Tetesi: Mchakato wa kumtangaza Mwalimu J.K Nyeree kuwa Mtakatifu

Haujasoma uzi wote,ndiyomaana umeuliza hilo swali.
Inawezekana ameusoma uzi wote lakini kwa sababu ni mrefu hakumbiki yote yaliyoandikwa. Kwa ufupi, hii hotuba imerudiwa mwaka huu lakini ni hotuba ya mwaka 2019 ambapo ilikuwa ni miaka 20 tangu Mwalimu atutoke mwaka 1999. Ila ujumbe wenyewe bado una maana hata sasa wakati mchakato bado haujafikia hatma. Binafsi nilipata nafasi kuzungumza na Baba wa Taifa mara mbili kwa mazungumzo ya kawaida siyo kwamba niliitwa nimekosea au kupewa cheo cho chote. Baba wa Taifa alikuwa mtu wa ajabu, hakuwa na dharau labda ujidharaulishe mwenyewe kwa kujidai unajua. Alikuwa anasisimua akizungumza kwa ufasaha na kuelezea dhana mbalimbali kutokana na ufahamu mkubwa wa mambo mengi aliokuwa nao kwa ajili ya kujisomea na kufuatilia taarifa na habari za dunia; lakini pia alikuwa anakusikiliza unachosema na kukuonesha kuwa anakuelewa na pia anakuuliza maswali ya dhati kabisa bila kebehi. Alikuwa mtafutaji na mchambuzi wa mambo.Ukimwambia kitu kipya ambacho hajawahi fikiria utaona macho yake yanang'aa anakuja kukuuliza ulipata wapi jambo hilo; ukisema kitabuni atataka umletee kitabu na atakisoma! Alikuwa hakurupuki; alitumia muda kujiandaa namna ya kuwasilisha hoja yake, iwe kwa mtu binafsi, kwa taifa au kwenye hadhara za kimataifa. Utapenda kupata nakala ya hotuba yake; hotuba yo yote ile ilikuwa ni makini. I greatly miss Baba wa Taifa. RIP Mwalimu.
 
Huu uzi usi comment bila kuwa umeusoma kwa kina. Sasa hapa tutajua waliusoma na wazee wa kukurupuka.
Ninakuhakikishia hutowapata watano watakaochangia wakiwa wameusoma na kuulewa. Hii ni JF mkuu'MTAZAMO'.

Andiko refu namna hii, halafu lenye maudhui ya namna hii, tena lililoandikwa kwa namna isiyo rahisi kueleweka na watu wanaopoteza 'attention' haraka, usitegemee kuona hayo unayosema yatokee.
 
Hii akili imetoka wapi leo; kama siyo moja ya muujiza inayosemwa kwenye andiko lenyewe kwamba kuna miujiza itakayoshuhudiwa wakati mchakato ukiendelea.
Naamini kwa Mwalimu Nyerere, miujiza mingi tu itajitokeza, hasa kuhusu taifa hili alilolipenda sana.
 
JULIUS KAMBARAGE NYERERE. BABA WA TAIFA LA TANGANYIKAA NA HATIMAE TANZANIA. BABA WA UTHUBUTU WA MAENDELEO YA NCHI YETU. MUASISI WA SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA. MPINGA UBAGUZI WA RANGI. MPIGANIA UKOMBOZI WA NCHI MBALIMBALI DUNIANI. MSULUHISHI WA MIGOGORO BARANI AFRIKA. MSOMI ALIECHUKIA UNYONYAJI NA UBADHIRIFU WA MALI ZA UMMA. RAIS ALIEKUFA MASIKINI. MPENDA DINI NA MHESHIMU DINI ZA WENGINE.

MY TAKE: JULIUS K. NYERERE ANASTAHILI KUWA MTAKATIFU. MCHAKATO UHARAKISHWE
 
Tanzania hatuja na mtakatifu hata mmoja tangia dunia iumbwe? Kwa nini? Tunawaombea mfanikiwe kwenye huu mchakato.

