Mbwana Samatta aanza kusugua benchi KRC Genk

Mbwana Samatta aanza kusugua benchi KRC Genk

Kinumbo

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2019
Posts
3,039
Reaction score
5,560
Mshambuliaji na Nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta hali imeanza kuwa tete katika klabu yake ya KRC Genk. Hii ni kufuatia kupigwa benchi mara mbili mfululizo katika mechi za ligi.

Mechi ya kwanza ilikuwa nyumbani pale KRC Genk walipo ikalibisha Waasland Beveren, katika mechi hiyo Samatta alianzia benchi kisha dakika ya 74 akaingia.

Mechi ya pili ni hapo jana tarehe 22. RSC Anderlecht waliikalibisha KRC Genk katika uwanja wao wa nyumbani. Kama kawaida Samatta alianzia benchi Kisha kupata nafasi ya kucheza dakika ya 63. RSC Anderlecht ilishinda kwa magoli wawili kwa bila.

Nafasi ya Mbwana Samatta imechukuliwa na Mnigeria Poul Onuachu.

Je, kwa hatua ni kuonyesha kwamba kiwango cha Mbwana Samatta kimeshuka ama ni mbinu za Mwalimu?
 
Wewe ni nani mpaka umpangie mwalimu mchezaji wa kuanza kikosi cha kwanza? Kwani hiyo Genk ina mchezaji mmoja tu, Mbwana Samata? Kwani kuanzia benchi kwa mchezaji mahiri kama yeye, kuna tatizo gani?

Vipi kama mwalimu anampumzisha kwa sababu ya uchovu (fatique) ya kucheza mechi nyingi?
 
Huyo kocha mpya hovyo Sana, unawezaje kumuweka Samatta nje kwenye mechi ngumu Kama hiyo?
Wakati Liverpool kawafunga Nyumbani na 'ugenini' ?
 
Kocha aliyekuwepo katimuliwa,maranyingi kocha mpya lazima aanze kutengeza timu upya na maranyingi wachoma mahindi huwa wanakiwasha kwa hasira kumprove kuwa kocha aliyepita alikuwa anakosea. Wachoma mahindi huwa wanafaulu au kufail, dogo atacheza tu. Agent wake afanye asepe pale.
 
Ki ukweli Samatta ni mzigo, sijui alifikaje hapo Genk. Nahisi nguvu za giza ndio zilizo msaidia.

Ila uwanjani ni mweupe sana. EPL hawezi cheza kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Siku zote wasiojua ndio wanawaona wanaojua hawajui, wewe hujui mpira ila unaona mpira tu ukipigwa na ndio maana unashangaa kwanini Samata yuko Genk ila hushangai kama Samata hajui iweje wewe upo JF ukicheza mpira kwa mdomo na Samata akicheza mpira Genk kwa miguu yake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbuka alikua captain..
Wewe ni nani mpaka umpangie mwalimu mchezaji wa kuanza kikosi cha kwanza? Kwani hiyo Genk ina mchezaji mmoja tu, Mbwana Samata? Kwani kuanzia benchi kwa mchezaji mahiri kama yeye, kuna tatizo gani?

Vipi kama mwalimu anampumzisha kwa sababu ya uchovu (fatique) ya kucheza mechi nyingi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom