KADRI sayansi na technolojia inavyozidi katika nchi zinazoendelea wataalamu wamekuwa wakitambua baadhi ya magonjwa ambayo miaka michache iliyopita yalikuwa hatambuliki kirahisi au wakati mwingine yakachanganywa na magonjwa mengine kwa sababu ya ukosefu wa vipimo sahihi. Leo tunaona tatitizo la mawe katika figo likijitokeza zaidi na wahusika wanashangaa kwa nini tatizo hili liongezeke zaidi?
Jibu la kwanza ni kwa sababu zamani hakukuwa na vipimo vya tatizo hilo kama CT-SCANER, Lakini pia kubadilika kwa maisha kunachangia kuongezeka kwa tatizo hili. Mawe katika figo au kidney stones ni aina ya madini yanayotengenezwa katika figo au katika njia ya mkojo.
Mawe haya hutengenezwa zaidi na madini ya calcium na oxalate au phosphate. Mawe haya yanaweza kutengenezwa kwenye figo au katika kibofu cha mkojo. Ukibwa wa mawe haya unatofautiana kuanzia mawe madogo kama 4mm mpaka 10mm. Ukubwa wa mawe huchangia sana aina ya matibabu anayopewa mgonjwa.
Chanzo
Chanzo kikuu cha mawe hayo ni kutopata mkojo wa kutosha amabayo inaweza kuchangiwa na kutokunywa maji ya kutosha au kuongezeka kwa madini yanayotengeneza mawe haya mwilini. Hi husababisha calcium nyingi katika mkojo ambayo huanza kutengeneza mawe.
Kuna baadhi ya magonjwa na yanayohusishwa na kuwa na mawe na kuna aina za dawa sinazohusishwa na ongezeko la mawe katika figo.
Magonjwa hayo ni pamoja na gout ambao huongeza tindikali (acid) katika damu na mkojo hiyo kutengeneza mawe yaitwayo uric acid stones.
Tatizo za ufyonzaji mkubwa wa calicium katika chakula ni tatizo la kurithi nalo husababisha kukithiri kwa kiwango cha calicium kwenye damu ambayo hutolewa mwilini kwa njia ya mkojo na hivyo kuteneza mawe kwenye njia ya mkojo. Magonjwa mengine yanayohusishwa na mawe ni kama kisukari, shinikizo la damu nk.
Kuna dawa zinazoweza kusababisha kuongezeka kwa mawe ni zile zitumikazo kutibu magonjwa ya tumbo ya kupunguza tindikali tumboni tumboni, dawa za kuongeza mkojo na dawa za Ukimwi na hasa dawa iitwayo indinavir.
Tabia ya ulaji wa vyakula vifuatatavyo kupita kiasi unaweza kukuweka katika hatari ya kupata mawe katika figo na kibofu cha mkojo. Navyo ni vyakula vya protini itokanayo na wanyama, chakula chenye chumvi nyingi, kutumia vyakula vyenye sukari kupita kiasi, vyakula vyenye vitamini D kupita kiasi na vyakula vyenye oxalate nyingi kama spinach. Kutokuwa na tabia ya kunywa maji inakuweka kwenye hatari zaidi.
Dalili zake
Dalili za mawe katika figo hutofautiana kutokana na mtu na mtu lakini zaini ni maumivu na vichomi ya tumbo upande wa chini (flank pains) na damu kwenye mkojo. Maumivu ya tumbo yanaweza kuwa makali kutokana na ukumbwa wa mawe.
Matibabu ya mawe katika figo na njia ya mkojo yanategemea ukubwa wa mawe pia. Mawe mmadogo ya ukubwa wa 4mm yanaweza kutoka yenyewe ndani ya masaa 48 kwa njia ya mkojo na mgonjwa atashauriwa kunywa maji kwa wingi.
Matibabu
Dawa za maumivu hutolewa kwa wenye maumivu makali na maumivu madogo. Pia kuna dawa zinazoweza kuyeyusha mawe lakini wakati mwingine hushindwa kufanaya kazi, hivyo njia nyingine za matibabu hutolewa.
Njia hizi ni kama kuwekewa kifaa maalumu chenye mtetemo ambacho hupasua mawe na kuwa kwenye vipande vidogo ambavyo hutoka kirahisi kwa njia ya mkojo baada ya kunywa maji mengi. Njia ya upasuaji mdogo inayoitwa lithotripsy inatumika mawe yanaposhindwa kupita kwenye mirija ya mkojo.
Kinga
Ili kujikinga usipate mawe katika figo na njia ya mkojo ni muhimu kunywa maji mara kwa mara, kuangalia vyakula tunavyokula kuepuka wingi wa calcium na oxalate. Ukitumia dawa nilizotaja hapo juu unywe maji mengi ili kuondoa madini kabla hayajatengeneza mawe.