Nami nimejifunza funza masuala ya hawa mbwa, na kufahamu baadhi ya mambo, kutokana na ndugu yangu kufuga, na kufanya biashara ya hawa viumbe. Nimemjuw huyo GS, Pitbul BB, RW nk. Kuna watu wanakuja kununua mbwa mkubwa, jamaa anachofanya ni kumwambia mteja jina la huyo mbwa, na kumkabidhi mnyororo, na kuondoka naye. Wakati mwingine, anatumwa kutoka mji mmoja mpaka mwingine, na mnunuzi anaenda kumpokea, akiwa kwenye box. Ila, cha msingi uwe unafahamu ku deal na hao mbwa, na ulijue jina la huyo mbwa.