Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,036
- 9,331
- Thread starter
- #21
Umenena Kaburunye, neno lako ni sawia
Umegongelea kwenye, kichwa na kwenye mkia
Umewatoneshe penye, donda wanaugulia
Dokta ndiye daktari, wa Kuponya Tanzania
Jibaba Bonge kamili, hoja yako ni murua
nimekubali mswahili, sistimu kuifumua
ni ukombozi wa pili, hapana kusuasua
Dokta ndiye daktari, wa kuponya Tanzania
Ogah jembe makini, umelonga kwa hisia
kwayo yako tathmini, Ikulu tutaingia
CCM haijiamini, ndo mana wanalia
Dokta ndiye daktari, wa kuponya tanzania.
Anysile mtaalamu, sina cha kuongezea
Yako ni nyingi ilimu, jinsi ulivyoelezea
Tutaishika hatamu, CCM tajiondokea
dokta ndiye daktari, wa kuiponya tanzania
Wambugani ncha kali, mzalendo mtanzania
tungo zako za akili, zenye uchungu na nia
wasikika toka mbali, kila pembe ya dunia
dokta ndiye daktari wa kuiponya Tanzania
Kamanda Kidundulima, umetuonyesha njia
Kamwe haturudi nyuma, wito tunaitikia
Kina baba kina mama, na vijana wote pia
dokta ndiye daktari, wa kuponya Tanzania
Unatisha sana Nyunyu, ulosema yaningia
we ni mvua si manyunyu, hazina ya Tanzania
tutawakwanyua kwanyu, kura sitowapigia
dokta ndiye daktari wa kuponya Tanzania
Golder maji ya dhahabu, nawe nakukubalia
yafaa tuwaadhibu, kura kutowapatia
kwani wametughilibu, miaka mingi twaumia
dokta ndiye daktari wa kuponya tanzania