Mbwa jamii ya Rottweiller waua mwangalizi wao Dar

Mbwa jamii ya Rottweiller waua mwangalizi wao Dar

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Yaani nifuge mbwa kwa ajili ya ulinzi alafu niishi kwa masharti magumu kiasi hicho eti kisa wana wivu! Kwani mbwa wa kufuga wameisha mpaka nikafuge wao
Masharti utafikiri unaenda kutaka utajiri kwa mganga wakienyeji
 
Ikiwa umesoma mstari mmoja hutonielewa nimekwambia ikiwa umechelewa kuwafungulia na endapo hawana actvities huwa wanakuwa aggressive, hivo unapoenda kuwafungulia usiku na endapo ule muda wa kawaida umechelewa vaa nguo walizozizoea na usijipake manukato kama unabisha endelea kubisha mimi nawajua hawa mbwa kwa uzoefu kwa sababu nawafuga kwa miaka kadhaa ninauzoefu nao. jiulize inakuwaje wanamshambulia mbwa mwenzao ambaye kila siku wanakuwa pamoja? ni ipi harufu ambayo walipaswa kuizoea zaidi kati ya mbwa mwenzao na ya kwako? chukuwa tahadhari kama huwezi kuendana na hawa mbwa usijaribu kuwafuga. mimi mtu akija kununua mbwa kwangu namweleza kabisa.
Sasa utajuaje kama nguo hii wameizoea?
 
Hahahahah mbwa ni domestic ila kuna breed sio za kufuga hasa hao Rotweillers na Pitbull. Hawafai kwa jamii zetu za kiswahilini swahilini ambako hakuna nidhamu.

Otherwise jiandae na msiba tena hao pitbull ndio balaa.
Vipi kuhusu bulldogs
 
Kwani mkuu nikivaa mavazi ya kunilinda na hatari mfano yale makoti magumu

mabuti miguuni halafu mikononi natia Gloves za maana,kichwani namalizia na Helmet

halafu nakua naenda wahudumia raia wangu,kuna shida mkuu kwenye mavazi yangu hayo

yani naingia bandani kwao nikiwa Full gwanda kama naenda Jupiter,si fresh mkuu FURY BORN

View attachment 1628723
Kama wanang'oa mpaka taa za gari hapo ndo watashindwa kukutafuna sasa.
 
Wana jamvi niwasalimu kwanza, na moja kwa moja niende kwenye mada.

Asubuhi ya leo nimepokea taarifa toka kwa rafiki yangu mmoja aliyeko Dar akitaka kufahamu kwa nini mbwa jamii ya Rottwieler hugeuka na kushambulia wamiliki na kufikia kuwaua. Hii ni kutokana na ukweli kwamba usiku wa kuamkia leo mbwa aina tajwa hapo wamemshambulia mpaka kumuua kijana mtunza bustani ambaye ndo alikuwa akiwatunza na kuwapa chakula.

PAMOJA na kuhitaji kupata ushauri tayari alikuwa ameconclude kuwa Rottweiler siyo mbwa wa kufugwa kitu ambacho mimi na kikataa kutoka na kwamba nimekuwa nikifuga jamii ya mbwa kwa miaka kadhaa, na hata ninapoandika bandiko hili ninao wanne, majike wawili na madume wawili.

JE, NI KWELI KWAMBA ROTTWEILLER NI HATARI SANA?
Jibu ni ndiyo, huyu mbwa anashikilia nafasi ya pili duniani hii ni kwa mjibu wa jarida la K-9 Dog day ya tarehe 26 August 2020, mbwa huyu anaguvu ya kung'ata ( PSI Pound per Square Inch or Pound-force per Square Inch 328 akiwa anakamata nafasi ya 12 dunia. Pamoja na hizo sifa hapo juu mbwa huyu bado kwangu ni mbwa rafiki endapo utakuwa naye karibu na kuonyesha unamjali sana, ( Kifupi ana wivu mnoooo ikiwa ulikuwa umezoea kucheza naye lakini ukabadilika na kuamishia mapenzi kwa kitu kingine kama paka, ng'ombe, mbuzi na hata mtoto Rottweiler anatabia ya kulipa kisasi, hata kama ni wao kwa wao ikiwa wako zaidi ya mmoja na wengine ukawa unawafungia kwenye kennel na mmoja ukamwacha free lazima huyu aliyeko free watamua tu.
Pia kama hauna muda wa kucheza nao kuwatembeza na kuwaruhusu kufanya mazoezi basi usifuge Rottweiler kwani kitakachofuata ni majonzi. Historia ya mbwa huyu inaenda mbali sana tangu zama za ufalme wa kirumi ambapo walitumika kusaidia wafugaji kuchunga mifugo na kuvuta mikokoteni. Kutokana na kuvuta mikokoteni mara nyingi mbwa hawa walivunjika mikia na ndo maana hata leo hii umekuwa kama utamaduni mara nyingi wamiliki wa hawa mbwa huwakata mikia.

NINI UFANYE KAMA UNAFUGA ROTTWEILER
Asubuhi kabla hujawaingiza bandani hakikisha unapata muda wa kuonana nayo cheza nao kidogo wafanyie groomimng, kisha waingize bandani na ikiwa unatabia ya kuwapa breakfast baada ya breakfast waache nje kwa muda ili wacheze, hakikisha una matoyi ya wao kuchezea kama vitenesi ( Napoongelea vitenesi nina maanisha vile ambavyo ni special kwa mbwa usinunue hivi vya kawaida make watatafuna na kumeza na hii inaweza kupelekea kifo. Nunua mifupa ile ya mpira wape waangaike nayo kwa muda kisha warudishe bandani.
Wafundishe utii kwa zile basic command kama ACHA, NJOO, INGIA NDANI. Tumia lugha hiyo kila siku.

