Mbwana Samatta: TP MAZEMBE imempaisha, Taifa Stars imemharibia soko

Mbwana Samatta: TP MAZEMBE imempaisha, Taifa Stars imemharibia soko

ebaeban

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
2,205
Reaction score
2,697
Huyu dogo Mbwana Sanmatta a.k.Samagoli timu yake anayoichezea imempandisha chati kweli,lakini stars imevunjia soko, jana mliona madalali majkwaani wanaangalia wachezaji walishindwa kuamini kama anaweza kucheza ulaya. Ndiyo maana mastar timu za taifa wanazikwepa, hapa na maana mastar wa Afrika, timu zao za taifa huzichezea kwa basi tu,sababu zenyewe ndiyo hizo./
 
madalali gani hao, unawajua hadi madalali?
 
dogo anajua na waswahili tunsema kama riziki ipo ipo tu, simba wanamtaka Mavugo ilihali anasugua bench Burundi ni ile kusema ukipenda chongo utaita kengeza
 
dogo anajua na waswahili tunsema kama riziki ipo ipo tu, simba wanamtaka Mavugo ilihali anasugua bench Burundi ni ile kusema ukipenda chongo utaita kengeza

Hoja kama hii ingetolewa na mkuu yahoo ningejua anawaponda mikia kwa vile hawatakii mema. Sikujua kama Mavugo anasugua benchi huko Burundi wakati huku TZ ni gumzo la Msimbazi. Kwa vile kauli imetolewa na mkuu Amavubi acha niamini kuwa ya Mavugo ni ya kweli.

Pamoja na Stars kupigwa kipigo cha karne, kipigo hicho hakikusababishwa na Samatta personally bali uwezo mdogo wa wachezaji wengi wa Tanzania. Kama riziki ipo haiwezi kupotea, go go go Samatta!

Katika ubora wake, George Opong Weah aliwahi kuwa mchezaji bora wa dunia akitokea katika nchi yenye kiwango duni cha soka, kwa uzalendo wake aliendelea kuichezea Liberia bila kigugumizi. Hayo ndiyo yanayotokea kwa Samatta.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom