HiDEmYiD
JF-Expert Member
- Mar 14, 2018
- 1,893
- 3,640
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ndio maana nimesema yanipite. mnaoweza endeleeni hadi hao mbwa wawaueIshi unavoweza siyo unavotaka, kifupi kama huwezi hata kupata breakfast huwezi kununua huyo mbwa, kwani mdogo wa miexi miwili utahitaji laki 5 hivo si level yako
Tuibie siri sisi tusiofuga mbwa kakaHapo kwenye dagaa, changanya unga wa dagaa na pumba ya mahindi then mpikie uji mzito utakuja kunipa habari yake
Kwahio ukinunua suti mpya lazima ukamuoneshe kwanza au??Hao wanatumia macho kukutambua, sasa wewe njoo na suti ambayo hawajahi kuiona
Hilo jicho la mjani hilo.
Haya madude ndio yapo kwenye katuni ya TOM & JERRY?
Mbwa ana hadi wivu???? huyo ni mnyama pori tunayemlazimisha kuishi nae homeGerman shepherd ni mkali lakini mtiifu sana na anafundishika kirahisi, anapokea order mapema na hasau. Rott shida yake kubwa ni mgumu kufundishika na kigeugeu anaka kukumbushwa Mara kwa mara
KakaMkubwa... sikuwa na lengo la kukukomoa bali elimu uliyotoa imekaa poa na binafsi nimeipokea vizuri tu na ndomana hata comment zangu ukicheki nimeonelea ili kumwepuka mnyama huyo hatari basi bora kufuga wanyama wakali wa porini ujue moja tu kuliko kufuga mbwa anayetambulika ni wa nyumbani lakini masharti yake ni zaidi ya simba au zaidi ya mke mdogo!!!POINT to note:- Hakupambana bali alishambuliwa na kuangushwa chini kingeereza nitumie neno ( attacked and be mauled) Kampuni ya ulinzi kufika mapema inategemea walikuwa umbali gani na nyumba ya mteja wao ambako ndo tukio lilikotokea, walifika mapema na kujaribu kufyatua risasizipatzo tano hewani.
4. Hao watu waliitwa kwa pamoja na wote wakafika kwa ujumla wao:- hawakufika kwa pamoja kumbuka mtu wa kwanza kushindwa kuwacontrol mbwa ni handler mwenyewe ambaye ni mtunza bustani aliyewafungulia usiku, mmiliki wa nyumba baada ya kushuhudia tukio na kuomba msaada kwa kampuni ya ulinzi, kampuni ya ulinzi nayo ikashindwa na kuita polisi waliowapiga mbwa wote risasi, ( Technical know how)
Kifupi mimi nililenga kutoa elimu kidogo kusaidia wale wachache amabao wanamiliki ama wanampango wa kumiliki Rottweiler ni namna gani wafanye ili kudhibiti, nadhani maelezo zaidi ukihitaji utayapata polisi.
Na pia sikuwa eneo la tukio bali nilipigiwa simu na mtu aliyefika eneo la tukio na kwa kutambua ninafuga mbwa wa aina hiyo akataka kujifunza kitu kutokana na tukio zima. ila kwa utashi wangu nikajaribu kushare ninachokijua kutokana na hao mbwa kwa vile nimewatumia kazini kwa zaidi ya miaka kumi na kitu, na ninawafuga kwa zaidi ya miaka nane. nimekuwa wakizaa ninauza watoto na nawatumia kwa ulinzi. asante.
kwa akili yako timamu wewe unaweza kuuliwa na mbwa mmoja, hata awe mkali vipi[emoji848]Umezoea kukutana na mbwa koko mkuu!!! Tena futa kauli maana wewe nikikuchanganya kwenye banda la pitbull mmoja tu, dakika tano nyingi ushakuwa kitoweo.
wewe unaweza kupigwa na mbwa mmoja hata awe mkali vipi na ukashindwa kummudu?Wewe umepiga kina Bobi na Simba unajisifu umepiga mbwa.
