Mchakato wa Katiba Mpya Senegal Sio Lelemama: Je, Unaweza Kukata Tawi Ulilokalia?

Fascinating

Senior Member
Joined
May 14, 2025
Posts
146
Reaction score
351
Wakuu, ni wazi kabisa kwamba mchakato wa kusuka Katiba Mpya barani Afrika sio lelemama hata kidogo. Tukio la jana, Juni 29, 2026, kwenye Bunge la Senegal limebainisha wazi kuwa safari hii sio lelemama, yaaani bunge liligeuka uskiku wa vitasa! Kushikana mashati, kusukumana, na kurushiana maneno mazito kisa tu mabadiliko ya mfumo wa utawala. Hali ambayo ndugu yetu Muliro huiita "taharuki"

Hekaheka hii ina mzizi mrefu wa kihistoria na funzo kubwa sana kwa siasa za Afrika, hususan kwetu sisi huku Afrika Mashariki. Na kuifahamu vizuri ni lazima tuanze kujaza mapengo yote ya kihistoria ili tuelewe kwa nini Senegal ipo kwenye hali ya sasa.

Juni 29, 2026: Kile Kilichojiri Bungeni

Mambo yalianza pale Mbunge wa Upinzani, Abdou Mbow ambaye ni mshirika wa karibu wa Rais wa zamani Macky Sall na chama chake cha APR (Alliance for the Republic) alipowasilisha hoja ya dharura ya kutaka kusitisha kikao hicho. Baada ya kuwasilisha hoja hiyo, Mbow alikaidi utaratibu na kugoma kabisa kuondoka kwenye Podium, huku akirusha matusi mazito na kashfa kwa wabunge wa chama tawala cha PASTEF.

Spika wa Bunge, Ousmane Sonko (ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani na nguzo kuu ya chama tawala), aliamuru maikrofoni ya Mbow izimwe mara moja na kumtaka ashuke. Mbow alipogoma, na ndipo ukumbi ulilipuka misuguano kati ya wabunge wa pande zote mbili.

Ili kurejesha amani, Sonko alilazimika kuwaita askari wa usalama wa bunge (National Gendarmerie), ambao waliingia ukumbini na kumkokota Mbow nje kwa nguvu. Katika hatua ya kulalamikia kitendo hicho, wabunge wote wa upinzani walisusia kikao na kutoka nje. Hatua hii iliuachia muungano wa PASTEF uwanja mweupe na kufanikiwa kupitisha Mswada Na. 11/2026 kwa kura zote za "ndio" bila kupingwa. Wakati hayo yakijiri ndani, nje ya bunge polisi walikuwa wakipambana na waandamanaji wa upinzani kwa mabomu ya machozi.

Kiini cha Misuguano: Mswada Namba. 11/2026 na "Systemic Rupture"

Chama tawala cha PASTEF, chini ya Rais Bassirou Diomaye Faye, kiliahidi mabadiliko makubwa ya kimfumo (Systemic Rupture). Katiba ya sasa ya Senegal inampa Rais madaraka makubwa mno (Hyper-presidential system) mfumo ambao mara nyingi umekuwa ukitumiwa na vyama tawala barani Afrika kujilinda na kukandamiza demokrasia.

Mswada huu mpya unaenda kupasua majipu yafuatayo:

  • Kusawazisha Madaraka: Unapunguza nguvu za Rais na kuongeza mamlaka ya usimamizi na udhibiti kwa Bunge la Kitaifa na Waziri Mkuu.
  • Kutenganisha Chama na Serikali: Rais aliyeko madarakani anapigwa marufuku kuongoza chama cha siasa. Mawaziri pia hawaruhusiwi kuwa wabunge kwa wakati mmoja.
  • Mageuzi ya Kimahakama: Baraza la sasa la Katiba (Constitutional Council) ambalo limekuwa likilalamikiwa kwa kuegemea upande wa Rais, linafutwa na nafasi yake kuchukuliwa na Mahakama mpya ya Katiba (Constitutional Court) inayojitegemea kikamilifu ili kusimamia migogoro ya uchaguzi.
  • Sauti ya Mwisho kwa Wananchi: Kutokana na uzito wa mabadiliko haya, Rais Faye ametangaza kuwa mswada huu utapelekwa kwenye Kura ya Maoni (Referendum) ili wananchi waamue wenyewe.
Uhusiano wa Kihistoria na ufanano wake na hapa kwetu "Malawi"
Hawa wanaopinga mswada huu (chama cha APR cha Macky Sall) ni wanufaika wakubwa wa mfumo wa zamani. Tukirudi nyuma kidogo katika historia ya Senegal:

  1. Enzi za Chama Kimoja: Léopold Sédar Senghor alitawala kupitia chama cha UPS (baadaye PS) katika mfumo wa chama kimoja. Mnamo 1974, alianzisha marekebisho ya kuruhusu vyama vingi kwa uchache, mfumo uliokuja kuwa huru kabisa chini ya mrithi wake, Abdou Diouf, mnamo 1981.
  2. Ujio wa PDS na APR: Chama cha PDS (Parti Démocratique Sénégalais) cha Abdoulaye Wade kiliingia madarakani mwaka 2000 na kuondoa utawala wa miongo minne wa chama cha kijamaa (PS). Mwaka 2008, Macky Sall alijitenga na PDS na kuunda APR, na kuja kushinda urais mwaka 2012.
Makosa Makubwa ya PDS na APR: Walipoingia madarakani, walilewa utamu wa "Katiba ya kifalme" waliyoikuta. Badala ya kuibomoa ili kuweka uwanja sawa wa kisiasa, waliitumia kukandamiza wapinzani wao (ikiwemo kumfunga na kumtesa Ousmane Sonko miaka michache iliyopita). Ndio maana leo hii wakiwa upinzani, wanapambana kufa na pona kuuzuia mswada huu kwa sababu unawanyang'anya "fimbo" waliyotegemea kuitumia pindi wakirudi madarakani.

Ulinganifu wa Nyumbani: Hii ni sawa na kusema siku ya siku itokee shishi-M ishindwe uchaguzi mkuu kule Malawi kisha chama kipya cha upinzani kikiingia madarakani kiamue kufuta kabisa yale madaraka ya ki-Mungu aliyonayo Rais kwenye Katiba ya sasa ya Malawi (kama vile kuteua wakurugenzi, majaji, na wakuu wa mikoa). Ni wazi kuwa shiwhi-M, ikiwa upinzani, itapambana dhidi ya mabadiliko hayo kwa sababu itakuwa inapoteza zana ya kifalme iliyoizoea.

Hii inatupa somo moja kubwa: Sio rahisi kupata mabadiliko ya kweli kama hamjashika kijiti. Wanufaika wa mfumo hawawezi kamwe kuwa mawakala wa mabadiliko. Ili kupata Katiba bora, lazima kwanza uwaondoe madarakani wale wanaolindwa na katiba mbovu.

Soma pia SENEGAL: Mtifuano wa kisiasa waendelea kati ya Sonko na Diomaye
 
Wakuu, ni wazi kabisa kwamba mchakato wa kusuka Katiba Mpya barani Afrika sio lelemama hata kidogo. Tukio la jana, Juni 29, 2026, kwenye Bunge la Senegal limebainisha wazi kuwa safari hii sio lelemama, yaaani bunge liligeuka uskiku wa vitasa! Kushikana mashati, kusukumana, na kurushiana maneno mazito kisa tu mabadiliko ya mfumo wa utawala. Hali ambayo ndugu yetu Muliro huiita "taharuki"

Hekaheka hii ina mzizi mrefu wa kihistoria na funzo kubwa sana kwa siasa za Afrika, hususan kwetu sisi huku Afrika Mashariki. Na kuifahamu vizuri ni lazima tuanze kujaza mapengo yote ya kihistoria ili tuelewe kwa nini Senegal ipo kwenye hali ya sasa.

View attachment 3619223

Juni 29, 2026: Kile Kilichojiri Bungeni

Mambo yalianza pale Mbunge wa Upinzani, Abdou Mbow ambaye ni mshirika wa karibu wa Rais wa zamani Macky Sall na chama chake cha APR (Alliance for the Republic) alipowasilisha hoja ya dharura ya kutaka kusitisha kikao hicho. Baada ya kuwasilisha hoja hiyo, Mbow alikaidi utaratibu na kugoma kabisa kuondoka kwenye Podium, huku akirusha matusi mazito na kashfa kwa wabunge wa chama tawala cha PASTEF.

Spika wa Bunge, Ousmane Sonko (ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani na nguzo kuu ya chama tawala), aliamuru maikrofoni ya Mbow izimwe mara moja na kumtaka ashuke. Mbow alipogoma, na ndipo ukumbi ulilipuka misuguano kati ya wabunge wa pande zote mbili.

Ili kurejesha amani, Sonko alilazimika kuwaita askari wa usalama wa bunge (National Gendarmerie), ambao waliingia ukumbini na kumkokota Mbow nje kwa nguvu. Katika hatua ya kulalamikia kitendo hicho, wabunge wote wa upinzani walisusia kikao na kutoka nje. Hatua hii iliuachia muungano wa PASTEF uwanja mweupe na kufanikiwa kupitisha Mswada Na. 11/2026 kwa kura zote za "ndio" bila kupingwa. Wakati hayo yakijiri ndani, nje ya bunge polisi walikuwa wakipambana na waandamanaji wa upinzani kwa mabomu ya machozi.

Kiini cha Misuguano: Mswada Namba. 11/2026 na "Systemic Rupture"

Chama tawala cha PASTEF, chini ya Rais Bassirou Diomaye Faye, kiliahidi mabadiliko makubwa ya kimfumo (Systemic Rupture). Katiba ya sasa ya Senegal inampa Rais madaraka makubwa mno (Hyper-presidential system) mfumo ambao mara nyingi umekuwa ukitumiwa na vyama tawala barani Afrika kujilinda na kukandamiza demokrasia.

