Mkuu muswada unaotarajiwa kuletwa bungeni, pamoja na mambo mengine unapashwa kutoa utaratibu rasmi utakaotumika siyo tu katika kukusanya maoni ya wananchi, lakini pia namna maoni hayo yatakavyoratibiwa na hatimaye kujumuishwa katika rasimu ya katiba itakayoandikwa kufuatia ukusanyaji wa maoni hayo. Hivyo kwasasa kazi ilyoko mbele ya sisi zote wenye mapenzi mema na taifa ili, ni kufanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba sheria itakayotungwa na bunge baada ya kuwasilishwa kwa muswada huo inatoa fursa na uhuru wa kweli kwa raia wote kushiriki katika mchakato uandikaji wa katiba mpya.