Ndugu yangu, nadhani umefika njia panda kidogo. Labda nikusaidie kidogo kuhusiana na maandiko juu ya oponyaji na imani. Labda tusome Yohana 5:2 NAHUKO YERUSALEM ( Arusha, Loliondo) PENYE MLANGO WA KONDOO PANA BIRIKA, IITWAYO KWA KIEBRANIA BETHZATHA, NAYO INA MATAO MATANO. 3 NDANI YA HAYO JAMII KUBWA YAWAGONJWA WALIKUWA WAMELALA, VIPOFU, VIWETE, NAO WALIO POOZA, WAKINGOJA MAJI YACHEMKE ( wakingoja dawa ya babu ichemke). 4 KWA MAANA KUNAWAKATI AMBAPO MALAIKA HUSHUKA, AKAINGIA KATIKA ILE BIRIKA( kikombe cha babu tayari malaika alisha shuka wakati dawa ya babu inachemka), AKAYATIBUA MAJI. BASI YEYE ALIYE INGIA WA KWANZA BAADA YA MAJI KUTIBULIWA, AKAPONA UGONJWA WOTE ULIO MPATA.( hapa sasa ni tofauti na babu, kwa babu yeye sio mtu anayekunywa wakwanza dawa, bali WOOOOTE watakao kunywa dawa kwa imani ya kupona WATAPONA, HAKUNASHARTI LA MARAMOJA KWA MTU MMOJA KWA SIKU) (ENDELEA KUSOMA HADI MSTARI WA 9)[/B]. Sasa ndugu yangu, n kwamba hakuna namna, sisi wanadamu tunavyo weza kumpangia Mungu juu ya uponyaji wake, ama kufikiri Mungu anatibu kwa namna moja tu ama kama tutatakvyo taka sisi.
Pia tafakari namna NAAMAAMAN ALIVYO PONYWA UKOMA WAKE 2 Wafalme 5:1-27, hapa utaona namna Naaamana alivyo ponywa, lakini alipo pewa masharti ya kuponywa hakuamini hadi wafanyakazi wake walipo mshawishi ndipo akakubali akaenda na kujichovya mara SABA naye akapona.
Lakini hata Yesu ALIPO WAPONYA WATU ALIWAPA MASHARTI YA KUTO TENDA DHAMBI TENA BAADA YA UPONYAji, (Hii ni sawa na kwa babu kuambiwa unakunywa dawa mara moja, kwa maana Mungu anakuponya mara moja tu, ukirudia dhambi ukapata tena ukimwi inamaana nafasi ulipewa ukamjaribu tena Mungu) sasa hapa tofautisha kutenda dhambi nakusamehewa dhambi, na kutenda dhambi na uponyaji ni vitu viwili tofauti.
Swala la vitambaa vya mama Lwakatare, Soma Matendo 19:11-12 sasa hapo kunahitajia kana ufahamu wakiroho, maanake nirahisi sana kwa watu kutumia style hii hali hivyo vitambaa vimechakachuliwa na nguvu za giza.
Mungu awabariki wote.