KUWA NA MUDA MAALUM WA KUWAPA CHAKULA
Usiwaache na njaa muda mrefu na endapo umechelewa kuwapa chakula na ikawa tayari ni usiku kabla ya kuwafungulia jaribu kuvaa nguo walizozizoea na usijipulizie manukato. Ikiwa umewafungua banda anza na yule mkorofi zaidi akishatoka nje akiwa peke yake ni rahisi kumkontrol na hatimaye kukutambua tena. Baada ya hapo ndo ufungulie waliobaki. Endapo utawafungulia wote na ni usiku wakaona labda paka na kuanza kumfukuza ukijaribu kuwazuia wasiposikia usijaribu kuwapiga make tayari wana hasira na watakugeuka. Wazungu wanesema respect the power' Rottweiler is a loaded gun if not properly handled. Be Leader and not a boss to the breed.

Usiwaache wakuongoze bali uwaongoze ( These are dogs and they leave in packs ) wewe ndo uwe pack leader na si wao.
Usiache hawa mbwa kuhudumiwa na house boy au garderner muda wote, kama itabidi basi mfundishe namna ya kuishi na hawa mbwa.

NAWAPENDA ROTTWEILER
Kwa sababu najihisi salama zaidi kuliko mbwa mwingine yeyote, kwangu mimi wamewahi kumdhibiti mchawi saa nane usiku, na ikabidi yeye mwenyewe aombe msaada na kuonekana na kila mtu pale nyumbani usku.

UFANYE NINI
UKISHAONA MBWA WAKO WANAMSHAMBULIA MTU NDANI YA COMPOUND USITUMIE FIMBO BALI WAZUIE KWA ORDER YA MDOMO NA IKIWA HAWAKUSIKILIZI TUMIA MPIRA KUWA MWAGIA MAJI.

Nasema hivi kwa sababu huyu aliyeuliwa wamiliki na waajiri wameshindwa kumsaidia hii ni kwa sababu hawajawazoea mbwa, wameita kampuni ya ulinzi nayo ikashindwa kumwokoa mpaka polisi nao hakuweza kumwokoa mpaka walipolazimika kupiga mbwa wote wanne risasi. Lakini ikiwa hii kampuni wangejua namna ya kumwokoa mtu anayeshambuliwa na mbwa ilikuwa watume gari ya fire na siyo mobili crews ambao pamoja na bunduki zao hawakuweza kutoa msaada.
Kuna watu huwa wanajitengenezea mabomu nyumbani
 
mi ninavyopenda kuwapa kisago mbwa, sidhani kama huyo akiniletea za kuleta ataenda hadithia mbwa wenzio kama kakutana na chizi zaidi yake, kitu siogopagi maisha yangu ni mbwa.
Umezoea kukutana na mbwa koko mkuu!!! Tena futa kauli maana wewe nikikuchanganya kwenye banda la pitbull mmoja tu, dakika tano nyingi ushakuwa kitoweo.
 
Nikiona Hivi nasikitika....au aina hii ya Mbwa ndo walimuuma na marehemu mzee Kingunge???
 
Mkuu nafikiri kuna makosa ya kimatumizi maana kwa nijuwavyo hawa jamii hiyo ya mbwa huwa ni walinzi kwenye sehemu ambayo watu wanakuwa hawapo kwa muda huo.kama vile bank au mahali panapohifadhiwa vito vya thamani na huwa wanawekwa baada ya muda wa kazi na kuondolewa kabla ya muda wa kazi na watu maalumu na wenye mava,I maalumu, hawa ni moja ya jamii ya mbwa ambayo ni wakali sana na uwezi wao wa kupokea amri ni mdogo sana wao kazi yao ni kushambulia kilichoko mbele yao.
Mbwa hawa hufugwa na polisi na kampuni maalum za ulinzi na si watu binafsi,
kweli kiongozi hawa mbwa sio wa kufugwa na raia wa kawaida ni hatari
 
Kwaiyo mtu ameshambuliwa wameita vikosi vyote ivo na vikafika bado wanamshambulia tu kweli tz hali imebadilika watu wako chap haraka now days
Me mwenyewe niliwaza sana hapo ila sikuelewa kwamba;

1. Walioitwa walikuwa chap sana kuitikia wito

2. Mbwa walikuwa wakishambulia mdogo mdogo (by degrees)

3. Jamaa alijitahidi kupambana nao saana hivyo pambano likachukua kitambo kidogo

4. Hao watu waliitwa kwa pamoja na wote wakafika kwa ujumla wao

5. Kila watu walioitwa walipambana kwa muda mdogo (dakika chache) tu na kusalimu amri

6. Kila kundi lililoitwa lilitumia utaalamu wao kuwadhibiti (japo mwishowe likashindwa) na ndio maana ikafikia kuitwa watu wote hao

Au ni vipi!!?
 
Hahaaa mimi napenda pet dogs warembo warembo
Kwa company frenchbulldog ni wazuri sana
1605688519246.png
 
Back
Top Bottom