Mchanganuo wa gharama ya kulima ekari moja ya mahindi

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,917
Reaction score
11,801
Huu hapa ni mchanganuo wa kulima ekari moja ya mahindi kwa sasa hivi
1. Kukodi shamba ekari 1 - 70,000/-
2. Kulima shamba mara 2 - 60,000/-
3. Mbegu pakiti 6 sawa kg 12 - 72,000/-
4. Kupanda mahindi - 30,000/-
5. Mbolea 2 - 140,000/-
6. Palizi 2 - 60,000/-
7. Kuweka mbolea - 30,000/-
8. Kuvuna/kupukuchua/mifuko - 100,0000/-

Jumla ya gharama huwa ni 550,000/- ~ 600,000/-

Mavuno
Mara nyingi mavuno hutegemea ubora wa ardhi na matunzo ya mazuri ya mazao, lakini mara nyingi ekari moja ya mahindi hutoa gunia 15 ~ 25, sasa ukipata kiwango cha chini gunia 15 ukauza kwa bei ya sasa 80,000/- unapata Tsh 1,200,000/- faida ya Tsh 600,000 kwa ekari.
 
Safi hio ni specific kwa eneo gani na wilaya ipi?
 
Mchanganuo mzur kabsa ingawa hiyoo n maximum calculator...lzm vbarua uwalalie kidogo ku minimize cost of running...
 
Kwa huku niliko, nimekodi ekari 3 Tsh 80,000/
Palizi ya kwanza kila ekari Tsh 21000 mara 3 63000

Ya pili napiga dawa ya magugu 25 kila ekari pamoja na mpigaji.

25000×3= 75000
Mbegu 30 Kg kila kg 10 ni 70000 jumla 210,000/
Kuvuna kila ekari ni 15000 mara 3 45000

Kupiga kila gunia 1000,
Watani gunia 60, so 60,000.

Mbolea mifuko 9 *70000

80000+65000+75000+210000+45000+630000
Total 115000, naongeza laki dharura. So 1,205,000.

Minimum bei ni 50k mara 60 ni 3M.
 
Kwa mazingira nlotoka
Kukodi ekar 1 =150k
Mbegu mahindi pakiti Moja =12k
Kulima ekari moja trekta =45k
Mbolea 120k
Palizi 2 50k
 
Ekari moja huhitaji mbegu ya mahindi kiasi gani? Ni umbali gani kutoka mche hadi mche?

Mi nilikuwa najua ni kg 4 kwa ekari.
 
Umekimbia mbio sana kwenye uandishi mkuu, ungeandika taratibu kidogo. Tunatamani kujifunza.
 
Ungemalizia pia hii faida ya laki 6 unaipata baada ya mda gani..

Kwangu mm ukilima chini ya ekari 10 bas faida na muda utakaotumia kupata iyo faida ni sawa na bure
 
Samahani ndugu ni mkoa gani huu naweza kupata nami eneo la kukodi ata kama ni ekari mbili huu ni mkoa gani ndugu yetu naomba nipe muongozo ndugu yangu!!
 
Kwa mazingira nlotoka
Kukodi ekar 1 =150k
Mbegu mahindi pakiti Moja =12k
Kulima ekari moja trekta =45k
Mbolea 120k
Palizi 2 50k
Ni.mkoa ganu huu ndugu yangu nahitaji hii kitu taifadhari kama hutojali share na mi zaidi maana nami nahitaji kulima ndugu yangu
 
Mkuu hii ni mkoa gani ambapo na mimi naweza kupata na mimi eneo la kulima!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…