Dunia Hii haijawahi kuwa na mtakatifu hata mmoja.

Kama tukio hili likitokea litaimarisha Imani na msimamo wangu kuhusu wale walioitwa watakatifu kwenye vitabu kama Biblia na vitabu vingine vinavyoheshimiwa kuwa Dunia inauongo mwingi
 


Wala sijausoma, sio relevant, This is why wakati mwingine na ushangaa ukatoliki, Utakatifu unakuwa determined na matendo ya mtu, sio umaarufu through a process ya Vikao.
 
Kama amekidhi vigezo hakuna shida.
Kigezo cha utakatifu ni kumuamini Yesu kua Ndie Bwana maana ukimkiri yeye unakua na uzima wa milele hivyo Nyerere alikua mwamini moja kwa moja ameingia katika ufalme wa MUNGU haihusiani na matendo yake bali ile neema Ya Mungu kwa kila atakaye mwamini mwana wa Pendo lake!
 
Tanzania hatuja na mtakatifu hata mmoja tangia dunia iumbwe? Kwa nini? Tunawaombea mfanikiwe kwenye huu mchakato.
Wewe jamaa unasoma bible gani?
tanzania kuna mamilion ya watakatifu elewa utakatifu unaupata kwa Kumuamini Yesu Kristo kua ni BWANA na ukimkiri kwa kinywa unapata wokovu maana Mungu anakupa haki ya kufanyika Mwana mrithi wa Ufalme Pamoja na mwana wa Pendo lake soma bible acha kusomewa!
 
Dunia Hii haijawahi kuwa na mtakatifu hata mmoja.

Kama tukio hili likitokea litaimarisha Imani na msimamo wangu kuhusu wale walioitwa watakatifu kwenye vitabu kama Biblia na vitabu vingine vinavyoheshimiwa kuwa Dunia inauongo mwingi
Watakatifu wapo kuna kisa kwenye biblia kuna maiti waliitupa Kwenye kaburi la nabii elisha yule maiti alipoigusa tu mifune ya elisha alifufuka pale pale imagine huo utakatifu .utakatifu ni kuwa safi bila dhambi watu hao wapo japo wachache.
 
Mt 23:9-12 SUV

Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni. Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo. Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu. Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa.
 
Watakatifu wapo kuna kisa kwenye biblia kuna maiti waliitupa Kwenye kaburi la nabii elisha yule maiti alipoigusa tu mifune ya elisha alifufuka pale pale imagine huo utakatifu .utakatifu ni kuwa safi bila dhambi watu hao wapo japo wachache.

Hakuna Mwanadamu asiye na dhambi hata mmoja. Kumaanisha hakuna mtakatifu hata mmoja.

Kufufua Wafu na utakatifu ni vitu viwili tofauti.
 
Namaanisha bila juhudi za mwenye heri,katoliki Leo isingekua na idadi hiyo ya waumini,zaidi ya nusu wangekua waislam na hivyo TEC kukosa jeuri ya kutoa matamko
 
Kipi ?!!

Kwa ajili gani ?!!

Unajionaje kuingilia hukumu ya MAHAKAMA yake isiyo na wakili ?!!![emoji15][emoji15][emoji15]

Hicho ni kiburi....repent[emoji120]
Tunajuwa alikuwa mchonganishi ,ameuwa watu namwenye mamlaka hayo ni mungu pekee lakini ukiingilia kazi yake mungu yeye anakuruhusu ilasiku yakikuta nikisago ,tambua ndugu yangu huyubwana alikuwa nayake mengi tu
 
Kipi ?!!

Kwa ajili gani ?!!

Unajionaje kuingilia hukumu ya MAHAKAMA yake isiyo na wakili ?!!![emoji15][emoji15][emoji15]

Hicho ni kiburi....repent[emoji120]
Lakini kumtangaza kuwa mwenyeheri sio kuingilia kazi yake mungu binaadam anaweza kuona yaliosirini?swali ulilonipa Mimi ulipaswa kuwauliza waandaji washughuli usika kama mungu kawaambia hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…