Hii inaweza kuongeza demokrasia ndani ya vyama vya upinzani
Tunadai tume huru ya Taifa na mazingara sawa ya kufanya kampeni lakini nyingi za vyama vya siasa hazileti uhuru wa kutoa mawazo!!
Tume nyingi ndani ya vyama vya siasa zinalinda Wakubwa na waanzilishi wa vyama hivyo!!!
Hakuna tume huru ndani ya vyma vysiasa hivyo ni bora kabla ya mchakato wa katiba mpya kila chama cha siasa wadau wake wafanye mchakato wa kubadili katiba zao ili kuepuka machafuko 2015 ambapo watu wengi wamekuwa wadadisi na wanahoji mambo ya msingi!!!
CHADEMA imekuwa ya kwanza kwa uvumilivu wa kisiasa na kufuatia na CCM lakini CUF na NCCR pamoja na kuwa na wasomi wa Uchumi na siasa wamekuwa wanaongozwa kwa Udikiteta!!!
Watu Wengi waliohama CUF (Lwakatare Safari), NCCR (Mabere Marando, Joseph Selasini) wamekuwa na Mchano mkubwa katika jamii ya demokrasia .
Angalia John Shibuda kutoka CCM alitaka kuvuruga CDM kwa hoja ya Posho lakini Hekima na uvumilivu wa kisiasa umeokoa na sasa hoja ya posho hata CCM wanamuona Shibuda ni mwehu!!!
Sasa ingekuwa CDM wamukurupuka kumufukuza Shibuda kama Seif alivyo kurupuka kumufukuza HR, kama Mbatia alivyokurupuka kumufukuza Kafulila ingekuwa aibu tupu!!!!!!!