Yaani katika vitu ambavyo mimi sivielewi na naona kuwa watu wanalipa gharama kubwa pasi na msingi ni hili la MC....
Yaani mtu kuongea ongea pale mbele kwa masaa kadhaa ndio analipwa kweli malaki kama sio mamilioni....
Mimi kulikuwa na sherehe ya mdogo wangu(ndoa) wenyewe waliandaa na msema chochote (MC) kwa bajeti Yao ambapo ni hela nyingi kidogo.....yule jamaa akawa mzushi mzushi kama huyo wa kwenu....
Mpaka siku ya sherehe watu wanakaribia kuingia ukumbini MC haonekani na namba zake hazipokelewi mara haipatikani....watu wakaanza kuchanganyikiwa....na taharuki ikatanda kwenye viunga vya ukumbi...
Mimi nikawaomba ratiba ya sherehe na kipaza sauti tu 🎤....jambo nikalianza mwenyewe mdogo mdogo....kutahamaki watu wakaanza kujaa ukumbini na Sherehe ikaenda fresh kabisa.....
Yule anayejiita MC akaja mbio mboo mida ya saa sita hivi kama kaja kuchungulia hivi watu walivyomuoa wakamkimbiza kama mwizi mimi huku ukumbini naendelea kuibagaza 🎤.....
Jambo likaisha salama na mimi msema chochote MC wa kujitolea nikaambulia ka laki ka kulainisha koo na supu asubuhi tena kenyewe nilitunzwa na wageni waalikwa baada ya kuwakosha kwa kucheza vyema na 🎤.....
Hawa wajinga wajinga wanakula hela ya bure kutokana na ulimbukeni wa sisi wabongo hasa sie walalahoi