Mbwana Samatta wa Genk kashasahaulika

Mbwana Samatta wa Genk kashasahaulika

bandiko lako linaonyesha jinsi ulivyo na husda,chuki na choyo.pessimistic bastard,mtu hana hata mwaka unataka afanane na kina drogba,unajua drogba ametumia miaka mingapi kufikia heshima na mafanikio aliyonayo?mbona hamna jema nyie?
 
Mtoa mada kwanza umeshakula au ndio umeamka na pombe za jana usiku maana naona unaweweseka tu hata hujui namna ya kutumia comparison theory..
Samatta hajamaliza hata mwaka akiwa Genk unawezaje kuwafananisha na hao akina Drogba ambao wamekaa katika timu muda mrefu...

Lete records za Drogba alipoanza kucheza pale Monaco na si uropoke tu
 
Wabongo bwana sijui lini tutajifunza kupenda vya kwetu na kuvisifia hata kama ni kweli vinachemsha? Huo ndio tunaita uzalendo. Cha kwetu ni cha kwetu tu.
 
Wabongo bwana sijui lini tutajifunza kupenda vya kwetu na kuvisifia hata kama ni kweli vinachemsha? Huo ndio tunaita uzalendo. Cha kwetu ni cha kwetu tu.
Bado tuko wajinga sana. Hatupendi hata kujifunza. Mfano kuna wakenya humu, lakini hatujiuliz mbona wao hawaleti nyuzi za kuponda vya kwao? Inabidi wabongo wenzetu hawa wenye roho za kichawi tuwabadilishe. Wakileta uzi wa kuponda tunaupita kama hatuuoni, kila akifungua haoni comment yoyote. watabadilika tu.
 
Mkuu acha uongo,Samatta aliumia kwenye mechi ya Europa dhidi ya Rapid Wien akakosa mechi 3 za ligi na jana ndio karudi.
 
Sammata mwendo wake Mdogo Mdogo tu kama Bombardier
 
Mpaka sasa sioni tena umuhinu wa Sammata kwa timu ya FC Genk. Kwa mfano jana Genk walishinda bao tatu bila mchango wa Samatta ndani ya uwanja. Kuna jamaa alikuwa ana assit ile mbaya na kufunga vizuri kiasi kwamba huezi mfananisha na mdogo wetu Samatta.

Mechi ile ingine iliyopita Samatta alikuepo ila mchango wake ulikuwa hafifu ndani ya uwanja na timu kupigwa tatu bila. Pia na hata sasa katika Pro league ya Belgium huyu bro wetu hayupo katika safu ya wafungaji bora.

Kwa maneno haya machache ninaamini bado Samuel Etoo, Didier Drogba, George Wear na Nwako Kanu ndio watabakia kuwa wafungaji bora wa Afrika waliowahi tisha Ulaya.
katika soka kuna kupanda na kushuka, hatua aliyofikia samatta naamini hata wewe usingeweza kuifikia kwahiyo kumponda ni kuonyesha jinsi gani ulivyo na chuki na wivu dhidi yake.

cha msingi ni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ambaye ndio mpaji wa wote na sio kumuanzishia thread ya kumponda. FANYA YAKO BRO, no offense meant.
 
ila hajapondwa jamani....nimeongelea hivi nikimaanisha alikuwa na mwanzo mzuri ila sasa kaporomoka kidogo...
 
Mpaka Tarehe 25 September alikua nafasi ya pili kwa ufungaji (Belgium pro league)
genk.jpg
 
yey kasema tu
Ili iweje? Unaweza linganisha etoo na Samatta hata muda wao wa kucheza ulaya haulingani, Natamani aje malaika aifungie hii mitandao ikija kufunguliwa samatta mchezaji bora barani ulaya na Chelsea
 
Back
Top Bottom