Mbwana Samatta huenda akasajiliwa na timu ya Middlesbrough ya Uingereza mwezi January.

Bora abaki Genk anacheza Europa anaoneka vizuri na timu kubwa kuliko aende Middlesbrough iliyo second division na hakuna mechi za kimataifa.
 
Utoke timu inayocheza uefa uropa uende timu ya daraja la pili? Hahahaaa Hesabu zinagoma kabisa. Genk inaongoza ligi kwa muda mrefu sasa ko we unasema genk ni sawa na timu ya daraja la pili?
 
Lakini kwa umri wake sasa yupo kwenye "peak" hivyo si vibaya akijiongeza kabla ya kufikia 30
Kumbe ni championship, aliposema daraja la kwanza nilidhani league one. Champioship sio mbaya, anaweza akapanda nayoo, wako wa nne.
 
Utoke timu inayocheza uefa uropa uende timu ya daraja la pili? Hahahaaa Hesabu zinagoma kabisa. Genk inaongoza ligi kwa muda mrefu sasa ko we unasema genk ni sawa na timu ya daraja la pili?
Akichukua kikombe msimu huu kama middlesbrough inamuhitaji aende, middlesbrough wako ktk nafasi nzuri kurudi ligi kuu na pia mshiko utaongezeka.
 
Mi naona asubili usajili mwezi wa tano,wakati huo akaze buti achukue golden boot na ajitahidi sana awe kwenye orodha ya wafungaji bora Europa league,hii itaongeza thamani yake katika usajili.BTW kwa sasa analipwa bei gani?
 
Samatta sizani kama atakubali kwenda, jamaa anajiamini na anajeuri, Simba aliwafanyiaga jeuri walivyo kataa kutimiza matakwa yake, pia Katumbi alikua mgumu kumwachia bila kukomaa asingetoka Mazembe. Anaweza asiende timu kubwa sana ila atakomaa aende ligi kubwa siyo kurudi nyuma. Kwangu bora abaki Genk mpaka ligi ishe kwa speed ya Genk mwakani watacheza champions league na dirisha kubwa anaeza pata timu nzuri zaidi. Ukizingatia kuna uwezekano akawa top scorer wa ligi yao.
 
Utoke timu inayocheza uefa uropa uende timu ya daraja la pili? Hahahaaa Hesabu zinagoma kabisa. Genk inaongoza ligi kwa muda mrefu sasa ko we unasema genk ni sawa na timu ya daraja la pili?
Kwa mfano wewe ndio unachezea Yanga inayoongoza ligi ya Tanzania halafu club ya Aston Villa inayoshiriki ligi ya Championship kule Uingereza ikakuhitaji utaacha kwenda kisa unachezea timu inayoongoza ligi?! Point yangu tafuta kigezo kingine cha kumshauri Samata asiende Middles ila sio hicho ulichoandika.
 
Nasikia jamaa jana katupia mbili tena huko ubelgiji.
 
Uko sawa ila pia inategemea na Genk kama wanataka kutengeneza faida ikiwa watamuuza kwa milioni 7 au 8.

Angalia walimsajili kwa kiasi gani kutoka TP Mazembe.
 
Eti samata alitengeneza jina lake TP MAZEMBE.. hakuna ulipoitaja simba..kwa hiyo usipoitaja simba unapata faida gani kwa mfano!! Hizi ni akili za AKILIMALI
 
Eti samata alitengeneza jina lake TP MAZEMBE.. hakuna ulipoitaja simba..kwa hiyo usipoitaja simba unapata faida gani kwa mfano!! Hizi ni akili za AKILIMALI
Duh kwa hiyo hilo nalo linahitaji mjadala?! Simba ilimtambulisha Mazembe ikamtengenezea jina.
 
Utoke timu inayocheza uefa uropa uende timu ya daraja la pili? Hahahaaa Hesabu zinagoma kabisa. Genk inaongoza ligi kwa muda mrefu sasa ko we unasema genk ni sawa na timu ya daraja la pili?
Championship inalipa zaidi ya ligi kuu ya Belgium
 
Samatta akomae hapo hapo Genk na pia azidishe tu kujituma,kumbuka Genk ndio team iliyowatoa kina De bruyne,Banteke na Thibaus courtois.
 
K
Kutoka Genk kwenda Middlesbrough timu ya Daraja la pili. Hapana kwa kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…