Mbwa kujisalimisha kwa chatu

Mbwa kujisalimisha kwa chatu

Hizo ni Story za Vijiwe vya Kahawa, Iko hivi Mbwa hajisalimishi kwa Chatu Bali huwa wanaenda kumshangaa chatu hasa Magamba yake, na pale kama Chatu ana njaa basi hukamata mmoja, Hata nyoka wa kawaida mbwa ana tabia ya kwenda kumnusa nusa na hicho ndio kinacho tokea kwa Chatu pia.

Mbwa mwitu wao wana mafunzo ya asili wakimuoana Chatu tiyari wanajua ni adui na hawawezi enda kunusa nusa.

Kama eneo ulipo lina Chatu na una Mwmbwa siku una muona Chatu ita Mbwa wako, then angalia wanacho fanya, wataenda Direct kuanza kumnusa nusa na huwa hawajui kama yule ni adui na anaweza wameza,
Huu ndo ukweli zingine huwa ni porojo
 
Ukiacha harufu tatizo ni kwamba mboni za macho ya mbwa zikiangaliana na mboni za macho ya chatu mbwa hulegea na hawezi kuondoka, ila mtu akimrushia kitu kama jiwe na kumpiga huyo mbwa ata shtuka na kuondoa macho kwa chatu na kukimbia. Tuwe na utamaduni wa kutembelea snake park zetu tutajifunza mengi sana.
Hahaaa, Isha jibiwa hapo juu, Mbwa hajui kama kama Chatu ni adui yake na yeye huwa anaenda kumnusa basi na katika maadui zake chaymtu hayumo make maadui anajua ni wanyama kama yeye
 
Kama kuna vichaka choma moto kuzunguka eneo lako kwanza ili ufukuze wanyama hatari halafu ndio ufuge hao mbwa.

Kuhusu suala la mbwa na chatu hilo lipo mbwa huwa anajipeleka mwenyewe hata kama chatu yupo kwenye kichaka
 
hivo vichaka ni maeneo ya watu ambao huwa wazito sana kutunza maeneo yao.
 
Halafu ajabu ni kwamba mbwa anamezwa huku anatingisha mkia Kwa furaha.

Mbwa na chatu wanajuwana vizuri tu,
Wala tusiingilie mipango yao.
 
Habari za muda huu wakuu, hongereni kwa mapambano ya usiku na mchana kuendelea kuifanya nchi yetu na dunia kwa ujumla kuwa sehemu bora na salama.

Iko hivi, nina mpango wa kufuga mbwa shambani kwa sababu sio siku nyingi nitaweka mifugo mingi kiasi lakini bado hakuna uzio(fence), sasa kuna jamaa yangu kaniambia kwamba nitakachokifanya itakuwa ni kutwanga maji kwenye kinu kwani mbwa huwa wana kawaida ya kujisalimisha wenyewe kwa chatu kwa ajili ya kumezwa(kuna vichaka vingi na vikubwa maeneo yanayolizunguka shamba). Hii ina ukweli wowote?

Kama ishu ni aina ya mbwa na mafunzo ni kwamba ninafikiria kati ya boerboel, GS au Doberman pinscher na nitawagharamiamafunzo.

Ushauri wenu tafadhali [emoji120].
Hawajisalimishi huwa wanamkazia au kumdindia chatu hata kama wanamuogopa. Mbwa wanatabia ya kuwa loyal kwa master wao.

Wakipewa eneo kulinda huwa wanasimamia wajibu wao hata kama kuna hatari mbele yao.

Kimsingi anachofanya mbwa ni kumkazia chatu sasa ikitokea yupo mbwa m'moja huwa anazidiwa timing ikitokea chatu kamuotea na kumkamata. Ila mbwa huwa wanafukuza sana chatu na wanyama wengine kwa kuwabwekea.

Wazungu huwa wanapenda sana mbwa kwa sababu hiyo.

Fuga wengi halafu chatu akosee aingie kwenye kumi na nane utakuja kujionea mzoga wake asubuhi namna watamlia mingo na kumshambulia kwa mtungo.

Jambo lingine chukua oil chafu changanya na mafuta ya taa kiwango kikubwa. Mfano, dumu la lita 20 la oil chafu changanya na lita 5 hadi kumi za mafuta ya taa kisha weka na chumvi hata pakti tano. Mwaga maeneo yote kuzunguka eneo lako unalotaka kulinda, chatu akinusa hatosogea hilo eneo. Mafuta ya taa na chumvi plus oil chafu ni adui mkubwa sana kwenye ngozi ya nyoka inamchana kama acid.
 
  • Thanks
Reactions: PYD
Kuna wengine wanasemaga ukihisi harufu ya viazi kwenye kichaka basi ujue hiko kichaka kina chatu [emoji23][emoji23]

Shikamoo vijiwe vya kahawa [emoji119]
Kuna majani huwa yananukia hivyo. Chatu anatoaje harufu ya viazi mviringo vya kuchemza? Akiachia ushuzi au?
 
