Mchakato Ujenzi wa Kiwanda cha Kuchambua Mbegu za Pamba Igunga Waanza

Mchakato Ujenzi wa Kiwanda cha Kuchambua Mbegu za Pamba Igunga Waanza

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

"MCHAKATO UJENZI WA KIWANDA CHA KUCHAMBUA MBEGU ZA PAMBA IGUNGA WAANZA "
Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Mohamed Bashe amemuhakikishia Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus George Ngassa kuwa mchakato wa ujenzi wa kiwanda cha kuchambua mbegu za Pamba umeanza na sasa hatua za awali zinaendelea vizuri kwenye ngazi za maamuzi.

Mhe. Bashe (MB) ametoa rai hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus George Ngassa kuhusu maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kuchambua pamba kwenye Mkutano wa Wadau wa Tasnia ya Pamba kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Hotel ya Morena Jijini Dodoma.

Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka mkazo wa ujenzi wa kiwanda cha kuchambua mbegu za Pamba kwenye Wilaya ya Igunga ikiwa ni ukanda unaofanya vizuri kwenye kilimo cha Pamba na kufanya vizuri kama kitalu cha mbegu za Pamba.

WhatsApp Image 2024-03-24 at 09.33.05.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-24 at 09.33.06.jpeg
 
Naomba msaada wa kupata bei za pamba kutoka mwaka 1993 hadi 2023
 
Jamani naomba mwenye kufahamu, upatikanaji WA mbegu za pamba anijuze. Napatikana MKOA WA GEITA WILAYA YA NYANG'HWALE
 
Back
Top Bottom