Leo majira ya Saa kumi na mbili asubuhi,zilianza kusambaa taarifa mitandaoni na kwenye vyombo mbili mbali vya habari juu ya kifo cha mwanasiasa na mchungaji maarufu hapa Tanzania Christopher mtikila.
Habari hizi zimewashtua watu wengi na hasa wapenda mabadiliko hapa nchi kwani kwa Mara ya mwisho mtikila alipata kuonekana kwenye kituo cha runinga cha star TV akimshambulia mgombea wa ukawa kuwa ni mgonjwa na yeye alitaka kwenda mahakamani kufungua kesi kumpinga mgombea huyo.
Mimi namfananisha kwa ukaribu sana mtikila na bwana mmoja hapa Tanzania ambaye anajiita mwanaharakti huyu ni bwana renatus mkinga watu hawa wana tabia moja wanafanana wote hawana woga pale wanapojenga hoja zao lakini mtikila yupo mbele kidogo ya mkinga kwani yeye anapoona jambo linafanyiwa mizengwe na mamlaka hukimbilia mahakamani kutafuta muafaka wa kisheria.ndio maana hata chama chake alichokuwa akikiongoza cha democratic party kiliweza kujizolea umaarufu mkubwa katika siasa za mahakamani kuliko zile siasa zilizozoeleka za majukwaani.
Mbali na hayo mtikila tutamkumbuka katika mambo mengi aliyowahi kuyapigania kama vile kudai taifa la Tanganyika,mgombea huru, katiba mpya na kwa kumbukumbu mtikila alikuwa ni mmoja kati ya wajumbe wa bunge la katiba na alishiriki kususia vikao vya bunge hilo ingawaje yeye hakuwa miongoni mwa wanasisa walioasisi ukawa.
Katika historia ya siasa za nchi hii mtikila atakumbukwa kwa mengi kwa mfano aligombea ubunge wa JIMBO la ludewa kwa tiketi ya chadema baada ya kifo cha Horace kolimba na kushindwa lakini pia aliwahi kuhukumiwa kifungo gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kutoa maneno ya kashifa kuwa serikali ilitumia fedha nyingi kwenye mazishi ya mwl Nyerere akidai kuwa ule ulikuwa ni mzoga tu.
Ingawaje inasemekana kuwa mtikila alikuwa ni mchungaji wa makanisa ya kiroho historia inaonesha kuwa huyu ni mwanasiasa mwanaharakati kupata kutokea katika nchi ya Tanzania .