Nimemaanisha kwenye banda ndanikwa akili yako timamu wewe unaweza kuuliwa na mbwa mmoja, hata awe mkali vipi[emoji848]
Mbwa mmoja asee hawezi niua atanijeruhi tu ila sio kunitoa uhaikwa akili yako timamu wewe unaweza kuuliwa na mbwa mmoja, hata awe mkali vipi[emoji848]
picha???Wana jamvi niwasalimu kwanza, na moja kwa moja niende kwenye mada.
Asubuhi ya leo nimepokea taarifa toka kwa rafiki yangu mmoja aliyeko Dar akitaka kufahamu kwa nini mbwa jamii ya Rottwieler hugeuka na kushambulia wamiliki na kufikia kuwaua. Hii ni kutokana na ukweli kwamba usiku wa kuamkia leo mbwa aina tajwa hapo wamemshambulia mpaka kumuua kijana mtunza bustani ambaye ndo alikuwa akiwatunza na kuwapa chakula.
PAMOJA na kuhitaji kupata ushauri tayari alikuwa ameconclude kuwa Rottweiler siyo mbwa wa kufugwa kitu ambacho mimi na kikataa kutoka na kwamba nimekuwa nikifuga jamii ya mbwa kwa miaka kadhaa, na hata ninapoandika bandiko hili ninao wanne, majike wawili na madume wawili.
JE, NI KWELI KWAMBA ROTTWEILLER NI HATARI SANA?
Jibu ni ndiyo, huyu mbwa anashikilia nafasi ya pili duniani hii ni kwa mjibu wa jarida la K-9 Dog day ya tarehe 26 August 2020, mbwa huyu anaguvu ya kung'ata ( PSI Pound per Square Inch or Pound-force per Square Inch 328 akiwa anakamata nafasi ya 12 dunia. Pamoja na hizo sifa hapo juu mbwa huyu bado kwangu ni mbwa rafiki endapo utakuwa naye karibu na kuonyesha unamjali sana, ( Kifupi ana wivu mnoooo ikiwa ulikuwa umezoea kucheza naye lakini ukabadilika na kuamishia mapenzi kwa kitu kingine kama paka, ng'ombe, mbuzi na hata mtoto Rottweiler anatabia ya kulipa kisasi, hata kama ni wao kwa wao ikiwa wako zaidi ya mmoja na wengine ukawa unawafungia kwenye kennel na mmoja ukamwacha free lazima huyu aliyeko free watamua tu.
Pia kama hauna muda wa kucheza nao kuwatembeza na kuwaruhusu kufanya mazoezi basi usifuge Rottweiler kwani kitakachofuata ni majonzi. Historia ya mbwa huyu inaenda mbali sana tangu zama za ufalme wa kirumi ambapo walitumika kusaidia wafugaji kuchunga mifugo na kuvuta mikokoteni. Kutokana na kuvuta mikokoteni mara nyingi mbwa hawa walivunjika mikia na ndo maana hata leo hii umekuwa kama utamaduni mara nyingi wamiliki wa hawa mbwa huwakata mikia.
NINI UFANYE KAMA UNAFUGA ROTTWEILER
Asubuhi kabla hujawaingiza bandani hakikisha unapata muda wa kuonana nayo cheza nao kidogo wafanyie groomimng, kisha waingize bandani na ikiwa unatabia ya kuwapa breakfast baada ya breakfast waache nje kwa muda ili wacheze, hakikisha una matoyi ya wao kuchezea kama vitenesi ( Napoongelea vitenesi nina maanisha vile ambavyo ni special kwa mbwa usinunue hivi vya kawaida make watatafuna na kumeza na hii inaweza kupelekea kifo. Nunua mifupa ile ya mpira wape waangaike nayo kwa muda kisha warudishe bandani.
Wafundishe utii kwa zile basic command kama ACHA, NJOO, INGIA NDANI. Tumia lugha hiyo kila siku.
