Akirejelea tukio la Agosti 25, 2026 ambapo kijana mmoja alidaiwa kushambuliwa na mbwa watatu waliokuwa wakizurura kando ya Bara bara ya Katani Road, na kupata majeraha yaliyohitaji matibabu hospitalini pamoja na chanjo za kuzuia kichaa cha mbwa, Kavindu sasa anataka Seneti kupata maelezo kuhusu hali hiyo na hatua zinazochukuliwa kukabiliana na hatari inayoweza kutokea kwa wakazi, hasa kuhusu ugonjwa wa kichaa cha mbwa (rabies).
Hili si suala la usumbufu pekee. Rabies ni ugonjwa hatari unaoweza kuambukizwa kupitia kuumwa na mnyama aliyeambukizwa, na mbwa wamehusishwa kwa kiasi kikubwa na maambukizi ya rabies kwa binadamu.
Utafiti wa awali uliofanywa Machakos pia ulionyesha kuwa idadi ya mbwa katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji inaweza kuwa kubwa, jambo linaloonyesha kwa nini udhibiti wa mbwa wanaozurura ni suala la afya ya umma.
Sasa swali linaloibuka Syokimau ni: Mbwa hawa wanatoka wapi, nani anawajibika kuwakamata na kuwahifadhi, na ni hatua gani zinachukuliwa kuhakikisha wakazi hawako kwenye hatari ya rabies?
Kwa Seneti, hoja sasa iko mezani kwa Kamati ya Afya kupata majibu.