Wewe nadhani umekosa uelewa.
Kuna mtu amewahi kukataa kuwa nchi imekuwa inahitaji nyongeza ya umeme? Watu walikuwa wanahoji uamuzi wa kuendelea kujenga mabwawa ya maji kama chanzo cha umeme wakati yaliyopo tayari yanashindwa kuzalisha umeme uliotakiwa kwa sababu ya upungufu wa maji. Na walikuwa sahihi sana. Na wala hilo bwawa haliwezi kuwa mwarobaini ya Tatizo letu kubwa la kukosekana umeme wa uhakika. Lazima tupate umeme wa vyanzo tofauti pia. Upgrading ya umeme wa gas ingetupatia umeme kwa haraka zaidi na kwa gharama nafuu zaidi.
Kuna mambo alifanya vizuri, na kuna mambo alifanya vibaya kabisa, hasa kwenye haki za watu, utawala wa sheria na demokrasia. Wa sasa amefanya vibaya zaidi, hasa kwenye uzalendo kwa nchi yake na usimamizi wa Serikali. Rasilimali za nchi amezifanya kama pipi, amezigawa hovyo kwa wageni kwaajili ya maslahi binafsi ya watu wa karibu yake. Viongozi na watendaji wa Serikali, kila mtu anafanya anavyotaka. Anayetaka kuiba ruksa, anayetaka rushwa ruksa, n.k.