Mbwana Samatta awachoka Watanzania wakorofi mtandaoni, awataka kuacha maneno ya kashfa

Mbwana Samatta awachoka Watanzania wakorofi mtandaoni, awataka kuacha maneno ya kashfa

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Samatta awachoka Watanzania wakorofi mtandaoni

Mshambuliaji wa klabu ya Aston villa na timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mbwana Samatta ameeleza masikitiko yake kufuatia maoni yasiyoridhisha ya Watanzania katika mitandaao ya kijamii.

Sama11.jpg

Samatta amesema hayo kufuatia Watanzania kutoa maoni yasiyoridhisha yakiwemo matusi katika kurasa za klabu ya Aston Villa na kurasa za wachezaji wa timu hiyo, wakidai kuwa mchezaji wao hapewi nafasi nyingi uwanjani.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Samatta ameandika,

"Mashabiki wa soka Tanzania nafahamu kuwa mnanipenda kijana wenu na mnapenda nifanye vizuri katika timu yangu mpya, lakini nawaomba muache kutoa maneno ya kashfa au yenye mlengo mbaya katika kurasa za timu au wachezaji, binafsi sifurahishwi".

Aston Villa ilicheza mechi ya ligi wikiendi iliyopita dhidi ya AFC Bournemouth ambayo pia ilikuwa ni mechi ya kwanza kwa Samatta katika Ligi Kuu nchini Uingereza na kufanikiwa kufunga bao, licha ya timu yake kupoteza kwa mabao 2-1.

Tangu Samatta atue Aston Villa, mashabiki na Watanzania wengi wamekuwa wakiifuatilia kwa ukaribu klabu hiyo mtandaoni. Ambapo tangu tetesi za usajili wake zilipoanza, takribani wafuasi 170,000 wameongezeka katika mtandao wa Instagram.

Source: EATV
 
Watu wapuuzi sana, yaani wanamuongezea jamaa pressure zisizo na maana wamuache a-concetrate kwenye game no matter what happens.
 
Anacholalamika Samatta ni kama kinachotokea humu JF. Watu wanatukana na kushambulia wenzao bila sababu ya msingi utadhani taifa letu ni la watu vichaa tupu.

Hakuna kuvumuliana wala kujenga hoja, ni matusi tu kama watu wana msongo wa mawazo.
 
Wabongo wanakosea sana,angalia yule jamaa wa Senegal aliyefunga goli vs taifa stars,walivyomtukana hadi jamaa akatoa ya moyoni,ili kufuta aibu waziri wa utalii akampa offer ya bure kuja kutalii serengeti.

Ni aibu sana kwa hawa wabongo wenzetu wenye viherehere

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samatta ni mpumbavu anapaswa apige kazi haswa, mambo ya mitandaoni aachane nayo. Ingekuwa hivyo akina Adebayo,Fellaini,Lukaku,Giroud, Rooney, Bale, n.k wangekuwa wameacha kucheza mpira. Kwanza wachezaji Wa ulaya walio wengi sana hawajisumbui na hayo mamitandao kuona washabiki wanavyotoa shombo
 
Anacholalamika Samatta ni kama kinachotokea humu JF. Watu wanatukana na kushambulia wenzao bila sababu ya msingi utadhani taifa letu ni la watu vichaa tupu.

Hakuna kuvumuliana wala kujenga hoja, ni matusi tu kama watu wana msongo wa mawazo.
Afterall hana muda mrefu ndio kwanza kaanza hiyo ligi,pili watu wengine wanadhani kuingia kwa Samatta Aston kutaifanya iwe kama Liverpool kwa ghafla,wao wameongeza mtu kwenye kikosi angalau timu ipate nguvu,kingine pia wajue ameingia msimu wa ligi tayari unaelekea mwishoni kwahiyo tusitegemee mabadiliko makubwa sana...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samatta ni mpumbavu anapaswa apige kazi haswa, mambo ya mitandaoni aachane nayo. Ingekuwa hivyo akina Adebayo,Fellaini,Lukaku,Giroud, Rooney, Bale, n.k wangekuwa wameacha kucheza mpira. Kwanza wachezaji Wa ulaya walio wengi sana hawajisumbui na hayo mamitandao kuona washabiki wanavyotoa shombo
Mtoto wa Mbagala yule itamchukua muda kidogo kuutoa u-mbagala wake kichwani na ku-adopt namna wachezi wenzake wanavyo handle pressure za mitandaoni.

dodge
 
Baadhi ya watanzania ni aina ya wale ndugu mmoja akifanikiwa basi anabebeshwa mzigo wote wa malezi ya ukoo, kila kona atatangazwa na kusifiwa balaa, Ole wake atakayemchokoza huyo mfanikiwa au yeye mwenyewe akionyesha dalili za kuelemewa lawama za wanandugu.

IMG_20200203_150205.jpg
 
Duh! Wanaweza kusababisha jamaa ahujumiwe na wachezaji wenzake, anyimwe hizo pasi kabisa.
 
Back
Top Bottom