KUWA NA MUDA MAALUM WA KUWAPA CHAKULA
Usiwaache na njaa muda mrefu na endapo umechelewa kuwapa chakula na ikawa tayari ni usiku kabla ya kuwafungulia jaribu kuvaa nguo walizozizoea na usijipulizie manukato. Ikiwa umewafungua banda anza na yule mkorofi zaidi akishatoka nje akiwa peke yake ni rahisi kumkontrol na hatimaye kukutambua tena. Baada ya hapo ndo ufungulie waliobaki. Endapo utawafungulia wote na ni usiku wakaona labda paka na kuanza kumfukuza ukijaribu kuwazuia wasiposikia usijaribu kuwapiga make tayari wana hasira na watakugeuka. Wazungu wanesema respect the power' Rottweiler is a loaded gun if not properly handled. Be Leader and not a boss to the breed.
Usiwaache wakuongoze bali uwaongoze ( These are dogs and they leave in packs ) wewe ndo uwe pack leader na si wao.
Usiache hawa mbwa kuhudumiwa na house boy au garderner muda wote, kama itabidi basi mfundishe namna ya kuishi na hawa mbwa.
NAWAPENDA ROTTWEILER
Kwa sababu najihisi salama zaidi kuliko mbwa mwingine yeyote, kwangu mimi wamewahi kumdhibiti mchawi saa nane usiku, na ikabidi yeye mwenyewe aombe msaada na kuonekana na kila mtu pale nyumbani usku.
UFANYE NINI
UKISHAONA MBWA WAKO WANAMSHAMBULIA MTU NDANI YA COMPOUND USITUMIE FIMBO BALI WAZUIE KWA ORDER YA MDOMO NA IKIWA HAWAKUSIKILIZI TUMIA MPIRA KUWA MWAGIA MAJI.
Nasema hivi kwa sababu huyu aliyeuliwa wamiliki na waajiri wameshindwa kumsaidia hii ni kwa sababu hawajawazoea mbwa, wameita kampuni ya ulinzi nayo ikashindwa kumwokoa mpaka polisi nao hakuweza kumwokoa mpaka walipolazimika kupiga mbwa wote wanne risasi. Lakini ikiwa hii kampuni wangejua namna ya kumwokoa mtu anayeshambuliwa na mbwa ilikuwa watume gari ya fire na siyo mobili crews ambao pamoja na bunduki zao hawakuweza kutoa msaada.
hao mbona niliwaona natty dogs kipindi fulani embu ingia kweny page yao instagram upitie utawaonaHawa jamaa nawaelewa Sana unambii chochote hapa namtafuta mnyama anaitwa Belgium Malinois huyu ndo hatari zaidi, bahati mbaya nchi nyingi zimempiga marufuku
huo uzi upo umu jukwaani nenda jukwaa la kilimo,uvuvi na ufugaji utaukutaMkuu nimekuelewa. Sasa labda nakuja kwako kununua GS au RW, Mimi ndio mara ya kwanza mbwa ananiona, hua mnafanyaje ili mbwa ambaye ndio anapewa mteja aweze kumzoea Siku hio.
**Mkuu kama hutojali kama utaweza kufungua thread kwa wale ambao tunapenda kufuga mbwa hao, mbinu, lugha za kutumia, vyakula, na mengineyo ya muhimu kwa aina zote za mbwa hao akina GS, RW, PB, nk
Picha gani unahitajipicha???
Furahisha jukwaa, mbwa wanaongelewa hapa akiwa mmoja anakuwa ndani ya dk 10 tu, akiamua.Mbwa mmoja asee hawezi niua atanijeruhi tu ila sio kunitoa uhai
tena mmoja asipoangalia ntamuua yeye yani nikidaka shingo siachiii
mpaka waje wasamaria wema kumuokoa,ntauliwa na mbwa watatu kuendelea
ila mbwa mmoja au wawili eti wanitoe uhai hiyo ngumu kumeza asee haitokaa itokee
kwa akili yako timamu wewe unaweza kuuliwa na mbwa mmoja, hata awe mkali vipi[emoji848]
Picha gani unahitaji
Furahisha jukwaa, mbwa wanaongelewa hapa akiwa mmoja anakuwa ndani ya dk 10 tu, akiamua.
picha???