Angalia basi tunavyo-complicate mambo. Kuna sherehe ya kuposa. Halafu sherehe ya kutambulishana. Halafu sherehe ya kupokea mahari. Hizi kwa bahati nzuri sehemu nyingi bado hazijawa corrupted.Baada ya tarehe ya harusi kutajwa ndipo fujo zinapoanza.
Tunaanza na Kitchen Party. Hii imekuwa corrupted. Badala ya kuwa ya kifamilia, kumfunda mwanao, kumpa vifaa vya nyumbani n.k. sehemu kubwa imewekwa kwenye mafunzo ya kujamiana. Imefika mahali tunakaribisha mashoga kutoa shule! Mafunzo yaliyokuwa na umuhimu katika jamii sisi tunayafanyia mas'hara! Hii vile vile imekuwa sehemu ya wakina mama kutambiana. Na kwenyewe tunakodi kila kitu maana hakuna mwenye sherehe, wote ni waalikwa wasiotaka kuchafuka siku ya sherehe.
Halafu tuna send-off. Hii nayo imekuwa corrupted. Badala ya kuwa sehemu ya ndugu za binti kumuaga ndugu yao imekuwa siku ya kuwaonyesha wanaotaka kuoa jinsi alikotoka binti kulivyo maji marefu. Hizi nazo zimekuwa ni reception bila harusi. Na kwenyewe hakuna mwenye shughuli. Wote ni waalikwa wasiotaka kuchafua pamba zao! Wazazi wakiwa na bahati wanapewa nusu dakika kumuasi binti yao maana MC anaenda na time na watu wengi walichofuata ni ulabu, muziki na vichekesho vya Mc na si nasaha za wazazi.
Siku ya harusi, ndiyo tusiseme. Hasira zote za kunyimwa kadi kwenye send-off tunamalizia hapa. Na penyewe cha muhimu ni kuwaonyesha watu jinsi tunavyoweza kula, kunywa na kusaza. Sifa imekuwa ni ufunguaji wa champeni na si nasaha za wazazi. Ndugu ambao hawakuwa na uwezo wa kuchanga ndiyo walie. Viti vya heshima vinapewa kwa hao wenye deep pockets, hata kama uhusiano nasi ni mdogo. Hapa tena mkazo si kwenye kushiriki bali ni kuonekana. Na penyewe hamna mwenye shughuli. Wote ni wageni. Wote wanaingia kwa kadi maana kamati ya harusi haina mashara. Hela zote zilizochangwa ni lazima watu wagide. Hakuna free loaders hapa hata kama wanaooana ni wapwa wao. Ngoma za asili nazo zinapewa dakika mbili maana ratiba ilichelewa kwa sababu maharusi walienda kupiga picha bich au Mlimani City! Maharusi wanatangulizwa na matarumbeta. Chakula ni kile kile, chips kidogo, wali, shingo la kuku, kipande cha chapati, mboga zilizochoka na ndizi zisizojulikana zilikotoka! Tunajipanga kupeleka hzawadi zetu za bilauli zilifungwa kwenye mabox na makaratasi mazuri. Maharusi wanacheza rumba moja kutoka katika muziki kutoka ughaibuni. DJ kuonyesha uzalendo anapiga Chakacha, bongo flava n.k. Wacheza ngoma za kitamaduni wako hoi maana hakuna aliyekumbuka kuwapa chakula. Watu wanatapika, wanajisaidia hovyo halafu wanaondoka wakisifia harusi.
Baada ya wiki mbili, tunavunja kamati. Hapo napo tunaelezwa kuwa kuna mbinamu wa Bwana harusi nae anakusudia kuoa hivi karibuni. Kamati inaundwa upya. Mchezo unaanza tena. Ndiyo maisha yetu. Ndiyo maendeleo yetu.
Count me out!
Amandla........