Wee jamaa acha chai
Mkuu fuatilia Sana video za mbwa kuliwa na chatu.
Mbwa analiwa huku anatoa sauti ya manung'uniko lakini anachezesha mkia Kwa furaha.

Wanajuwana vizuri tu.
 
Chatu ana harufu ya nyama huwa anatoa mdomoni sasa mbwa huwa anajisogeza akidhania chatu anatapika nyama hapo ndio mwisho wake
Mhhhhhh..... harufu ya nyama tena?mbona hatujawahi kusikia chatu kumkamata Paka sababu paka nae ni mpenzi pia wa nyama nyama 🤔
 
Habari za muda huu wakuu, hongereni kwa mapambano ya usiku na mchana kuendelea kuifanya nchi yetu na dunia kwa ujumla kuwa sehemu bora na salama.

Iko hivi, nina mpango wa kufuga mbwa shambani kwa sababu sio siku nyingi nitaweka mifugo mingi kiasi lakini bado hakuna uzio(fence), sasa kuna jamaa yangu kaniambia kwamba nitakachokifanya itakuwa ni kutwanga maji kwenye kinu kwani mbwa huwa wana kawaida ya kujisalimisha wenyewe kwa chatu kwa ajili ya kumezwa(kuna vichaka vingi na vikubwa maeneo yanayolizunguka shamba). Hii ina ukweli wowote?

Kama ishu ni aina ya mbwa na mafunzo ni kwamba ninafikiria kati ya boerboel, GS au Doberman pinscher na nitawagharamiamafunzo.

Ushauri wenu tafadhali [emoji120].
NI KWELI KABISA, IKO HIVI..

CHATU AKISHAMUONA AU KUHISI KUWA KUNA MBWA HUTOA HARUFU NZURI SANA. INAYONUKIA NA KUMVUTIA MBWA. MBWA HUMSOGELEA CHATU KWA LENGO LA KWENDA KULA MZOGA. MBWA HUAMINI KUWA HUO NI MZOGA.WAKATI HUO CHATU HUTULIA KAMA VILE AMEKUFA NA KUENDELEA KUTEMA ILE HARUFU KUPITIA NJIA YA HAJA NA MATUNDU YA PUA, BAADA YA MBWA KUSOGEA KARIBU KABISA CHATU HUMGEUZIA KIBAO MBWA NA KUMVIRIGA NA KUMUUA KISHA KUMMEZA. MBWA ANAPOKOSA UHAKIKA WA ANACHOKIFANYA AU ANAPOONA KUWA AMESHINDWA HUKUNJIA MKIA TUMBONI LAKINI ANAPOKUWA NA UHAKIKA NA ANACHOKIFANYA AU KUKIMBIZA HUINUA MKIA JUU. MBWA ANAPOMSOGELEA CHATU HUKUNJIA MKIA TUMBONI KAMA ISHARA YA KUTO KUWA NA UHAKIKA WA ANACHOKIFANYA.
TENDO AMBALO HUMGHARIMU.

HII NI SAWA NA KUSEMA

UNAMDANGANYA DADA WA WATU NJOO GHETO MALARIA YAMENIKAMATA SANA. HATA KULA WALA KUOGA SIWEZI

AKIJA UNAMGEUZIA KIBAO NA KUMTAFUNA.
 
Habari za muda huu wakuu, hongereni kwa mapambano ya usiku na mchana kuendelea kuifanya nchi yetu na dunia kwa ujumla kuwa sehemu bora na salama.

Iko hivi, nina mpango wa kufuga mbwa shambani kwa sababu sio siku nyingi nitaweka mifugo mingi kiasi lakini bado hakuna uzio(fence), sasa kuna jamaa yangu kaniambia kwamba nitakachokifanya itakuwa ni kutwanga maji kwenye kinu kwani mbwa huwa wana kawaida ya kujisalimisha wenyewe kwa chatu kwa ajili ya kumezwa(kuna vichaka vingi na vikubwa maeneo yanayolizunguka shamba). Hii ina ukweli wowote?

Kama ishu ni aina ya mbwa na mafunzo ni kwamba ninafikiria kati ya boerboel, GS au Doberman pinscher na nitawagharamiamafunzo.

Ushauri wenu tafadhali [emoji120].
Chatu huwa sio tu anajisalimisha,huwa anajisalimisha huku anajua kinachoenda kutokea,maana mmbwa huwa anatoa ile sauti ndogndogo ya maumivu huku kaficha mkia,sie tuliochunga ukiona mmbwa nyuma yako anagugumia unageuka chap kukagua..mita chache unamuona chatu..basi unamuokoa kwa kumkata na panga au unamchinja huyo chatu.

Sio story za vijiweni ni kweli,mmbwa kwa chatu ni fala...!
 
Back
Top Bottom