MCGregor :Niko radhi kufia uwanjani lakini sio kupigwa na Floyd Mayweather

MCGregor :Niko radhi kufia uwanjani lakini sio kupigwa na Floyd Mayweather

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Mwanamasumbwi Conor MCGregor ametamba kwamba lazima amchakaze Mayweather kwa namna yoyote ile ,Conor alienda mbali zaidi kwa kudai kuwa labda afie uwanjani ndo ushindi pekee atakao upata mayweather lakini kinyume na hapo lazima amtandike Floyd tena hamtandiki kwa Point bali kwa Knockout

Conor amedai kuwa ameangalia mapambano mengi ya Floyd na amegundua udhaifu wake upo sehemu gani hivyo basi yeye na kocha wake wanafanya training za kutosha za kwenye huo udhaifu wa Floyd ili amdondoshe mapema zaidi

Conor kwa kuonesha yupo makini kwa kiasi gani ameamua mpaka kuiba mbinu za Jeff Hornet ili kundhibiti Floyd mayweather na kuandika historia mpya kwenye ndondi .

Kwa upande wa Floyd alipoulizwa kuhusu tambo hizo akasema kuwa Conor uwezo wa kushinda hilo pambani ni mkubwa kwa sababu yeye (Floyd) umri umeshamtupa mkono na kasi pamoja na accuracy yake ya kurusha ngumi imepungua kwa kiasi kikubwa kulinganisha na miaka 10 mpaka 20 iliyopita

Screenshot_2017-07-07-00-41-51_1.jpg
 
Akifa atazikwa, kwani hajaanza yeye na hatomalizia yeye..
 
Kweli jamaa ni mpiganaji mzuri Ila asije akachanganya na mateke na bila mateke uwezo wake utapungua
 
Floyd naona hata hili pambano alichukulii serious kwani anajua atamnyoosha hata maandalizi yake nayaona ya kawaida, ila sijajua kwa nn Floyd anachagua watu wadhaifu.
 
Floyd naona hata hili pambano alichukulii serious kwani anajua atamnyoosha hata maandalizi yake nayaona ya kawaida, ila sijajua kwa nn Floyd anachagua watu wadhaifu.
kwa kweli hata mimi hili pambano sijalifurahia kabisa
 
Floyd apigwe tu hamna shida. Tyson alipigwa itakuwa yeye
 
Back
Top Bottom