Mbwana Matumla akamatwa na madawa ya kulevya Spain.

Hawa sheria ile kwao tu wamezidi kujifanya wao ndo wanaijua pesa alafu wakija hapa wanajifanya kusumbua sana mitaani.
 
hivi watu hawakomi au njaa au nin! wenzio wanadakwa daily we bado unajigeuza punda.
 
Duh huyo mwanangu mwenyewe Mbwana M mara ya mwisho tunaachana Mkoani Moro kata ya Mgeta kijiji cha Kikeo tulikuwa Camp mgodini na wana kibao au ameona madini hayalipi?
 
Duh huyo mwanangu mwenyewe Mbwana M mara ya mwisho tunaachana Mkoani Moro kata ya Mgeta kijiji cha Kikeo tulikuwa Camp mgodini na wana kibao au ameona madini hayalipi?

Wewe sema hayo madili yanalipa na kama ndio mbona hata baiskel huna?
 
Ukijaribu kuconnect dots utakumbuka kuna kipindi yule kiongozi wa chama cha ngumi nae alidakwa na ngada thou sijajua hatma yake ilikuaje.
 
Wakamatwe kwa kosa gani lenye ushahidi? Hebu tuacheni, kamateni punda!

Hahahah...ukifuatilia sheria za baadhi ya nchi wenyewe wana deal na wale drug lords tu
 
Maisha wanayatafuta kienyeji sana

Nyakati hubadilika lakini wao hawataki
kubadilika ni kubeba sembe tu.
 
ahh huyu jamaa si ni police au aliacha IGP kazi unayo.police kawa punda



Kipaji chake cha ngumi kilichoanza kuonekana tangu akiwa kinda akirithi kutoka kwa baba na kaka zake, kilimwezesha Mbwana Matumla 'Golden Boy' kupata ajira bila kutarajia ndani ya Jeshi la Polisi mwanzoni mwa miaka ya 1990. Bondia huyo maarufu aliyeshikilia taji la Ubingwa wa Mabara wa UBO, uzani wa Superfly, alivutwa Polisi tangu akiwa yupo darasa la tano katika Shule ya Msingi Mgulani. Alisema alichukuliwa na Polisi ili kuichezea timu yao na ngumi na alipomaliza masomo yake ya msingi alipewa ajira mwaka 1993.

Miaka miwili baadae alipelekwa kwenye shule ya uaskari ili kuwa askari kamili, wakati ambao alikuwa tayari alishaisaidia timu hiyo kutamba katika ngumi, huku mwenyewe akijijengea jina anga za kimataifa. "Huwezi amini niliajiriwa Polisi kama utani baada ya kuwavutia kwa kipaji changu, nakumbuka nilichukuliwa nikiwa darasa la tano, lakini niliajiriwa mwaka 1993 kabla ya kupelekewa 'depo' mwaka 1995," alisema.

Mbwana, aliyetwaa mataji mbalimbali katika ngumi za ridhaa akiwa na Polisi na timu ya Taifa, alisema hata hivyo alilazimika kuacha ajira jeshini mwaka 1997 baada ya kushawishiwa kuingia katika ngumi za kulipwa zilizompa mafanikio zaidi kimaisha. "Niliacha kazi Polisi mwaka 1997 na kutumbukia kwenye ngumi za kulipwa kwa ushawishi wa kocha, Norman Hlabane, wa Afrika ya Kusini, aliyekuwa akimnoa kaka Rashid, ndiye aliyenipa hili jina la 'Golden Boy' kwa kukunwa na ukali wangu," alisema.

Mbwana, alisema alipanda ulingoni kwa mara ya kwanza katika ngumi za ridhaa katika michuano ya wazi na kumpiga Abdul Mgweno aliyeichezea klabu ya Urafiki. Aliendelea kutamba akiwapiga wapinzani wake na kuteuliwa kwenye timu ya taifa, ambapo aliisaidia kuiletea sifa Tanzania kwa kutwaa medali kadhaa kwenye michuano mbalimbali kabla ya kuhamishia makali yake kwenye ngumi za kulipwa.

Mbwana alilitaja pambano la kwanza kwa ngumi za kulipwa kwake lilikuwa dhidi ya Mussa Njeu aliyempiga kwa KO, raundi ya kwanza na kuingia moja kwa moja kwenye orodha ya mabondia wa Kanda ya Tano mwaka huo wa 1997. Taji la kwanza kimataifa kwake ni mkanda wa WBU-International alipomchakaza kwa KO ya raundi ya kwanza bondia wa Hungary, Tamas Szakallas, katika pambano lililofanyika Tanzania, Desemba 19, 1998. Mataji mengine aliyowahi kutwaa ni WBA, WBN, PABA, WBU, ICB, IBO na UBO anaoushikilia hadi sasa ambapo aliutwaa mara ya kwanza mwaka 2009 kwa kumpiga Mganda, Festus Omondi, na kutetea hivi karibu mbele ya Mkenya Gabriel Ochieng.

Mbali na mikanda hiyo, Matumla, ambaye ni mnazi mkubwa wa timu ya Simba na klabu ya Manchester United ya Uingereza iliyofungwa 3-1 na Barcelona katika fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa usiku wa kuamkia jana, amewahi kutwaa tuzo mbalimbali ikiwemo ile ya Mwanamichezo Bora inayotolewa na TASWA mwaka 1993 na 1998, Shujaa wa Taifa mwaka 2000 na ile ya Guinness Book.

Mbwana aliyelitaja tukio la kupata mtoto wa kiume (Yusuf) kuwa ndilo la furaha mwake, alisema kucheza kwake ngumi kumemsaidia mengi kama kujenga nyumba mbili, kumiliki kiwanja Ukonga, jijini Dar es Salaam na kuendesha shughuli za biashara. "Pia, nimeijua dunia kupitia ngumi, nina marafiki wengi, kifupi ngumi zimenisaidia sana," alisema.

Mbwana anayependa kula ndizi kwa nyama na soda aina ya Fanta, alisema mchezo wa ngumi nchini umedorora sasa kwa kuwepo migogoro na kukosekana kwa wadhamini, akidai angekutana na Rais hicho ndicho kingekuwa kilio chake kwake. "Ngumi zimetelekezwa licha ya kuitangaza nchi kwa kutoa mabingwa wa dunia, hivyo ningemuomba Rais asaidie ziwe na wadhamini kama alivyofanya katika soka," alisema.

Na kama yeye Mbwana angekuwa angekuwa Rais wa nchi hii, angeboresha huduma zote za jamii, akihakikisha rasilimali za nchi zinasaidia kuinua uchumi kuwanufaisha wananchi wote, pia kusaidia kuinua michezo ili kusaidia ajira kwa wengi. Mbwana anayekunwa na Floyd Mayweather Jr. kwa umahiri wake wa kutupa ngumi ulingoni, amepanga kustaafu ngumi miaka mitano ijayo ili awe kocha wa mchezo huo. "Nimepanga kustaafu miaka mitano ijayo niwe kocha kuinua nyota wapya, tayari nimeshaianza kazi hiyo nikishirikiana na kaka Rashid."

Mbwana Ally Matumla, alizaliwa Aprili 8,1975, Dar es Salaam. Ni mtoto wa tano kati ya watoto 11 wa Mzee Ally Matumla, alisoma Shule ya Msingi Mgulani na kujihusisha katika michezo hasa soka, sarakasi kabla ya kugeukia ngumi hadi leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…