Samahani sana mkuu yaani "babu" unataka kumfananisha na Yesu????????? Khaaaaa yaani wewe jamaa wa ajabu sana unamfananisha Messi na Ngasa?! Yesu ni world ICON huwezi kumfananisha na mtu wa kawaida mkuu..............
Mkuu hapa mwenye kuponya ni MUNGU na si Paulo. Nguvu iliyokuwa ndani ya Paulo ni nguvu ya MUNGU inayoweza kuwa ndani ya mtumishi mwingine yeyote leo akijitoa kumtumikia kisawasawa. Nguvu hiyo yaweza kuwekwa kwenye vitambaa kwa kuombewa na kupelekwa kwa wagonjwa na wakapokea uponyaji.
.
Naunga mkono hoja.
Ila katika kitabu cha biblia tunachokiamini kuna aya inawataka wanawake wenye kuukiri uchaji wafunikwe kwa mavazi ya kusitiri (dicent).
Avatar yako inaunga mkono ushauri huo?
Judy, kwanza nianze kwa kusema unafanya vema kuuliza maswali kwa mtazamo wa kitheologia kwa sababu kuuliza maswali hakumaanishi mtu hana imani, ila kama una mashaka na jambo analofanya Mungu kupitia Mchungaji Masapila katika kijiji kidogo cha Samunge hilo ni jambo lingine na unahitaji Mungu akufunulie kwani mambo haya ya imani hufahamika kwa imani. Theologia kama neno lenyewe lilivyo ni muunganiko wa maneno mawili "theos" lenye maana ya Mungu kwa lugha ya Kiyunani na "logia' lenye maana ya elimu. Muungano wa maneno haya mawili ndiyo yanayotupa neno theologia lenye maana kwa kifupi "elimu kuhusu Mungu." Kwa mantiki hiyo, si vibaya kuuliza maswali kwa sababu kuwa mkristo hakumaanishi kuamini bila kuuliza maswali yanayohusu Mungu na imani kwa ujumla kwa sababu maswali husaidia sana katika kuimarisha imani kama yanaulizwa katika msingi wa kuimarisha imani ya mtu.
Hata hivyo, inawezekana kuuliza maswali na tusipate majibu yanayotosheleza utafiti wetu ama kuridhisha akili na ufahamu wetu wa kibinadamu. Hii inatokana na ukomo (limitation) wa uwezo wa ufahamu wa kibinadamu. Judy, naamini utakubaliana nami kwamba binadamu, hata mwenye akili nyingi sana ana ukomo wa ufahamu wake. Hawezi kuelewa kila kila kitu hata mambo ya kawaida sembuse ya Mungu ambayo pasipo ufunuo wa Roho Mtakatifu ni vigumu sana kuyaelewa.
Kwa kuwa wewe ni mtheologia kwani umejitambulisha hivyo, bila shaka unafahamu kwamba Mungu amekuwa akitenda miujiza akiwatumia watu tofauti tofauti kwa nyakati tofauti na kizazi tofauti kulingana na mahitaji yao. Nionavyo mimi suala la msingi hapa siyo jinsi Mungu anavyofanya miujiza ama anamtumia nani na ni wapi ila ni yale anayofanya Mungu kupitia mtu anayemchagua. Suala lingine ni je ishara hizo zinathibitishwa kwa Neno la Mungu (Biblia) na zaidi sana ni nani anayepewa sifa, utukufu, enzi na heshima? Kwa maneno mengine, je anayetumiwa anawaongoza watu wamwone Mungu aliyemkabidhi huduma yenyewe ama anajiinua yeye mwenyewe na kujitwalia sifa? Haya pamoja na mambo mengine ambayo sitaweza kuyasema hapa yana umuhimu mkubwa katika kuchunguza huduma ama unabii uwao wote.
