UZUSHI WA MBWANA MATUMLA KUNASWA NA UNGA HISPANIA WAWASHANGAZA WENGI
Wiki iliyopita ilihitimika kwa redio moja kutangaza habari kwamba mmoja wa wanafamilia ya mzee Matumla, Mbwana Matumla amenaswa na unga nchini Hispania na kuwashangaza wengi.
Watu waliozungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki walisema kwamba walishangaa kusikia habari hiyo huku wakiwa wanamwona Mbwana mitaani.
Sasa huyu kakamatwa Hispania huku tukiwa tunamwona mitaani, maana yake nini jamani? Alihoji msomaji wetu mmoja na kuongeza kwamba, yeye alikutana na bondia huyo siku tano nyuma.
Ijumaa Wikienda lilimsaka Mbwana kwa njia ya simu yake ya mkononi bila mafanikio, lakini lilipomtafuta kaka mtu, Rashid Matumla, Jumamosi iliyopita alisema Mbwana amejaa tele nyumbani kwake, Gongo la Mboto, Dar.
source Global Publisher