Mbwana Samatta ajiunga na Klabu ya Havre Athletic Club ya Ligue 1

Mbwana Samatta ajiunga na Klabu ya Havre Athletic Club ya Ligue 1

Aisee! Dogo ana nyota ya kipekee sana. Yaani amecheza Afrika, amecheza Ubelgiji, amecheza Uingereza, amecheza Uturuki, amecheza Ugiriki, na sasa Ufaransa! Na kote huko anacheza timu za ligi kuu tu!!

Hongera nyingi kwake.
 
Mzee kazuyoshi miura BADO anasakata kabumbu na vijana. Samatta hapa anazidiwa miaka ya kutosha
 

Attachments

  • Screenshot_20250805-190821.png
    Screenshot_20250805-190821.png
    730 KB · Views: 42
Nilikuja na project Fulani ya kujenga hoteli pamoja na uwanja WA mpira hapohapo hotelini. Uwanja unakuwa ni pitch TU haiusishi majukwaa na mambo mengine, kwa nchi yetu fursa BADO kibao. Case study ULIKUA uwanja WA karatu WA rhino rangers Kuna WATU hawakuona HIYO fursa, ila amini usiamini, KLABU ya Azam nayenyewe imeweka kambi HAPO pre season, ni SIKU chache TU baada ya michuano ya cecafa kufanyikia HAPO.



Kwishaaaaa
 
The one and only Tanzanian son who make us proud. Huko akiwashe sana, all the best Captain Diego💪
 
Wikipedia inatuambia ana miaka 34.
Kwanza hata umri huo bado ni questionable.

Samatta ni mkubwa kwa chama....Samatta ni mkubwa kwa kapombe, Samatta ni mkubwa kwa Zimbwe...Samatta ni mkubwa kwa Thomas Ulimwengu.

Aliocheza nao Mazembe wamestaafu wote.....wakiwemo wa rika lake.

Samatta alicheza Simba 2010/11
Je mchezaji gani aliyekuwa akicheza Simba au hata Yanga wakati huo ambaye bado anacheza hadi leo?

Samatta amekwenda ulaya akiwa amechelewa....Nitajie mchezaji yeyote uliyemwona 2010 akiwa Manchester united, Arsenal, Mamelodi, Mtibwa, Simba au Yanga ambaye anacheza hadi leo 2025/26 season.
Ronaldo na messi wanacheza tangu 2000 huko, kuna pirlo kuna buffon, uwezo wanakuwa nao sema klabu haziwaamini tu
 
Kipaji,kujituna,malengo na nidhamu ndio vinakufanya ufanikiwe,

Hakuna cha Nyota wala Mwezi,
Yani mtu huna kipaji wala hujitumi halafu team za Europe zikuchukue kisa Nyota?
Hizo team za Europe hiyo Nyota hua wanaionea wapi zaidi ya kuangalia Kipaji cha mchezaji?
 
Back
Top Bottom