Mchakato wa mabadiliko Simba umekwama

Mchakato wa mabadiliko Simba umekwama

rodrick alexander

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Posts
16,784
Reaction score
23,312
Huko Simba mambo bado, juu ya ile ishu ya mabadiliko ya klabu hiyo ili iendeshwe kwa mfumo wa hisa ambao mchakato wake ulianza tangu mwaka 2017 umekwama ikielezwa tatizo likiwa ni katiba ya klabu hiyo, kiasi cha Ofisi ya Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kurudisha mpira Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Simba inapambana kutaka klabu hiyo iendeshwe kisasa kwa hisa na tayari imekuwa ikimtangaza Rais wa Heshima wa klabu hiyo, Mohammed ‘Mo’ Dewji kuwa ni mwekezaji wake akidaiwa kumiliki asilimia 49 ya hisa, huku 51 zilizobakia zikiwa ni za klabu.

Mchakato unaelezwa ulishapata ruksa kwa Tume ya Ushindani nchini (FCC) kisha Ofisi ya Wakala na Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na sasa ilitua RITA ambako maofisa wake walijifungia kufanya uchambuzi wa kina na kubaini kuna tatizo katika katiba ya klabu hiyo.

Rita wala hawakutaka mambo mengi inaelezwa baada ya kuangalia katiba ikionyesha mwekezaji mwenye asilimia 49 ana mamlaka makubwa kuliko wenye asilimia 51 ikashtuka na kuamua kurudisha jambo hilo ofisi za BMT wakitoa maelekezo kwa Simba ifanye kitu mambo yawe sawa.

Karibu mwaka wa tano tangu mchakato huo uanze, lakini ukiwa umeshindwa kukamilika baada ya kupita sehemu mbalimbali, hali iliyoibua sintofahamu huku mwekezaji huyo mara kadhaa akilalamika katika mitandao ya kijamii akidai kuonewa kutokana na jambo hilo kutofikia tamati.

Hata hivyo, juzi mmoja wa vigogo wa Simba aliliambia Mwanaspoti mchakato huo umekwama RITA ambao ndio wenye mamlaka ya kupitisha Bodi ya Wadhamini ya klabu hiyo kwa mujibu wa katiba ya Simba.

Alisema RITA imebaini kuwepo na upungufu kwenye katiba hiyo baada ya kupitia suala hilo na kulazimika kuirejesha katiba hiyo BMT ambao ndio waliwasilisha RITA jambo hilo.

“Tumetakiwa kumaliza sintofahamu iliyopo kwenye katiba yetu, hivyo RITA imeirudisha BMT na tayari baraza nalo limeirudisha Simba,” alisema kigogo huyo aliyeomba hifadhi ya jina.

Japo mabosi wa RITA walikataa kuzungumzia suala hilo walipoulizwa, lakini Katibu Mkuu wa BMT, Neema Msitha alikiri kuipokea katiba hiyo kutoka RITA.

“Ni kweli imerudishwa kwetu, na kilichobaki ni sisi kuwasiliana na Simba kuwajulisha hilo, sikuwepo ofisini, kwa ajili kujadili hilo ndio nimerudi, lakini suala lao limerudishwa kwetu, nilipokuwa nje ya ofisi nililiacha kwa msajili (Evodius Kyando),” alisema Neema na kuongeza;

“Kuna some issue (baadhi ya mambo) katika katiba yao ndio inapaswa kurekebishwa, hivyo wasiliana na msajili atakuwa na majibu mazuri kuhusu jambo hilo.”

Kwa upande wa msajili huyo alipoulizwa alisema; “Kimsingi kuna mambo mengi pale Simba, hili suala lilifika kwetu na tukawarudia kuwaelekeza wanachotakiwa kuboresha. Mwanasheria wa Simba, ndiye anayepaswa kulizungumzia zaidi hilo, kwa vile maelekezo yote tumeshapeana na tunasubiri feedback (mrejesho) kama tulivyokubaliana.”

Mwanasheria wa klabu, Hosea Chamba alipotafutwa alisema jambo hilo ni pana na hakuwa kwenye mazingira ya mazuri ya kulizungumzia.

“Niko bize kidogo na suala hili ni pana, nipe muda wa saa mbili (kuanzia saa 4:13 asubuhi juzi) kisha nipigie,” alisema Hosea na kukata simu.

Hata hivyo, baada ya muda huo alipigiwa simu hakupokea, hata jana asubuhi alitafutwa tena, simu yake iliita bila kupokelewa, ila kiongozi wa Simba aliyeomba hifadhi ya jina alisema kinachotakiwa kwa sasa kuboreshwa kwa baadhi ya vipengele vingi ndani ya katiba ya klabu hiyo ambavyo haviko sawa.

“Wanadai kuna vitu vingi havipo sawa, mfano mwekezaji ana hisa 49 halafu ndiye mwenye mamlaka makubwa kuliko mwenye hisa 51, wanasema sio sawa, lazima klabu itendewe haki na kulindwa,” alisema.

Awali Simba ilitaka kumpa mwekezaji asilimia 51 na klabu kubaki na 49, kabla ya serikali iliingilia kati na Mo inadaiwa alishatoa Sh20 bilioni.