Ni vema pia tujihadhari sana tunapozungumza habari za Mungu kwani akili zetu za kibinadamu hazitoshi kuyafahamu mambo haya kikamilifu. Ningeshauri kwamba tuzungumze na Mungu kwa njia ya sala ili atufunulie ukweli juu ya mambo tunayoyaona na kuyasikia kama yanatokana naye ama ni unabii wa uwongo. Kufanya hivyo ni muhimu ili tusijetukagombana na Mungu. Mwisho kwa sasa ningesema kama alivyosema Gamalieli aliyekuwa Rabi aliyeheshimika na jamii ya Kiyahudi, kama kazi hii inayofanyika Samunge ni ya Mungu itasimama la kama si ya Mungu siku si nyingi itapotea na kama dawa ni sumu Mungu anao uwezo wa kuigeuza iwe chakula maana imeandikwa "mtawakanyaga nyoka na nge na nguvu za yule Ibilisi, hata mkinywa kitu cha kufisha hakitawadhuru, mtaweka mikono juu ya wagonjwa nao watapokea afya." Mungu akubariki katika kuyatafakari hayo na ingia kwenye maombi.
PHP:binafsi nashindwa kuiita karama, uwezo wa Mungu hauna mipaka ya mahali wala wakati. hainiingii akilini kwamba mti huo ukichemshwa mahali pengine nje ya kiiji cha samunge, hauponyi na babu akikuombea bila kukupa kikombe chake kwa mkono wake huponi!
Mbona huulizi kwanini yesu alipokuwa anaponya watu mfano alipokuwa anamponya yule kipofu alichukua mate akachanganga na udongo akapaka machoni pa yule jamaa na akaona. Mbona asimwambie ona tu na akaona. Au mbona Yesu alipokuwa harusini mjini kana aliwaambia watu wajaze maji yale mapipa, mbona huulizi asingeeamuru tu mapipa yajae divai? So hili ni swala la imani and the way it is executed sioni shida, it depends Mungu anataka adhihirike vipi na wapi na kwa namna gani. So kwa kuwa ni swala la imani then sioni sababu ya kuhoji mashart ya Babu...
thanks my dear. ubarikiwe sana.
mi hoja yangu ni kuwataka wote tuwe na kawaida ya kutafakari na kujaribu (ku-test) kila kinachoitwa revelation. kupokea tu ndoto au ufunuo eti kwa kuwa imekuja "kupitia mchungaji" ni kukubali bila sababu yoyote kuwa we are not resposible Christians. hao wanaonishambulia eti nampinga au namhoji Roho Mtakatifu na kunukuu mafungu tele tele ya biblia, wamerukia tu kuhitimisha kuwa "......hiyo ni kazi ya Roho Mtakatifu" bila kui-test! na hii ni hatari kwani siku moja hata shetani ataleta ndoto (na amekwishaleta nyingi sana) na watu watajazana kwake na hatimaye kuangamia pamoja naye kwa kukosa maarifa.
kumbukeni kuwa imani ya kikristo ni tofauti na imani nyingine. hii inaanzia kwenye (brain) rationality na kukua kuelekea spirituality na si kinyume chake. wote wanaokimbilia kusema kuwa "masuala ya imani magumu kueleweka" au "Roho Mtakatifu ana namna nyingi za kutenda kazi na ni ngumu kuzielewa kwa akili zetu" nk wanakimbia wajibu wao. wanajaribu kutuaminisha kuwa imani ya kikristo huanzia kwenye spirituality kushuka chini kwenye brain (rationality), na hivyo haiwezekani kuzielewa basis za imani!. ni uongo mkubwa sana huu na ni silaha ya ibilisi ili watu waangamie kwa kukataa kwa makusudi kutafuta maarifa.
ufunuo wowote unaokuja nje ya neno la Mungu haupaswi kupita bila kuhojiwa. Roho Mtakatifu si lazima adhihirishwe kwa miujiza. Mungu hujishughulisha na kuponya roho na si kuponya Mwili. hata pale mwili unapopona ni kwa sababiu roho imepona na hivyo uponyaji wa rohoni umepelekea uponyaji wa mwili. uponyaji wowote uanziao kwenye mwili bila kuzingatia uponyaji wa roho, ni wa kuhojiwa.
