Mbwa wana uwezo wa kuwaona Wachawi?

Mbwa wana uwezo wa kuwaona Wachawi?

Verified

Senior Member
Joined
Apr 11, 2013
Posts
117
Reaction score
377
Wasalaam ndugu wana JF

Kwa almost miaka 12 iliyopita, ninaishi katika eneo ambalo inasemekana lina mauza uza japo binafsi sikuwahi kuyaona kwa macho, ingawa nishaua wanyama ambao wamekuja kiajabu ajabu mara nyingi sana kama nyoka, ndege n.k

Katika eneo langu, ninafuga Mbwa, ninao mbwa 5, walioshiba vizuri, nimeona nilete uzi huu kuwauliza wataalam wa hizi fani kwamba ni kwa jinsi gani jambo hili linawezekana.

Kwa karibia week nzima mfululizo, mbwa wangu wamekua wakibweka sana kama wameona kitu kila ifikapo saa 8:17 usiku (2:17 AM), yaani mara zote ambazo nimeshtushwa na kubweka kwa mbwa, kila nikiangalia saa ni saa nane na dakika 17 usiku, jambo hili limenifilirisha na kujiuliza, inakuwaje muda na dakika uwe ni ule ule mara zote mbwa wanapobweka kwa nguvu kama wameona kitu?
 
Wasalaam ndugu wana JF

Kwa almost miaka 12 iliyopita, ninaishi katika eneo ambalo inasemekana lina mauza uza japo binafsi sikuwahi kuyaona kwa macho, ingawa nishaua wanyama ambao wamekuja kiajabu ajabu mara nyingi sana kama nyoka, ndege n.k
Basi wachawi wako very punctual. UMUGHAKA na mpenzi wake Monica, pia adui yao Mzee MAKONO watuambie, je mbwa anaona wachawi? Au wachawi hawaoni mbwa?
 
Screenshot_20221101-220324_WhatsAppBusiness.jpg
 
Machimbo nishayakutajia ndugu. Duka la nguo linakufa ila dula la dawa za asili linadunda miaka nenda rudi 😅 vilinge ni konyo
 
Ahundred perce mbwa wanaona vitu vingi katika ulimwengu wa roho. Mbwa wa nyumbani kwangu na wajirani huwa wanalia kwa kulalamika kila muda wa adhana ya msikitini unapofika. Nilimuuliza shekhe mmoja nguli hapa Dar mahusiano ya mbwa na adhana akaniambia wazi kuwa mbwa wanawaona majini wanaokuwa wanaenda misikitini kuswari.
 
Kuhusu kutokea kwa matukio hasa kwa muda unaofanana richa ya siku kuwa tofauti,
Mimi ni shuhuda wa hili,
nilikuwa nastuka na ndoto za ajabu halafu muda unafanana na ule niloamka jana.
 
Nenda pale kkoo shimon karibu wanapo uza matoyo wanauza dawa za asili ukipita uwo mtaa harufu flan za tokukera mpaka kichea kuuma ulizia, au nenda vingunguti kwa mnyamani maduka yamejaa tele
Ukiona umepita sehem ka hiyo kichwa kikuume basi kama utakua na jini
 
Ahundred perce mbwa wanaona vitu vingi katika ulimwengu wa roho. Mbwa wa nyumbani kwangu na wajirani huwa wanalia kwa kulalamika kila muda wa adhana ya msikitini unapofika. Nilimuuliza shekhe mmoja nguli hapa Dar mahusiano ya mbwa na adhana akaniambia wazi kuwa mbwa wanawaona majini wanaokuwa wanaenda misikitini kuswari.

Duh, mkuu kama hutojali muulize Sheikh, Je hao majini wanaenda kwenye misikiti hii hii ya wanadam au wana misikiti yao? Na kama ni hii hii ni kwa nini wasiwe na ya kwao wategemee misikiti inayojengwa na wanadam?
 
Back
Top Bottom