Mswada huu mpya unaenda kupasua majipu yafuatayo:

  • Kusawazisha Madaraka: Unapunguza nguvu za Rais na kuongeza mamlaka ya usimamizi na udhibiti kwa Bunge la Kitaifa na Waziri Mkuu.
  • Kutenganisha Chama na Serikali: Rais aliyeko madarakani anapigwa marufuku kuongoza chama cha siasa. Mawaziri pia hawaruhusiwi kuwa wabunge kwa wakati mmoja.
  • Mageuzi ya Kimahakama: Baraza la sasa la Katiba (Constitutional Council) ambalo limekuwa likilalamikiwa kwa kuegemea upande wa Rais, linafutwa na nafasi yake kuchukuliwa na Mahakama mpya ya Katiba (Constitutional Court) inayojitegemea kikamilifu ili kusimamia migogoro ya uchaguzi.
  • Sauti ya Mwisho kwa Wananchi: Kutokana na uzito wa mabadiliko haya, Rais Faye ametangaza kuwa mswada huu utapelekwa kwenye Kura ya Maoni (Referendum) ili wananchi waamue wenyewe.
Uhusiano wa Kihistoria na kwa kufananisha na hapa kwetu "Malawi"
Hawa wanaopinga mswada huu (chama cha APR cha Macky Sall) ni wanufaika wakubwa wa mfumo wa zamani. Tukirudi nyuma kidogo katika historia ya Senegal:

  1. Enzi za Chama Kimoja: Léopold Sédar Senghor alitawala kupitia chama cha UPS (baadaye PS) katika mfumo wa chama kimoja. Mnamo 1974, alianzisha marekebisho ya kuruhusu vyama vingi kwa uchache, mfumo uliokuja kuwa huru kabisa chini ya mrithi wake, Abdou Diouf, mnamo 1981.
  2. Ujio wa PDS na APR: Chama cha PDS (Parti Démocratique Sénégalais) cha Abdoulaye Wade kiliingia madarakani mwaka 2000 na kuondoa utawala wa miongo minne wa chama cha kijamaa (PS). Mwaka 2008, Macky Sall alijitenga na PDS na kuunda APR, na kuja kushinda urais mwaka 2012.
Makosa Makubwa ya PDS na APR: Walipoingia madarakani, walilewa utamu wa "Katiba ya kifalme" waliyoikuta. Badala ya kuibomoa ili kuweka uwanja sawa wa kisiasa, waliitumia kukandamiza wapinzani wao (ikiwemo kumfunga na kumtesa Ousmane Sonko miaka michache iliyopita). Ndio maana leo hii wakiwa upinzani, wanapambana kufa na pona kuuzuia mswada huu kwa sababu unawanyang'anya "fimbo" waliyotegemea kuitumia pindi wakirudi madarakani.

Hii inatupa somo moja kubwa: Sio rahisi kupata mabadiliko ya kweli kama hamjashika kijiti. Wanufaika wa mfumo hawawezi kamwe kuwa mawakala wa mabadiliko. Ili kupata Katiba bora, lazima kwanza uwaondoe madarakani wale wanaolindwa na katiba mbovu.
Angalia watanganyika tulivyo hovyo. One of the best thread leo ni jii. Ina ujumbe wote ambao chadema wanaupigania. Hakuna aliye comment au kutoa maoni! Mbuzi mbuzi tupu pumbavu
 
Kwahiyo Faye na Sonko ni wanademokrasia wa kweli! Tazama wapo madarakani lakini wanataka mabadiliko ya katiba yatakayowanufaisha Wasenegali wote hadi wapinzani. Wakati huohuo wapinzani hawataki mabadiliko hayo kwa sababu wanaamini ipo siku watarudi madarakani na kuendelea kuminya demokrasia!
 
Kazi kweli kweli
 
Mswada huo utasainiwa na nani Sasa?.
 
Angalia watanganyika tulivyo hovyo. One of the best thread leo ni jii. Ina ujumbe wote ambao chadema wanaupigania. Hakuna aliye comment au kutoa maoni! Mbuzi mbuzi tupu pumbavu
Shida ni kulinganisha democracy ya hai jamaa na hi chaos

Umenajisi thread
 
Kwahiyo Faye na Sonko ni wanademokrasia wa kweli! Tazama wapo madarakani lakini wanataka mabadiliko ya katiba yatakayowanufaisha Wasenegali wote hadi wapinzani. Wakati huohuo wapinzani hawataki mabadiliko hayo kwa sababu wanaamini ipo siku watarudi madarakani na kuendelea kuminya demokrasia!
Ni mageuzi mühimu

But are Senegalese happy?
 
Ni mageuzi mühimu

But are Senegalese happy?
Wengi wana furaha na kazi ya kiongozi ni kuwaongoza wananchi wafikie malengo mazuri lakini viongozi wa upinzani hawataki mabadiliko chanya
 
Back
Top Bottom