Ndugu zangu wana jf naombeni ushauri. Kwa ufupi nataka kufanya biashara ya kusambaza mchanga na kokoto, ila kabla ya kuanza ningependa kujua yafuatayo
. Biashara hii ipoje?
. Sehemu ya kupata malighafi
. Masoko yake yapoje?
. Mtaji kiwango cha chini cha kuanzia
Tafadhali sana naomba ushauri wenu...!!
Mkuu hii ni biashara ya wenye ubavu wa fweza na vifaa pamoja na logistical management.
Kwa kuanzia uwe na ingalau malori mawili au matatu ya tani 25.
Tani mpja ya kokoto kule Lugoba ni Tshs 35,000
Kwa kawaida tani hiyo inasafirishwa kwa Tshs 20,000 mpaka Dar.
Hivyo basi gari moja kufikisa Dar ni Tshs 1,375,000 kabla ya kodi na ushuru.
Gari moja yaweza fanya tripu moja kwa siku
Hivyo basi ukiwa na gari mbili unsongea turnover ya Tshs 2, 750,000 kwa siku moja,
Mahesabu haya hujaweka, trafiki njiani, wizi wa dereva(mafuta na kokoto),posho ya dereva, wear and tear ya gari, na overwight ya mizani( fine mbaya sana hapa)
Ukiyaweza hspo ingia ngoma ucheze.