Samahani sana mkuu yaani "babu" unataka kumfananisha na Yesu????????? Khaaaaa yaani wewe jamaa wa ajabu sana unamfananisha Messi na Ngasa?! Yesu ni world ICON huwezi kumfananisha na mtu wa kawaida mkuu..............
Jambo hili usiliangalie kitheolojia liangalie kiroho, ukiliangalia kitheolojia hutapata majibu, maana mpaka sasa theolojia imeshindwa kutoa majibu mengi ikiwa ni pamojana chanzo cha Mungu ni nini? theologia imekuwa ikipinga baadhi ya mambo ya kiroho kitu kinachowafanya baadhi ya watumishi mara wanapobobea katika elimu ya theologia wamwache Mungu na kufanya mambo ambayo yapo kinyume na mafundisho ya kiroho. Nafikiri wewe ni baadhi ya wanatheolojia wengi ambao hawana nguvu za roho mtakatifu bali wamejawa na udadisi na maswali ili kujipa upenyo wa kupinga uwezo wa Mungu. Mzee yule kama angejiita ni mganga wa kienyeji kusingekuwa na swali watu wangeenda kisirisiri kujipatia dawa, kwakuwa amesema dawa hiyo ameoteshwa na Mungu watu hawaamini maana wengi wanamashaka na uwezo wa Mungu, hii ni hatari na aibu sana. Inapotokea mtu anayemjua Mungu tena Mtu mwenye imani akahoji uwezo na sababu za dawa hiyo kuoteshwa mzee huyo tu ni kujaribu kuhoji utendaji wa kazi za Mungu ambapo kiimani ni sawa na ujinga au ushamba wa kiimani.nakumbuka huko nyuma mch. rwakatale wa mikocheni B assemblies of God aliwahi kutumia mtindo wa kununua vitambaa (leso) vyeupe na kuviombea kisha anawapa watu ati wakivitumia kama kuviwekwa kwenye viipaji vya nyuso zao au za wagonjwa wao nyumbani, wanapona maradhi yanayowasumbua. shuhuda nyingi sana zilitolewa na ilifikia mahali kama mtu yumo ndani ya basi akielekea kanisani na akagundua kuwa kasahau kitambaa nyumbani huteremka na kurudi kukifuata, yaani kikawa sacred kupita kitambaa cha kawaida.
binafsi sikuwahi kuunga mkono tabia ya huyu mama kuombea vitambaa na kuvifanya kama hirizi, na kwa kweli sikuona msingi wa jambo hilo kitheolojia.
sasa tena ameibuka Mch. Mwasapile akidai kupata ndoto juu ya mti ambao unapochemshwa, kikombe kimoja tu cha maji yake kinatosha kutibu magonjwa sugu kama ukimwi, kisukari, kansa, pumu nk. hapa pia sioni msingi wa kitheolojia.
kwa mujibu wa BBC, mch. mwasapile alisema si maji yale yanayoponyesha bali ni maombi. sasa mi najiuliza iweje neema ya Mungu ya uponyaji ijifungamanishe na maji kiasi kile? tena kiasi cha kwamba bila hayo maji neema hiyo haifanyi kazi? mbaya zaidi wanasema kuna masharti kama: lazima akupe kwa mkono wake, huruhusiwi kunywa zaidi ya mara moja nk. hapa neema ya Mungu inaletwa kwa masharti!
binafsi nashindwa kuiita karama, uwezo wa Mungu hauna mipaka ya mahali wala wakati. hainiingii akilini kwamba mti huo ukichemshwa mahali pengine nje ya kiiji cha samunge, hauponyi na babu akikuombea bila kukupa kikombe chake kwa mkono wake huponi!
siwezi kutoa hukumu juu ya babu lakini naamini Mungu ni mkuu na muweza kuliko anavyoonekana kupitia hali ya huko loliondo. biblia inatuasa, tusimzimishe Roho, tusitweze unabii, tujaribu mambo yote tushike lililojema na tujitenge na ubaya wa kila namna (1 thesalonike 5:19-22)
naomba mnielewe kuwa sikejeli ndugu zetu wanaogua magonjwa mbalimbali sugu wanaopata faraja ya pekee huko samunge kwa babu, la hasha. haya ni mawazo yangu tu yaliyojikita kutazama jambo zima kitheolojia zaidi na sijatumwa na mtu yoyote. pia tusiwabeze wale wanaoonyesha kuhoji mantiki ya kanisa la KKKT kujipambanua pamoja na huduma hii ya babu.
HUKUMU NI ZAKE BWANA
mbarikiwe sana wapendwa
Glory to God
Nenda ukanywe kombe kwa imani utapona, peleka kitambaa kwa Rwakatale kwa iman utapona.
"The secret of the word of God"
If u know the word of God u can use it to cure and raise dead bodies .
Believe me the power of the word of God is very strong if u know how to use it.
sasa tena ameibuka Mch. Mwasapile akidai kupata ndoto juu ya mti ambao unapochemshwa, kikombe kimoja tu cha maji yake kinatosha kutibu magonjwa sugu kama ukimwi, kisukari, kansa, pumu nk. hapa pia sioni msingi wa kitheolojia.
nakushukuru mpendwa.
kwa haya machache uliyoandika umesaidia sana angalau watu wajue kuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya huyo babu na Yesu. kilicho dhahiri hapa ni kuwa hata baadhi ya wanaonukuu biblia, hawaijui vizuri biblia yenyewe.
pia sijui kwa nini wameamua kukaa kimya kuhusu vitambaa vya rwakatare!
Glory to God
mh! Yangu macho, nasubir ushahidi

