Nadhani mbali na kufanya vizuri uwanjani, kama ulivyosema yampasa Samatta kuangalia namna gani anafungua milango na kutengeneza njia kwa ndugu zake aliowaacha huku ila nao wapate kujongea kunako ulimwengu wa kwanza wa michezo.
Na wala hili siyo ombi bali ni wajibu wake ambao amejibebesha mwenyewe mabegani mwake (kwa kupambana ha hatimaye kutoboa).
Kuna namna nyingi Samagoal anaweza saidia wadogo zake ikiwemo kuanzisha shule ya soka/michezo yaani academy. Naamini muda si mrefu Maestro huyu atakuwa kwenye nafasi ya kufanya hivyo. Mbali na kusaidia wadogo zake, kwa kujenga academy hata yeye atakuwa amefanya uwekezaji mkubwa utakaomnufaisha yeye na wanaomzunguka.
Sent using
Jamii Forums mobile app