not properly handled. Be Leader and not a boss to the breed.
Usiwaache wakuongoze bali uwaongoze ( These are dogs and they leave in packs ) wewe ndo uwe pack leader na si wao.
Usiache hawa mbwa kuhudumiwa na house boy au garderner muda wote, kama itabidi basi mfundishe namna ya kuishi na hawa mbwa.
NAWAPENDA ROTTWEILER
Kwa sababu najihisi salama zaidi kuliko mbwa mwingine yeyote, kwangu mimi wamewahi kumdhibiti mchawi saa nane usiku, na ikabidi yeye mwenyewe aombe msaada na kuonekana na kila mtu pale nyumbani usku.
UFANYE NINI
UKISHAONA MBWA WAKO WANAMSHAMBULIA MTU NDANI YA COMPOUND USITUMIE FIMBO BALI WAZUIE KWA ORDER YA MDOMO NA IKIWA HAWAKUSIKILIZI TUMIA MPIRA KUWA MWAGIA MAJI.
Nasema hivi kwa sababu huyu aliyeuliwa wamiliki na waajiri wameshindwa kumsaidia hii ni kwa sababu hawajawazoea mbwa, wameita kampuni ya ulinzi nayo ikashindwa kumwokoa mpaka polisi nao hakuweza kumwokoa mpaka walipolazimika kupiga mbwa wote wanne risasi. Lakini ikiwa hii kampuni wangejua namna ya kumwokoa mtu anayeshambuliwa na mbwa ilikuwa watume gari ya fire na siyo mobili crews ambao pamoja na bunduki zao hawakuweza kutoa msaada.