Mchanganuo wa biashara ya kuingiza faida ya 150,000/= kwa siku/ 4,400,000 kwa mwezi

Gharama zote zimeweka Huko mkali. Kwa siku Gharama za mafuta pikipiki tatu tumekafilia kila pikipik tuweke mafuta ya sh.7000. inakua 21,000 jumla, Chakula inakua 5,000
 
Wazo lako ni zuri alafu pia ni realistic...
 
Mtu kama hujawai kufanya biashara ni lazima uwe na picha ya faida kubwa kubwa kichwani, ila ukiingia kwenye biashara ndio utajua hayo mawazo yalikua potofu, bahati mbaya wengi wanaamini ukishamiliki biashara basi kila siku ni faida, Ukitaka kupanda ngazi sharti uanze kukanyaga ngazi za chini, vinginevyo utapasuka msamba.
 
Mkuu biashara za kwenye maandishi huwa ni rahisi sana, na tamu munooo!!ingia kwenye field ndio utakuta mambo ni tofauti sana hasa kwa biashara zetu hizi za kiswahili!!mfano unadhania kijana mmoja kuuza trey 45 za mayai kwa siku ni kazi rahisi hivyo?!!
Mfano dar, hiyo fremu iliyopo karibu na soko wapi utaipata kwa 80, 000?
Hizo pikipiki zenyewe ni biashara pasua kichwa sana tu.
 
Yaah million 4.4 faida Ni kubwa Sana kwenye hiyo biashara watu wengi wangezama Sana huko.

Ila kwangu ninavyoona Kwanza haina haja kuchukua pikipiki tatu zote hizo moja tu inatosha ambayo utaitengenezea kisehemu pale nyuma Cha kuchukulia trey hata 30 au 20 za kusambaza kwa wateja ukimaliza unarudi ofisin kuchukua tena mzigo mpya.
Na all in all ni biashara nzuri Kama ukipata wateja wengi Hawa wengine wasikukatishe tamaa mkuu.

Na ili kuepukana na mayai yaliyoharibika itabidi upate supplier mwaminifu au uwe na kifaa Cha kupimia hayo mayai ili uwe mwaminifu kwa wateja wako.
Maana supplier wako anaweza siku moja kukuchenjia akakuwekea mayai viza yote na ukapata hasara.

Na kingine Kumbuka hutaweza kuuza mayai trey 45 kila siku Kumbuka Kuna kupanda na kushuka labda Leo trey 20 siku inayofuata trey 15 na Tena trey 30 au 40 kwa kila kijana au hata trey 50 kwa hiyo angalia Hilo kwanza na jiwekee kiwango Cha chini mauzo yasishuke trey 20 au 15 kwa kila kijana Ila Kama yakipanda itakuwa sawa.
Na ukitaka kuongeza faida utaanzisha hapohapo biashara ya mayai ya kuchemsha ambapo utakuwa na Vijana wa kukusambazia mayai na mengine kuuzwa hapo hapo dukani.
 
Hawa wateja utakaowahudumia haraka haraka hivyo wanatoka wapi ghafla hivyo? Unafikiri wakati ambao wewe ulikua hujaingia kwenye hio huduma wao walikua hawapati hio huduma? Kama walikua wanaipata basi hapo ndio kuna kazi, ni uchukue miezi kadhaa ndio wateja waanze kuielewa huduma yako, sababu wao pia walikua na mahali wanaipata hio huduma na hawawezi tu kuhama ghafla na kununua bidhaa yako wakati haujaongeza dhamani yoyote kwayo.
 
Shukran mkuu umekua optimistic. Alaf hii ni kitu realistic kabisa bas tu kuna watu wana criticize tu hawaelewi. ila hii ni faida ya ufugaji wa kuku kibiashara. Hapa hutakua na limit ya mzunguko wa biashara, the effort the more mzunguko.

Embu fikiria watu wangapi wanakula chips mayai kila siku, Kuna.vijiwe vingapi vya chips, Kuna watu wanauza gunia moja mpaka mbili za chips kwa siku, ulishawah kufukiria wanatumia trei ngapi za mayai. Wenye maduka ya kawaida, Wenye bekari, mahoteli wanatumia mayai kama breakfast na kwenye mabenki pia, wapika vitumbua, wapika keki. its just a matter of marketing na kujibrand. [emoji2]
 
Pessimist opinion. CONTROLA
 
Kumbuka hapa vijana wanatumia pikipiki, hawatembei kwa mguu au baskeli. so wanaweza kukava eneo kubwa saana. Trust me kama Mtu umempa mafunzo ya jinsi ya kumfuata mteja its very possible. Kila mmoja unampangia maeneo yake yakusupply mzigo
 
Uvunaji sumu za nyoka Ni faida mls moja Ni dola 1.4 kwa nyoka anayelishwa sawa huvunwa ml8-10kwa wiki wakiwa 100 = na mls 1000 sawa na laki322000 kwa wiki sawa na M15 kwa mwaka kwa nyoka 100 tuh je wakuwa 10,000 alisikika mwana CHADEMA mmoja
Soko lake lipo wapiii na Aina ganiii za nyoka wanaotakiwaaa,je unavunaje hao nyoka
 
Inawezekana kwa kweli...kuna jamaa hapa Kinyerezi ana frame analetewa mayai 300 trays na 9 Hills Company na ndani ya siku 2-3 mzigo mwingine unawasili,na hana pikipiki wala baiskeli ni watu wanakuja wenyewe dukani...sipati picha kama angejiongeza na pikipiki 2 used for delivery....na kuna wakati analazimika kufunga duka kwa kukosa/kuchelewa mzigo ...
 
100% Ufugaji unalipa. Demand pia ni kubwa. Na hapo bado hajawaza nje ya box Kuongeza na Huduma zingine kama Kuuza kuku waliokwisha andaliwa kwenye masherehe. Infact Ufugaji unalipa kama ukija na ubunifu wakitofauti.
 
Mkuu hapo nimeweka kiwango Cha chini ukijitahidi kwa siku ukiwa na pikipiki moja trey 20 na Kama ukimaliza mzigo utarudi Tena kufata mzigo mwingine Kumbuka Kuna vibanda vya chips wengine kwa siku wanamaliza trey hata 3 mpaka tano Sasa ukiwa na wateja Kama hao 10 ndani ya Dar nzima si unaweza ukauza mzigo...???

Mkuu Kosoa na wewe wapi Pana shida na toa suluhisho usikimbilie tu kukosoa ndo maana tupo hapa kupeana maujuzi namna ya gani ya kuboresha hii biashara na kuiendeleza

Angalizo kabla hujaingia kwenye hii biashara nashauri tafuta kwanza Ni wapi pa kuyapata hayo mayai na kwa Bei gani na je Yana faida na Kama faida ipo Rudi utafute soko Ni akina Nani wa kuwauzia hayo mayai tafuta hata wateja 10 wa kuanza nao angalau hata trey 10 ukishapata Rudi Tena utafute eneo au frame na leseni pia na mwisho Anza kazi na Muda huo ukianza kazi endelea kutafuta wateja wapya na jitahidi kila siku upate wateja wapya angalau 2 Hadi watatu uone biashara itakavyokuwa taratibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…