MCD wa Twanga Pepeta afariki dunia

Hivi kwanini mnaogopa kusema ni..ngoma tu..eti muda mrefu...madai yao tafsida....ni ugonjwa wa kawaida saanaaa msiogope
 
Kama kuna mdau ana access na wimbo unaoitwa "KUOLEWA" ametunga Luiza Mbutu upo kwenye albam yao inayoitwa FAINALI UZEENI, aisee MCD kapiga tumba ya hatari sana humo. Kuna sehemu Ally Choki anamtaja MCD then vyombo vyote vinasimamishwa inasikika tumba ya MCD tu
 
Aliyekuwa mpiga Tumba mahiri wa bendi ya muziki wa dansi nchini African Stars Twanga Pepeta, Soud Mohamed 'MCD', ambaye baadaye alihamia bendi ya Mashujaa na baadaye kurejea tena Twanga Pepeta, amefariki Dunia katika hospitali ya KCM-Moshi.

Taarifa za kifo cha mpiga tumba huyo aliyekuwa mahiri katika kuzicharaza Tumba, zimetolewa na kuthibitishwa na Msemaji wa Bendi ya Twanga Pepeta,Hassani Rehani.
Taarifa zinaeleza kuwa MCD amefariki baada ya kusumbuliwa na maradhi ya muda Mrefu.


MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN.
 

Nilitaka kuandika kama wewe vile! Asante kwa kutukumbusha. Jamaa MCD tutammis sana kama tunavyommis Baba Diana, Baba Zaituni, Baba Sharifa (Abuu Semhando).
 
Hii tabia ndo inafanya ukimwi uonekane ugonjwa wa aibu..
 
Hii tabia ndo inafanya ukimwi uonekane ugonjwa wa aibu..

Sanaaa.....ukimwi sio ugonjwa wa siri na kutisha tena...anakufa wa maralia wa ukimwi anadunda...tatizo watu wanajua ukimwi ni wa ngono tuu..u can stay as long as u want
 
Nilitaka kuandika kama wewe vile! Asante kwa kutukumbusha. Jamaa MCD tutammis sana kama tunavyommis Baba Diana, Baba Zaituni, Baba Sharifa (Abuu Semhando).

Umesahau kumalizia Baba Mwanahamisi.......Abuu Semhando! Hiyo combination ilitisha sana. Pamoja kiongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…