Baadhi ya waliokuwa wanachama wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) na baadaye kuhamia vyama vingine vya siasa wameomba msamaha kwa wananchi na wafuasi wa chama hicho, wakieleza kuwa wameamua kurejea ili kushiriki katika kukijenga na kuendeleza harakati za kushika dola.
wakizungumza jana, oktoba 16, 2026, katika viwanja vya manyema, mjini moshi, mkoani kilimanjaro, mchungaji peter msigwa, aliyewahi kuhamia chama cha mapinduzi (ccm) kabla ya kurejea chadema, pamoja na patrick assenga, aliyehamia chama cha ukombozi wa umma (chaumma) na baadaye kurejea chadema, wamesema wamegundua kuwa walifanya makosa kuondoka katika chama hicho.
wamesema uamuzi wao wa kurejea chadema unatokana na kutambua umuhimu wa kuungana na wanachama wengine katika kukijenga chama hicho na kuendeleza harakati zake za kisiasa. aidha, wamewaomba wananchi na wafuasi wa chama hicho kuwasamehe na kuwapokea tena ili kwa pamoja waendelee na safari ya kukijenga chama na kufikia lengo la kushika dola.
Chanzo:Jambo tv