neno la Mungu ni kamili na halihitaji miujiza ili liwe kamili au lipate nguvu. kama maelfu ya watu wamiminikao loliondo leo wamekuwa wakisikia injili kila siku wasiamini, ila leo wakasema wanaamini kwa sababu wameona ishara ya dawa ya ajabu, basi hilo haliwezi kupita bila kuhojiwa na wenye kuamini neno la kweli. pia haijathibitika kuwa wote wanywao ule mti humrudia Mungu kwa toba bali inajulikana kuwa kila anywaye hujiondokea zake na habari kuishia hapo. Mungu ninayemfahamu hana tabia hiyo.
neno la Mungu liiko wazi, alikuja kuokoa na kutafuta kilichopotea, na ndio maana hata wakati wa Yesu ama Elisha (kama wengi walivyotoa mifano ya Naamani mshamu aliyeponywa ukoma na wengine walioponywa) si kila aliyekuwa na ukoma laiponywa! tafakarini sana hapo ndugu zangu.
Yesu mwenyewe alituonya mara nyingi sana tusiwe vipofu na kutahadharisha kuwa kipofu akimongoza kipofu mwenzie, wote watatumbukia shimoni. kwa msingi huuu, ni wajibu wa mkristo kuzijaribu kila roho ili kuona kuwa zimetokana na Mungu.
mwenye kuweza kutafakari na atafakari. mimi nimetimiza wajibu wangu
Glory to God
Dada Judith,
Mambo ya MUNGU hayapimwi kwa theolojia hata kidogo bali kwa ROHO MTAKATIFU. Tunahitaji kukaa sana katika uwepo wa MUNGU maishani mwetu ili ROHO MTAKATIFU atufunulie ni kipi cha kweli na kipi si cha kweli vinginevyo twaweza kujikuta tukataa huduma ya MUNGU au kukubali huduma isiyotokana na MUNGU. Kuhusu suala la vitambaa yaweza ikawa si MUNGU kama mtumishi mwenyewe hayuko na MUNGU na inaweza ikawa ni MUNGU kama mtumishi mhusika yuko na MUNGU vizuri maana tunaona hata enzi za mtumishi wa MUNGU Paulo watu waliponywa kwa vitambaa.
Acts 19 (Amplified Bible)
11And God did unusual and extraordinary miracles by the hands of Paul,
12So that handkerchiefs or towels or aprons which had touched his skin were carried away and put upon the sick, and their diseases left them and the evil spirits came out of them
Judith, I think you need to remember that God the Father of our Lord Jesus Christ is an unlimited God. I agree with you that every prophecy and everything we do must be proved by the Scriptures (Bible) for it is in Scripture the whole revelation of God is revealed. However, God is unlimited and dreams have been one of the ways that God revealed to His people and this God has never changed. He is the same God who was who is and ever shall be. Kwa hiyo Mungu anaweza kujifunua hata leo kwa njia apendayo na mara nyingi hujifunua kwa watu wasiokuwa na umaarufu kama Mch. Masapila ambaye watu wengi wanakuwa na mashaka juu ya huduma anayoifanya. In healing foe example, Jesus himself use different ways to heal the sick his word (speech) being the first way. But He also used different means. In healing the blind man He used the soil by making mud and applied to the eyes of the blind man and he was able to see or in other words his sight was restored. In other occassions He only touched the sick and their health was restored immediately. Another example is that of a woman who suffered from bleeding for more than a decade who said in her heart if I go and touch His garment I will get well. She did and indeed her health was resotred. Healing took place even before the earthly ministry of Jesus at Siloam etc. So you see this is a God who is unlimited by our understanding of who He really is. Therefore, let us not limit God by our meager understanding of Scripture because God is above our human understanding. I agree with you on having the knowledge of Scripture but don't forget that God also speaks to us when we pray and that is why prayer for a Christian is mandatory. Prayer is a special way through which we hear God and God listens to us. So, my dear sister do not undermine the role of prayer in your Christian life. So, my sister in Christ I beseech you in the name of Jesus to pray for it is in this way, along with the understanding of Scriptures that we can understand the things that are God's and the things that are not of God. I wish you God's peace which surpasses all understanding as you continue on with your spiritual journey.
PHP:binafsi nashindwa kuiita karama, uwezo wa Mungu hauna mipaka ya mahali wala wakati. hainiingii akilini kwamba mti huo ukichemshwa mahali pengine nje ya kiiji cha samunge, hauponyi na babu akikuombea bila kukupa kikombe chake kwa mkono wake huponi!