MwanaSpoti
 
Hapo waliozingua ni hao RITA. Kama wamepitia katiba na inaonyesha kuwa mwenye asilimia 49 ana nguvu kuliko mwenye asilimia 51, sidhani kama hilo linawahusu sana maana mpaka suala limefika kwao ina maana pande zote wameridhia katiba ilivyo.

Sasa wao wanakuja na habari za kutetea maslahi ya upande fulani kisa wanaona kama wamedhulumiwa.
 
Ni taratibu za kiuendeshaji ndio zipo ivyo mkuu. Mwenye 51% anatakiwa kuwa na nguvu zaidi ya mwenye 49%. Unachosema ni sawa na wewe unataka kumtapeli mtu baada ya kushtukiwa ukajitetea kwa kusema yeye mwenyewe amekubali nimtapeli
 
Sasa RITA wameamua kuwa wanasheria wa upande mmoja badala ya kusimama kati? Kama shauri limefika hadi RITA bila upande wa 51% kugundua umedhulumiwa basi labda huo upande wa 51% una mamluki waliopandikizwa wenye nia ya kuufaidisha upande wa 49%

Halafu hawajasema hizo nguvu ni zipi, ni kura au masuala mengine? Ingependeza wangeweka wazi maana wasijekuwa wanafanya mambo kwa kukariri tu wakati vitu vingine vinaweza kubadilika kulingana na makubaliano ya pande mbili. Inawezekana hao 51% walikubali kuachia baadhi ya mambo yaende upande wa pili ili mchakato uendelee/umalizike.
 
Hawa 51% hawana msaada na hawaisadii Simba na hawajulikani ni kina nani
Hawa wanachangishwaga tu hela za vibegi na michango ya mtandaoni, faida kubwa ni kwenda uwanjani kwa buku 3 na kushangilia kwa nguvu

#nguvumoja
 
Sasa RITA wameamua kuwa wanasheria wa upande mmoja badala ya kusimama kati? Kama shauri limefika hadi RITA bila upande wa 51% kugundua umedhulumiwa basi labda huo upande wa 51% una mamluki waliopandikizwa wenye nia ya kuufaidisha upande wa 49%

Halafu hawajasema hizo nguvu ni zipi, ni kura au masuala mengine? Ingependeza wangeweka wazi maana wasijekuwa wanafanya mambo kwa kukariri tu wakati vitu vingine vinaweza kubadilika kulingana na makubaliano ya pande mbili. Inawezekana hao 51% walikubali kuachia baadhi ya mambo yaende upande wa pili ili mchakato uendelee/umalizike.
Mkuu upande wa 51% chini ya chairman mangungu ,hawana shida

Shida ni kwamba kuna watu nje ya chairman mangungu ndio waliona hayo mapungufu

Na kama unakumbuka wakati wa kampeni ?kuna mgombea alisema kuwa akishinda atabadili vifungu ktk katiba ..ndio vifungu hivyo vinavyo mpa 49% nguvu na kumnyima 51%

Kama chairman mangungu anajua kuwa 51% haina nguvu ,dhidi ya 49% na yuko kimya basi kuna tatizo
 
Na kama unakumbuka wakati wa kampeni kuna mgombea alisema kuwa akishinda atabadili vifungu ktk katiba ..ndio vifungu hivyo vinavyo mpa 49% nguvu na kumnyima 51%
Sasa huyo mgombea ina maana aliona kuna tatizo ambalo Mangungu hajaliona wala kulisemea, sasa mbona unasema Mangungu ambaye ndiyo mwakilishi mkuu wa 51% hana shida?
 
Sasa huyo mgombea ina maana aliona kuna tatizo ambalo Mangungu hajaliona wala kulisemea, sasa mbona unasema Mangungu ambaye ndiyo mwakilishi mkuu wa 51% hana shida?
Mangungu ni mtu wa tajiri ndio maana halioni hilo jambo, na ndio maana uchaguzi ,tajiri alitumia nguvu nyingi mangungu ashinde, na baada ya uchaguzi,tajiri akaibuka na kusema anahojumiwa na watu walio ndani ya simba
 
Sijaelewa
FCC( Fair competition commitee) wameona sawa,
RITA ( msajili wa vizazi na Vifo ) anaona sio sawa? Kazi yake si ilitakiwa kudili na hizo hati?
Anaelewa vizuri wakuu anijuze.
 
Mangungu ni mtu wa tajiri ndio maana halioni hilo jambo, na ndio maana uchaguzi ,tajiri alitumia nguvu nyingi mangungu ashinde, na baada ya uchaguzi,tajiri akaibuka na kusema anahojumiwa na watu walio ndani ya simba
Basi kama unatambua hilo, usimtetee Mangungu maana yeye ndiye anashikilia dhamana ya wanachama sasa kama amewekwa mfukoni na upande wa pili, shida iko hapo.
 
Basi kama unatambua hilo, usimtetee Mangungu maana yeye ndiye anashikilia dhamana ya wanachama sasa kama amewekwa mfukoni na upande wa pili, shida iko hapo.
Mie simtetei mangungu, mie ni wale tunataka 51% iwe na nguvu ,na kwenye kampeni nilikuwepo
 
Back
Top Bottom