nakumbuka huko nyuma mch. rwakatale wa mikocheni B assemblies of God aliwahi kutumia mtindo wa kununua vitambaa (leso) vyeupe na kuviombea kisha anawapa watu ati wakivitumia kama kuviwekwa kwenye viipaji vya nyuso zao au za wagonjwa wao nyumbani, wanapona maradhi yanayowasumbua. shuhuda nyingi sana zilitolewa na ilifikia mahali kama mtu yumo ndani ya basi akielekea kanisani na akagundua kuwa kasahau kitambaa nyumbani huteremka na kurudi kukifuata, yaani kikawa sacred kupita kitambaa cha kawaida.

binafsi sikuwahi kuunga mkono tabia ya huyu mama kuombea vitambaa na kuvifanya kama hirizi, na kwa kweli sikuona msingi wa jambo hilo kitheolojia.

sasa tena ameibuka Mch. Mwasapile akidai kupata ndoto juu ya mti ambao unapochemshwa, kikombe kimoja tu cha maji yake kinatosha kutibu magonjwa sugu kama ukimwi, kisukari, kansa, pumu nk. hapa pia sioni msingi wa kitheolojia.

kwa mujibu wa BBC, mch. mwasapile alisema si maji yale yanayoponyesha bali ni maombi. sasa mi najiuliza iweje neema ya Mungu ya uponyaji ijifungamanishe na maji kiasi kile? tena kiasi cha kwamba bila hayo maji neema hiyo haifanyi kazi? mbaya zaidi wanasema kuna masharti kama: lazima akupe kwa mkono wake, huruhusiwi kunywa zaidi ya mara moja nk. hapa neema ya Mungu inaletwa kwa masharti!

binafsi nashindwa kuiita karama, uwezo wa Mungu hauna mipaka ya mahali wala wakati. hainiingii akilini kwamba mti huo ukichemshwa mahali pengine nje ya kiiji cha samunge, hauponyi na babu akikuombea bila kukupa kikombe chake kwa mkono wake huponi!

siwezi kutoa hukumu juu ya babu lakini naamini Mungu ni mkuu na muweza kuliko anavyoonekana kupitia hali ya huko loliondo. biblia inatuasa, tusimzimishe Roho, tusitweze unabii, tujaribu mambo yote tushike lililojema na tujitenge na ubaya wa kila namna (1 thesalonike 5:19-22)

naomba mnielewe kuwa sikejeli ndugu zetu wanaogua magonjwa mbalimbali sugu wanaopata faraja ya pekee huko samunge kwa babu, la hasha. haya ni mawazo yangu tu yaliyojikita kutazama jambo zima kitheolojia zaidi na sijatumwa na mtu yoyote. pia tusiwabeze wale wanaoonyesha kuhoji mantiki ya kanisa la KKKT kujipambanua pamoja na huduma hii ya babu.