Mbona huulizi kwanini yesu alipokuwa anaponya watu mfano alipokuwa anamponya yule kipofu alichukua mate akachanganga na udongo akapaka machoni pa yule jamaa na akaona. Mbona asimwambie ona tu na akaona. Au mbona Yesu alipokuwa harusini mjini kana aliwaambia watu wajaze maji yale mapipa, mbona huulizi asingeeamuru tu mapipa yajae divai? So hili ni swala la imani and the way it is executed sioni shida, it depends Mungu anataka adhihirike vipi na wapi na kwa namna gani. So kwa kuwa ni swala la imani then sioni sababu ya kuhoji mashart ya Babu...
Umenena vema mkuu. Nadhani tuache kupiga mayowe si muda mrefu tutayaona wenyewe(ushuhuda). Miujiza ya Mungu wa Ibrahim,Isaka na Yakobo huwa haiji kwa kifichokificho na haihitaji marketing wala propaganda. It is just a matter of time when waliopona kweli tutawaona na kama hawajapona tutawajua!
Samahani sana mkuu yaani "babu" unataka kumfananisha na Yesu????????? Khaaaaa yaani wewe jamaa wa ajabu sana unamfananisha Messi na Ngasa?! Yesu ni world ICON huwezi kumfananisha na mtu wa kawaida mkuu..............
kumbe huwa tunawalaumu baadhi ya wasilamu kuwa wanarukia kunukuu mstari mmoja wa Biblia na kung'ang'ana nao bila kujua maana yake na wakati huohuo tuna wakristo chungu mzima wasio na uelewa wowote wa maandiko! watumishi wa Mungu ongezeni bidii na kazi ya Bwana, mavuno ni mengi ila watenda kazi ni wachache
Glory to God
jana nilikuwa naangalia EMMANUEL TV ya TB JOSHUA kwa wale wanaofuatilia yeye anaponya kwa ktumia maji yanaitwa anointed water ssa hivi kaleta mpya ipo kwenye chupa ndogo saana km zile za rangi ya kucha. sasa alichosema ni kuwa ile chupa alibidi iwe tupu lkn alimwomba mungu aweke maji kwa vile kizazi hiki kisicho na imani wala matumaini itakuwa vigumu kuamini so mle ndani kuna maji na yana nguvu ya ajabu. hapa nataka kuwaambia wale wasio na imani kwamba babu anaponya kwa kile kikombe na mizizi ile ikishabarikiwa inakuwa na nguvu ya ROHO MTAKATIFU wewe binadanu wa kawaida unaona maji ya kawaida lkn ROHO MTAKATIFU anakuwepo pale kukupa wewe uponyaji
The new testament asks us to question the spirits in operation. All miracles performed after redemption were through the name of Jesus which is the power above all in heavens and on earth. Its important to note that during Jesus time so was during prophets and priests before He came used media to perform miracles because the holly spirit was not yet released into the world. Alikuwa anavuvia watu au vitu na hivyo kusababisha miracle kutokea; lakini sasa yupo available in whoever believeth in the above all name Jesus. Hahitaji tena hizo media for our bodies are His temple and he uses our body organs to perform miracles. Bali katika yote bado nguvu na uweza una yeye Mungu wetu; kama la toka kwa Ibilisi halitadumu na itaonekana wazi lakini kama ni la Mungu basi If God say yes who can be against?
Hapo kwenye blue ndo msisitizo the power was in Paul na siyo handkerchiefs...Hata kunasehemu kivuli chake kilipomgusa mtu alipata uponyaji...Nasisitiza roho matakatifu yupo ndani yetu sasa hivi kama alivyokuwa kwa Yesu so its not about media its about the power that worketh in us...ndiyo maana nashindwa kum qualify mchungaji/babu au kum disqualify maana anasema dawa lazima akupe kwa mkono wake which means the power is inside him...Lakini pia a devil can do miracles in the same maner ndiyo maana lazima tuipe muda ili kweli ijidhirishe huku tukiendelea kuomba..Kitu kingine ni kuwa ili uwe muujiza wakimungu lazima uthibitishwe na vitu vitatu so far Babu peke yake ndiyo mwenye revelation why? Hii ni kanuni ya Mungu kwamba ushuhuda wa watu watatu ndiyo kamili...Time will tell.
