Mchambuzi: Simba bado wanacheza mpira wa ovyo

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
19,637
Reaction score
29,473
Simba bado wanacheza mpira wa hovyo

"Achana na idadi ya magoli yaliyofungwa na Simba leo, kwa aina ya timu iliyokutana nayo na aina ya mchezo ulivyokuwa ilikuwa ni nafasi ya kutupa mechi safi tofauti na hii tuliyoiona.Simba hii hata ukiangalia bar unasinzia"[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

SHAFFIH DAUDA ,DIGALA.

NB: Nafasi bado Iko wazi Kwa Makolo kwenda kupiga tuition pale jangwani
 
Ufaza mwingi, pale hakuna kocha.
Timu inashinda ila mashabiki hatuna furaha
Kocha unamuonea tu mkuu. Timu inaonekana morali ipo chini sana.
Either pressure imekuwa juu sana ama wachezaji wanataka kufanya vitu vingi ambavyo havipo katika maelekezo ya mwalimu.

Shida zaidi ya Simba inakuja wakiwa hawana mpira. Wachezaji wanatembea na huoni uthubutu wao katika kutafuta mpira.
 
Ukikutana na timu yenye mpira mbovu usitegemee game itakuwa nzuri. Simba ikikutana na timu nzuri ya level yake ndio utaona huo mpira mzuri mnaoutaka.

Mchambuzi akae kwa kutulia
 
Hapo ndo kazi ya mwalimu inapoonekana.
Kama mchezaji hajitumi mtie benchi weka wengine wacheze.

Kuna wachezaji pale Simba hata wakicheza pumba kila siku hawana pressure maana wana namba za kudumu (Mfano Zimbwe, Kapombe, Saido, Mzamiru et al).


Kocha hafanyi rotation ya wachezaji, kila mechi watu walewale na ameshindwa kabisa 100% kupandisha morali ya timu.


Mwanzo ALITUDANGANYA eti anapenda mchezo wa kasi na kusema akina Chama wanamchelewesha, lakini hivi ukiangalia toka aje yeye na kabla yake, kipi kimeongezeka kiuchezaji tofauti na kushuka?.

Timu inapata matokeo ya kimchezo yatokanayo na uwezo binafsi ila sio mbinu za kocha.

Hata ukiangalia timu inavyojipanga wakati wa kushambulia au kukaba ni kituko. Kuna gap kubwa sana na mashimo mengi uwanjani yanayoachwa wazi.

Simba tumezoea ball linatembea dakika 90 kwa kasi na matokeo yanapatikana. Hata likifungwa goli moja wakati ball limetembea washabiki tulikuwa tunafurahi tofauti na sasa ambapo hata tukishinda 5 bila nadhani bado hatutakuwa na furaha.
 
Kabisa mkuu,....sijui tatizo nini
Yaani sijui ni kocha. Mfano ile mechi ya Ngao ya Hisani, aina ile ya mpinzani wa Simba ilitakiwa afungwe 3-0 ndani ya dakika 90, lakini akaitesa Simba hadi ikaponea kwenye matuta. Simba ni timu kubwa, haitakiwi kufikishwa kwenye matuta
 
Mashabiki wa Simba ni kero sana. Mimi naona mpewe timu muiendeshe kwa kila kitu. Hamna shukrani kabisa. Kazi tu kuwavunja moyo wachezaji, kocha, viongozi na wawekezaji. Kifupi hamfai kuwa Mashabiki katika ulimwengu uliostaarabika.
 
Nadhani kinachowatesa mashabiki wengi wa Simba ni neno "LUNYASI".
Chanzo cha hili neno hakionekani Kwa Sasa na mashabiki walishakizoea. Vinginevyo timu imepata matokeo chanya inatosha.
 
Mashabiki wa Simba ni kero sana. Mimi naona mpewe timu muiendeshe kwa kila kitu. Hamna shukrani kabisa. Kazi tu kuwavunja moyo wachezaji, kocha, viongozi na wawekezaji. Kifupi hamfai kuwa Mashabiki katika ulimwengu uliostaarabika.
Je tusiseme ukweli kwakua wachezaji watavunjika moyo?
 
Hii ni mdol
Huo ni mdoli wa kolo🦁.Na sio Thimbaaa😂😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…