HUKUMU NI ZAKE BWANA

mbarikiwe sana wapendwa

Glory to God
hapo umenena vema, by the way nasikia babu ametabiri kifo chake, atakufa siku ya jumatatu ya pasaka.Dada Judy hongera kwa wazo uko sahihi sana maana neno la mungu lina fundisha tusiziamini kila roho bali tuzichunguze Kama kweli zinatokana na mungu, inamaana mungu alishajua shetani atacopy vitu vyake na atavifanya kwa wanadamu na wanadamu wafikirie ni mungu na kumbe siye mungu,
Hii tabia ya watu kusikia miujiza na kuikimbilia na baadae kuja kuiponda imekuwa kitu cha kawaida sana kwa dunia ya sasa imezidi, mama Rwekatare, Kakobe, Ngurumo ya upako nk. walipaparikiwa sana na walipata wafuasi wengi sana ila baada ya muda walipondwa sana na wote walikuwa wanatumia bible kufanyia miujiza kwahiyo navyoona huu ndio huohuo mtiririko unaendelea sana sana napenda kuwashauri hivi technic zote anazozitumia mungu kwa wanadamu shetani keshaziiga na yeye antumia hizozo anatuchezea tuu akili zetu kwhiyo tunapaparika tuu bure vitabu vya dini vinatuongoza vizuri sana ila tunavisoma Kama vya hadithi hatuelewi tumebakia kukariri mistari ya bible 'we have to study and to learn the bible and not read' umizeni vichwa kumjua mungu Kama mnavyoumiza kufaulu mitihani sio kukupaparikia miujiza acheni uvivu wa kumuomba mungu wenyewe.
Wagonjwa nawataka radhi sio kwamba wagonjwa msiende loliondo nendeni mkanywe dawa kupona kweli mtapona ila sio kwasababu umepona ufikirie ndio mungu amekuponya 'hata Yesu walimwendea wakamwambia kumbuka bwana tulitumia jina lako kuponya magonjwa na wagonjwa walipona lakini aliwaambia tokeni kwangu siwajui' Nani vigumu kweli kumwambia mgonjwa asiende loliondo aijalishi anaeponya ni shetani au ni mungu cha msingi amepona au vipi wanajamii

Ndugu yangu, nadhani umefika njia panda kidogo. Labda nikusaidie kidogo kuhusiana na maandiko juu ya oponyaji na imani. Labda tusome Yohana 5:2 NAHUKO YERUSALEM ( Arusha, Loliondo) PENYE MLANGO WA KONDOO PANA BIRIKA, IITWAYO KWA KIEBRANIA BETHZATHA, NAYO INA MATAO MATANO. 3 NDANI YA HAYO JAMII KUBWA YAWAGONJWA WALIKUWA WAMELALA, VIPOFU, VIWETE, NAO WALIO POOZA, WAKINGOJA MAJI YACHEMKE ( wakingoja dawa ya babu ichemke). 4 KWA MAANA KUNAWAKATI AMBAPO MALAIKA HUSHUKA, AKAINGIA KATIKA ILE BIRIKA( kikombe cha babu tayari malaika alisha shuka wakati dawa ya babu inachemka), AKAYATIBUA MAJI. BASI YEYE ALIYE INGIA WA KWANZA BAADA YA MAJI KUTIBULIWA, AKAPONA UGONJWA WOTE ULIO MPATA.( hapa sasa ni tofauti na babu, kwa babu yeye sio mtu anayekunywa wakwanza dawa, bali WOOOOTE watakao kunywa dawa kwa imani ya kupona WATAPONA, HAKUNASHARTI LA MARAMOJA KWA MTU MMOJA KWA SIKU) (ENDELEA KUSOMA HADI MSTARI WA 9)[/B]. Sasa ndugu yangu, n kwamba hakuna namna, sisi wanadamu tunavyo weza kumpangia Mungu juu ya uponyaji wake, ama kufikiri Mungu anatibu kwa namna moja tu ama kama tutatakvyo taka sisi.
Pia tafakari namna NAAMAAMAN ALIVYO PONYWA UKOMA WAKE 2 Wafalme 5:1-27, hapa utaona namna Naaamana alivyo ponywa, lakini alipo pewa masharti ya kuponywa hakuamini hadi wafanyakazi wake walipo mshawishi ndipo akakubali akaenda na kujichovya mara SABA naye akapona.
Lakini hata Yesu ALIPO WAPONYA WATU ALIWAPA MASHARTI YA KUTO TENDA DHAMBI TENA BAADA YA UPONYAji, (Hii ni sawa na kwa babu kuambiwa unakunywa dawa mara moja, kwa maana Mungu anakuponya mara moja tu, ukirudia dhambi ukapata tena ukimwi inamaana nafasi ulipewa ukamjaribu tena Mungu) sasa hapa tofautisha kutenda dhambi nakusamehewa dhambi, na kutenda dhambi na uponyaji ni vitu viwili tofauti.
Swala la vitambaa vya mama Lwakatare, Soma Matendo 19:11-12 sasa hapo kunahitajia kana ufahamu wakiroho, maanake nirahisi sana kwa watu kutumia style hii hali hivyo vitambaa vimechakachuliwa na nguvu za giza.
Mungu awabariki wote.