Kinacho nitatiza mimi ni kwanini babu hataki Jina la Yesu litukuzwe? Naamini tunatakiwa kulikiri jina lake na kumtukuza yeye kwa mema aliyotutendea.pamoja na ukweli kuwa hekima ya Mungu surpases all our undeerstanding, bado we can undersatnd Him and his plan to the extent of His revelation through the scriptures. he revealed Himself to us so that we can be the sons and doughters of the light. His word gives us sight so that we no longer move and live on earth as blinds, but as people acquaited with all understanding and wisdom to his own glory.
Glory to God
Hicho ni kitu kingine kinacho nitatiza kwasababu tulipewa Roho Mtakatifu ili atusaidie tunachotakiwa ni kuliita jina lake wakati wowote kwa imani naye atatenda kwasababu yeye ni mwaminifu.kwa mujibu wa BBC, mch. mwasapile alisema si maji yale yanayoponyesha bali ni maombi. sasa mi najiuliza iweje neema ya Mungu ya uponyaji ijifungamanishe na maji kiasi kile? tena kiasi cha kwamba bila hayo maji neema hiyo haifanyi kazi?
Mimi naona kama imani ya uponyaji kwa babu inawekwa kwenye kikombe zaidi kuliko Roho Mtakatifu kitu ambacho si sahihi. Hii inanitatiza sana.
Amen
Ubarikiwe ndugu yaani hapo uliposena ni kweli kabisa. Kinacho nitatiza mimi ni kwanini babu hataki Jina la Yesu litukuzwe? Naamini tunatakiwa kulikiri jina lake na kumtukuza yeye kwa mema aliyotutendea. Hicho ni kitu kingine kinacho nitatiza kwasababu tulipewa Roho Mtakatifu ili atusaidie tunachotakiwa ni kuliita jina lake wakati wowote kwa imani naye atatenda kwasababu yeye ni mwaminifu.
Unarikiwe Miss Judith kwa kuleta mada hii.
asante sana mpendwa chamoto. picha inayokuja kwa haraka hapa ni kuwa wakristo tunapaswa kujua nini mapenzi ya Mungu katika maisha yetu na namna mapenzi hayo yanavyotimizwa kupitia baraka za Neno la msalaba. vinginevyo tutakuwa tunamsingizia Roho Mtakatifu kuhusika na kila kitu tusichokielewa au tunachokiendekeza kwa kushindwa kwetu kutafakari vyema juu ya wokovu wetu.
wengi wamekurupuka kuamini kuwa kwa kuwa tiba ya loliondo imeleta faraja kwa waliokuwa wakiteseka na magonjwa, basi imetoka kwa Mungu bila hata kuijaribu hiyo roho ya ufunuo kama inatokana na Mungu. kwamba ufunuo (ndoto) imekuja kupitia mchungaji mstaafu hakutoi uthibitisho wa moja kwa moja kuwa ndoto ile ilitoka kwa Mungu. hata shetani kishatumia watu wengi wanaojiita wachungaji/maaskofu kufanya kazi zake na wengine tunawajua. hivyo ni muhimu tukazijaribu hizi roho kabla ya kuzitukuza na kujishirikisha nazo. na njia pekee ya kuzijaribu ni kutumia maneno ya Mungu.
kama tiba hii au nyingine yoyote iliyokwishatokea na itakayotokea duniani haiko consistent na maneno ya Mungu, mimi katu sitajishirikisha nayo wala kuitukuza hata ningekuwa nimesongwa na shida na maradhi ya namna gani. nitamtukuza Mungu wangu siku zote, iwe katika magonjwa, afya, tabu, misiba, katika kunenwa vyema na kunennwa vibaya nk, ili utumishi wangu usije ukalaumiwa siku ya kuja kwake (2 Corinthians 4-10). amina
kwa kweli ingekuwa makosa sana kuliacha jambo hili likapita hivihivi tu bila kulihoji eti kwa sababu tu limeshabikiwa na wengi.
ubarikiwe sana mpendwa, tuendelee na mjadala
Glory to God