Mchambuzi mmoja akilaumu mashabiki na kutaka wasipige kelele!

Mchambuzi mmoja akilaumu mashabiki na kutaka wasipige kelele!

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Nimeshangazwa sana na mtu ameaminiwa kuwa mtangazaji na mchambuzi wa mpira lakini hatumii vizuri akili yake kufanya kazi yake.

Amelaumu mashabiki wa Simba kuwa hawana msaada kwa timu.
Hawanunui kadi za uanachama wala hawalipii ada ya uanachama.

Hawananui jezi,na wala hawana mchango wowote wa maana kwa timu.
Mimi naomba nimuulize,ni wapi kadi za uanachama wa Simba zinatolewa?
Je wauza jezi walipata hasara kiasi gani kwa kuagiza jezi na hazikununuliwa?

Je anajua jezi nyingi zinazouzwa mikoani ni feki au yeye ndiye chawa wa wauza jezi feki?
Unadhani kila mtu mkoani anavaa vitu feki au hawajui vitu quality?
Kwa taarifa yako,kuna mashabiki wengi tu wa yanga kutoka huku mikoani wananunua jezi hadi elfu themanini jezi moja.
Hawa wa Simba wanasikitika tu kuona aina za jezi zinazouzwa hazina quality.
Huwezi kununua tu jezi unavaa unaonekana muuza mkaa.

Mashabiki wanalipia app za timu zao,wanasafiri kutoka mikoani kwenda Dar kusapoti timu kwenye mechi za kimataifa.
Mashabiki wanaingia kwenye mechi kusapoti timu.
Mashabiki wananunua bidhaa za mwekezaji wakiamini ni mchango wao kwa timu.
Mashabiki ni nguzo muhimu ya kuvutia waekezaji.
Kwa sasa Hier wa yanga bidhaa zao zina soko na kupendwa kwa kuwa tu zimetangazwa kupitia platform za timu inayofuatiliwa na hao mashabiki unaowaona hawana maana.

Kama umetumwa na mwekezaji,mwambie aiache timu aone kama timu itakufa
 
Akusome akibisha basi atakuwa na sababu nyingine
Mashabiki wanajaa kwenye viwanja vyenye jua Kali sana vyoo vibovu usafiri wa shida huduma za kwanza hovyo migahawa hakuna
Kimsingi mashabiki wasilaumiwe hata kidogo
 
SIMBA SC ipo mahututi, haipo kwenye status ya timu ya kuitegemea kwasasa.

Sio Wachezaji Uwanjani, Kamati ya Usajili wala Menejimenti kwa ujumla

Narudia Mo Dewji afanye kitu au atuachie timu yetu
 
Hao wachambuzi ni machawa Simba Ina sapoti kubwa ya mashabiki Ila mwekezaji na viongozi wako kwa ajili ya maslahi yao, mwekezaji anafikiri akiwapa uanachama wabunge ndio Simba itanufaika wakati Kuna mashabiki wengi wanataka Kadi za uanachama wao wanawapa Kadi za mashabiki ambazo hazina faida yoyote.
Walileta mchango wa uwanja pesa wakala wanadanganya wamejenga uzio.
Wameuza Basi la timu kinyemela halafu MCHAMBUZI WA mchongo keshavimbiwa maharage anabwabwaja hovyo.
 
Back
Top Bottom