Mch Peter Msigwa: Serikali na Rais Samia Suluhu Hassan, swallow your pride & ego. Mwachieni Tundu Lissu, hana hatia..!

Mch Peter Msigwa: Serikali na Rais Samia Suluhu Hassan, swallow your pride & ego. Mwachieni Tundu Lissu, hana hatia..!

The Palm Beach

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
4,249
Reaction score
11,592

View: https://youtu.be/MlQRJzlk_JM?si=6mw_RwolPu_sNa9P
Ameyasema haya leo akiongea na waandishi wa habari huko Iringa.

Ameitaka serikali chini ya CCM ikiongozwa na Rais Samia kuweka kiburi na majivuno (pride & ego) pembeni na wasione haya, soni wala aibu kukiri kuwa wameshindwa, wamwachie Tundu Lissu with immediate effect bila masharti yoyote kwa sbb hana hatia..

Amesema, ishu ya Tundu Lissu wala sio ya kisheria wala la kimahakama bali CCM na viongozi wao wanalipa sura ya kisheria na kimahakama kama egemeo tu katika kujitetea kwao huku waki - buy time pengine wakidhani kuwa utafika wakati watatekeleza ajenda yao ovu ya kumuua mtu huyu asiye na hatia...

Ushahidi ni kuwa sasa ni zaidi ya siku 450 Tundu Lissu Yuko gerezani. Kesi haiendelei kwa sbb iko wazi kuwa mtu huyu hana kosa na hivyo ushahidi wa kumtia hatiani haupo. Na bahati mbaya kuwa, mahakama nayo imeshindwa kufanya maamuzi ya kutoa haki kwa sbb imebanwa pua, ikashikiliwa miguu na mikono na hawahawa wanaomuweka gerezani (Samia na serikali yake). Kila mtu ndani ya CCM, serikali na raia wa kawaida anajua kuwa hii ni kesi ya Samia na serikali yake....

Aidha, jumuiya za kimataifa UN, AU, European Union, Commonwealth, Amnesty International, nchi washirika na wahisani wa maendeleo ya nchi yetu kama USA, UK, Germany zinajua na ndio maana zinatoa matamko na mengine yakiwa magumu kwelikweli kumeza...

Ameendelea kusema, kwa sasa mikakati inaendelea kusukwa chini kwa chini kufanya CHADEMA na viongozi wake waonekane kama kuomba msamaha ili iwe kama gateway kumfanya Samia mtakatifu na aliowaonea wana makosa..

Mch Peter Msigwa amesema, kwa anavyomfahamu Tundu Lissu, wasahau hilo. Hawezi kuomba radhi kwa kosa lisolokuwepo...

Amemaliza kwa kutolea mfano wa kisa cha Mfalme Sauli na Saudi. Kwamba, Mungu alimkataa Mfalme (Rais) Sauli wa Israel kwa sbb ya kiburi, ego, ukatili na kukosa utii...

Huyu mfalme (Rais) Sauli akiwa bado madarakani, Mungu akamtia mafuta Mfalme mwingine (Daud) kuwa Rais badala ya Sauli...

Rais Sauli akiwa angali madarakani bado na madaraka ya u - Rais mikononi mwake akajua kuwa, huyu Daudi kwa umaarufu wake na kupendwa na watu, anaweza kunitoa madarakani...

Ili kulinda cheo chake na madaraka yake ya u - Rais akaanza kufanya vita na Daudi akitafuta kila njia ya kumuua asifanikiwe bila kutambua kuwa, anayetaka kumuua Yuko chini ya ulinzi wa aliye mkuu na juu kuliko wote..

Scenario ya Sauli na Daud ndiyo inafanana kwa kiasi kikubwa na Samia/CCM vs Tundu Lissu/CHADEMA...!

Akamalizia hapo Mch. Peter Msigwa
============​
MY COMMENTS
Mfano wa Mfalme Sauli na Daudi, umetolewa pia na Askofu & Mch Josephat Gwajima several times...

Yeye hayuko direct kama alivyofanya Mch Peter Msigwa leo bali anaongea kwa "code" za kiroho...

Ni wenye ufahamu wa ndani tu ndio watamwelewa. Lakini ukweli ni kuwa, kila kitu kinahusu hatima ya utawala wa CCM/Samia!
 
Samia alidhani utawala wake utakuwa rahisi baada ya kuua watu Oct 29
 
Ukweli ulio wazi.
Na naona harakati zimekuwa nyingi si punde mwamba atatoka.
 
Jiwe linalopigwa na nyundo kila siku hata kama halionekani kuvunjika kuna siku litapigwa kidogo tu litavunjika.
Haya mambo ya tarehe za maandamano zinatangazwa hakuna kinachotokea si mazuri kujirudia rudia.
Kesi iitwe maamuzi yatoke apate haki yake nchi ipunguze sababu za watu kutishia kuandamana.
 
Back
Top Bottom