Safari ya kumsaka mrithi wa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Fredrick Shoo, inatarajia kuanza wakati wowote kuanzia sasa wakati kikao cha Halmashauri Kuu ya Kanisa hilo kikitarajiwa kukaa ili kupokea majina matatu ya maaskofu waliopendekezwa kugombea wadhifa huo wa juu.