Mchambuzi: Wapinzani Tanzania wajivue gamba siasa wanazofanya haziakisi utashi wao kutatua matatizo yaliyopo

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Akizungumza jioni hii kupitia kipindi cha BBC kinachotathimini mwekekeo wa mambo katika mwaka tuanaouanza, mchambuzi huyo amesema kwa upande wa Tanzania wapinzani wanatakiwa wajifungie na kujivua gamba.

Amesema vyama vya upinzani vinapaswa kujitazama upya namna vinavyofanya siasa na hali ya demokrasia ndani ya vyama vyao kwani vingi vina mwekekeo wa kidikteta ingawa vinaimba kupigania demokrasi.

Amesema ilani za vyama hivyo hazina maelezo ya wazi namna gani wakipewa nchi wataitoa kwenye matatizo yaliyopo. Zaidi sana wanajenga hoja za kushambulia watu na kutukana matusi. Amesema Kwa maoni yake hizo siasa zimepitwa na wakati.

My take

Badala ya kutukanana matusi nadhani Kuna la kujifunza toka kwenye huo uchambuzi.
Mambo mazuri sio lazima yakufurahishe.
 
Hizi habari zinazoletwa bila kichwa wala miguu zinafanya mjadala kuwa wa upande mmoja tu,wa vilaza.

Hakuna jina la huyo mchambuzi, hakuna audio/video ya huyo mchambuzi wala hata picha.

Tujitathmini wana JF.
 
Mbona post nzima ni your take hii?!
 
Hizi habari zinazoletwa bila kichwa wala miguu zinafanya mjadala kuwa wa upande mmoja tu,wa vilaza.

Hakuna jina la huyo mchambuzi, hakuna audio/video ya huyo mchambuzi wala hata picha.

Tujitathmini wana JF.
Nilisikiliza haraka sikubahatika kunukuu jina la mchambuzi lakini niliona alichokichambua ni muhimu Kwa maslahi mapana ya upinzani
 
Back
Top Bottom