Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini na Mwenyekiti wa mstaafu wa kanda ya Nyasa Chadema, akiambatana na Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Ndugu Amos Makalla amebainisha kuwa Chama chake cha zamani kinafaa kupuuzwa kutokana na kutokuwa na ajenda zinazogusa maisha ya wananchi na badala yake wanang'ang'aniza ajenda na mabadiliko yenye kuwarahisishia Vigogo wa chama chao kuweza kushika madaraka ya nchi.
Wakati akizungumza na wananchi wa Jiji la Mbeya, Mch. Msigwa amewataka kuzungumzia kuhusu maboresho yanayohitajika kwenye sekta ya afya, kilimo, usafiri na usafirishaji, akiwataka kuwa na shukrani kwani hata wanayoyadai, yamefanyiwa maboresho na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Akizungumzia miongoni mwa maboresho hayo, ametaja kuhusu wakurugenzi wa Halmashauri kutokuwa sehemu ya kusimamia uchaguzi, Kuwa na uwezo wa kumpigia kura mgombea urais umtakaye ukiwa popote ndani ya nchi sambamba na mgombea kutopita bila ya kupingwa.
"Nimekuwa huko (Chadema) tena mbunge kwa miaka kumi, hatuwezi kuwa na Chama kinachojulikana kwa kupinga tu. Chama chetu cha Mapinduzi kinajulikana kaa kazi na namna kinavyoshughulikia matatizo ya watu." Amesema Mch. Peter Msigwa.