Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Sasa kama unayo (tayari heshima kwa mwenzio hamna) kuficha kunasaidia nini kama sio unafiki?
Ukiwa mkubwa utajua kunasaidia nini, kuvunja ndoa unadhani jambo rahisi?
Ukiwa mkubwa utajua kunasaidia nini, kuvunja ndoa unadhani jambo rahisi?
Sasa kama unayo (tayari heshima kwa mwenzio hamna) kuficha kunasaidia nini kama sio unafiki?
Kwani visasi na kukomeshea kunasaidia nini?
Bora huyo anayeweka mambo hadharani ili mwenzie ajue ukimwi unamnyemelea, aweze kuchukua tahadhari kuliko yule wa kimya kimya....... Silent Killer!!!!!
umenena. Waeleza wamezidi, sijui ni ulimbukeni au sifa za kijinga. Wengine hadi matumizi yanasitishwa! Kisa nyumba ndogo
Naona sasa mambo ya nyumba ndogo yameshakubalika kwenye jamii ya Tanzania. Sasa sielewi kwa nini watu hutokwa na mapovu pindi wagunduapo kuwa wenza wao wanazo.
Kwasababu mkuki kwa binadamu mchungu zaidi ya klorokwini. Watu wakiwa na nyumba ndogo hua wanatangaza kwa sifa ila wakigundua wenzao nao wanao wananywea na kuanza kulia lia.
Kwasababu mkuki kwa binadamu mchungu zaidi ya klorokwini. Watu wakiwa na nyumba ndogo hua wanatangaza kwa sifa ila wakigundua wenzao nao wanao wananywea na kuanza kulia lia.
Mijitu mingine ikipata nyumba ndogo huanza mbwembwe kwa wake zao na ndugu na jamaa pia.
Utakuta mtu anaondoka nyumbani alfajiri, unarudi saa tisa usiku, shati limejaa ma lipstic, unarudi na harufu ya pafyum ya kike, na mbaya zaidi ndani una bikini NYEKUNDU, mkeo akikuuliza unakuja juu kinyama.
Hivi ni lazima ukiwa na nyumba ndogo uupigie baragumu ulimwengu?