Mbwana Samatta uwezo wake wa kawaida Mno, Anabebwa na bahati tu!

Mbwana Samatta uwezo wake wa kawaida Mno, Anabebwa na bahati tu!

Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa Mbwana Samatta Tangu alivyotua katika Club ya KRC Genk ya Belgium akitokea TP Mazembe ya DRC.

Kiukweli jamaa kiwango chake ni cha kawaida sana na anabebwa sana na bahati kubwa aliyonayo kwani performance yake haitishi sana.

Ukiangalia magoli anayofunga asilimia kubwa ni ya kawaida sana yasiyo na ufundi (hufunga zaidi kwa kichwa na asilimia kidogo kwa mguu na setpieces).

Kwa namna soka la Ulaya lilivyokuwa na ushindani hasa kwa mabeki wakatili (kama akina Pepe) sioni Samatta akifanya lolote mbele yao, kwani mbinu zake mguuni hazitishi mabeki na ni za kawaida sana.

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.....Jamaa some how Anajitahidi na anaendelea kujitahidi kwani ameonesha ujasiri na amekuwa Idol kwa Vijana wengi wenye ndoto za mafanikio kwenye soka kama ya Samatta.

Kama ataweza kuuona uzi huu au aambiwe na mtu wake wa karibu aliyeko humu basi nimwombe ndugu yangu Samatta, aongeze zaidi juhudi na ajifunze mbinu nyingi za kufunga kwani yeye kama forward kazi yake uwanjani ni magoli tu na si vinginevyo. Bila kisahau Kujisahau na Kuvimba kichwa akuepuke sana kwani magazeti ya bongo yanapamba wachezaji hadi wanakuwa under pressure na mwishowe huharibu carrier yao.
Wewe mwenye uwezo kuliko yeye uko wapi?? Jf unaandika nyuzi.. Mwezio yuko Genk anafunga magoli na mshahara wa zaidi ya Euro 50,000.. Hakuna bahati kwenye soka he is that good ndio maana anachez soka ulaya....
 
Mnaojidai wakosoaji wake wakubwa tunaimani bado mnahesabu magoli yake ya kawaida. Hao wa kwenu mafundi wa Mpira mmekaa nao kwenye vijiwe vya kahawa na na vya madawa ya kulevya huku mnayemchukia kwa kutokujua mpira yuko Europa league.
 
Mnaojidai wakosoaji wake wakubwa tunaimani bado mnahesabu magoli yake ya kawaida. Hao wa kwenu mafundi wa Mpira mmekaa nao kwenye vijiwe vya kahawa na na vya madawa ya kulevya huku mnayemchukia kwa kutokujua mpira yuko Europa league.
Mungu Fundi wenye wivu wameze supu ya viwembe
 
Wewe mbona una hiyo bahati , acheni chuki za kijinga izo kina roho morata wanakosa magoli na Yuko na kipa na bado anaonekana mchezaji Bora kwa nn msimuheshimi samata
 
Mleta mada na yule jamaa mbishi ni wachawi wakubwa kuliko wanaopaa na ungo.
Pumba.vu!!!
 
Wewe nawe una kichwa kibovu sijapata kuona, sasa samata akiwa ni mbahatishaji wewe kinakuuma nini ,mbona upo kama dada vile mwanaume shobo, mbwana ni mchezaji mwenye jitihada sana na sio bahati ndiyo umemeweka hapo...mpira sio gambling

Sent using Jamii Forums mobile app
TOKA NIZALIWE SIJAWAHI KUONA KENGE KAMA WEWE. MTU ANAPIGA GOLI MBILI UGENINI DHIDI YA BESKITAS BADO HUONI KUWA NI SUPER? HIVI ROHO YA WIVU KAMA ULIYONAYO WEWE IPO MAHALA PENGINE DUNIANI? UNAKERA SANA. WEWE NI MCHAWI
 
Back
Top Bottom