Mbwana Samatta akiwa majaribioni CSKA Moscow

Mbwana Samatta akiwa majaribioni CSKA Moscow

Joined
Jan 12, 2015
Posts
55
Reaction score
19
43e00d1a50be906012571d9c0e140c09.jpg



MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, amezidi kugeuka lulu kwa timu za Ulaya baada ya matajiri wa Urusi, CSKA Moscow nao kuonyesha nia ya kumsajili katika dirisha dogo linalomalizia usajili.

Samatta aliyeondoka nchini mwishoni mwa wiki kuelekea Hispania kufanya mazungumzo na moja ya timu ya huko inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga', sasa amekutana na zali jingine nchini humo baada ya CSKA nayo kumfukuzia.

Mtoa habari wetu aliyekaribu na Samatta amelipasha MTANZANIA kuwa CSKA imeridhishwa na kiwango cha Samatta na inataka kumsajili kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Urusi.

"CSKA kwa sasa ipo Hispania kwa ajili ya kambi ya mazoezi kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi yao. Walikuwa wanamfuatilia kwa muda mrefu hivyo wanaona hivi sasa ni muda sahihi kwao wa kumsajili," alieleza.

Mbali na timu kutoka Hispania na Urusi zinazomwania, chanzo hicho kilieleza kuwa Samatta anatakiwa na timu nyingine za Italia na Uswisi, huku timu mbili kati ya hizo nne kutoka mataifa hayo zikiwa ni washiriki wakubwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kila mwaka.

"Watanzania wasiwe na wasiwasi, taarifa njema ya Samatta inakuja muda si mrefu na itajulikana anakwenda Urusi, Hispania, Uswisi au Italia," alieleza.

"Kwa sasa yupo Hispania na jana alitarajia kuanza mazoezi na moja ya timu hizo, watamuangalia mara ya mwisho kabla ya mazungumzo ya pande zote kuanza kisha kufanyiwa vipimo vya afya na kusajiliwa rasmi."
CSKA iliyotolewa kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu ikiwa na Bayern Munich, AS Roma na Manchester City (Kundi E), kwa sasa inashika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Urusi kwa pointi 34, huku Zenit yenye pointi 41 ikiwa kileleni.

Kama Samatta atafanikiwa kujiunga na matajiri hao wa Urusi, anaweza kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao na kuwafikia wachezaji wengine wa Afrika Mashariki kutoka Kenya, Mackdonald Mariga (wakati akiwa Inter Milan) na Victor Wanyama (wakati akiwa Celtic).

Samatta alijiunga na TP Mazembe akitokea Simba mwaka 2011, kwa sasa amebakisha mkataba wa mwaka mmoja ndani ya timu hiyo inayomilikiwa na mfanyabiashara Moise Katumbi.

1b1932fa6bfb1b4297dd86632a5114b4.jpg
188fce2bb39f93ae049c7cb5b9146f2a.jpg



AISEE BAD News hapa....

Friendly Match. CSKA Moscow - Sion. Video broadcast
01/21/15
January 21 CSKA Moscow will hold the first friendly match in preparation for the second half of the season 2014/15. Rival red and blue will be the Swiss "Sion."


CSKA: Akinfeev, Fernandez, V. Berezutski, Ignashevich, Nababkin, Vernblum, Nath, Tosic, Eremenko, Dzagoev, Musa.


In today's and tomorrow's match will not be able to attend several players CSKA Moscow. George Shennikov unwell, Georgi Milanov felt discomfort in the hip adductors and Svetoslav St George and Dmitri Efremov were damaged at yesterday's daily workout. Both players will travel to Moscow for medical examination depth. Also yesterday, the ankle injury was located on the viewing Mbavana Samatta, who apparently also miss both friendlies.


The meeting will be held in the Spanish San Pedro del Pinatar on the Pinatar Arena. Beginning at 14:00 Moscow time.
 
PFC CSKA MOSCOW @PFC_CSKA_MOSCOW



На просмотре в ПФК #ЦСКА находится танзанийский форвард Мбвана #Саматта, который тренируется вместе с командой. pic.twitter.com/ZChXG9YkyI

Translation in English "
On view in PFC CSKA is # Tanzanian forward Mbvana # Samatta, who trains with the team."

Source: http://en.pfc-cska.com
 
Hongera sana mkuu Samatta uzidi kubarikiwa mapaka uko majuu wapige saluti kwa mtoto wa kibongo .
 
Last edited by a moderator:
Ukicheza Simba kwa Tanzania ni rahisi sana kufika Mbali kimpira… labda uharibu mwenyewe kama…
Yule Anduje Ngasa kipindi ameenda kufanya Majaribio pale Kwa Wagonga nyundo wa London "WestHam Utd" angekuwa ametokea Simba leo hii tungekuwa tunaongea vingine kuhusu yeye…
 
ukicheza simba kwa tanzania ni rahisi sana kufika mbali kimpira… labda uharibu mwenyewe kama…
yule anduje ngasa kipindi ameenda kufanya majaribio pale kwa wagonga nyundo wa london "westham utd" angekuwa ametokea simba leo hii tungekuwa tunaongea vingine kuhusu yeye…
sio kweli acha mahaba niue wewe simbwa
 
Ukicheza Simba kwa Tanzania ni rahisi sana kufika Mbali kimpira… labda uharibu mwenyewe kama…
Yule Anduje Ngasa kipindi ameenda kufanya Majaribio pale Kwa Wagonga nyundo wa London "WestHam Utd" angekuwa ametokea Simba leo hii tungekuwa tunaongea vingine kuhusu yeye…



mchezaji gani toka mikia ambaye amewahi kucheza premier league ulaya toka JK aingie madarakani?
 
Ukicheza Simba kwa Tanzania ni rahisi sana kufika Mbali kimpira… labda uharibu mwenyewe kama…
Yule Anduje Ngasa kipindi ameenda kufanya Majaribio pale Kwa Wagonga nyundo wa London "WestHam Utd" angekuwa ametokea Simba leo hii tungekuwa tunaongea vingine kuhusu yeye…

Kweli hata Nonda Shaaban alichezea Simba!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ukicheza Simba kwa Tanzania ni rahisi sana kufika Mbali kimpira… labda uharibu mwenyewe kama…
Yule Anduje Ngasa kipindi ameenda kufanya Majaribio pale Kwa Wagonga nyundo wa London "WestHam Utd" angekuwa ametokea Simba leo hii tungekuwa tunaongea vingine kuhusu yeye…

Haya mahaba yenu ya kijinga ndo maana hamna maendeleo, Haruna Moshi Boban, Seleman Matola, Henry Joseph, Shomari Kapombe, Emmanuel Okwi, n.k wamechezea timu gani na wako wapi wakifanya nini? HAPA NI MCHEZAJI KUJITAMBUA kama angekalia kuvuta mibhangi kama hao wenzake hakuna kitu!!!!
 
Back
Top Bottom