Mchanganuo wa gharama ya kulima ekari moja ya mahindi

Mchanganuo wa gharama ya kulima ekari moja ya mahindi

mkuu kg 12 za mbegu ni sawa na miche 24,000 kwny eka moja inawezekana japo wengi tupo kwny miche 17,000 kwa spacing ya 30x90cm
Kitu tunachokosea mara kwa mara ni mbolea, kama tuna ambiwa kila mche tuweke grams 5 ya kila mbole meaning 5x24,000= 120,000gm ya mbolea sawa na 120kg = sawa na mifuko miwili na nusu kwa maana hiyo kwa eka 1 utahitaji jumla mifuko 5 ya mbolea.
Hata kwa miche 17,000 bado utahitaji kilo 170 ya mbolea jumla ni karibia mifuko 3.5 Ukiachilia mbali mvua pia nadhan tunashindwa kufanya vzr kwny kilimo kwa kukosa taarifa muhimu zinazopelekea kupata mazao hafifu.
Na anza rasmi kulima mwaka huu ntajitahidi kufata maelekezo yote ya kitaalamu pamoja na kushare taarifa kwa wanavijiji lilipo shamba ili kubalance stories nitajitahidi kuweka hapa jukwaa pendwa
Umenisaidia sana kujua kwamba kumbe mche mmja unakula gramu 5 tena hapo ni ikiwa imewekwa Kwa ushahidi na hakuna vitu vilivyosababisha ikapotea kama timing mbaya
 
Huu hapa ni mchanganuo wa kulima ekari moja ya mahindi kwa sasa hivi
1. Kukodi shamba ekari 1 - 70,000/-
2. Kulima shamba mara 2 - 60,000/-
3. Mbegu pakiti 6 sawa kg 12 - 72,000/-
4. Kupanda mahindi - 30,000/-
5. Mbolea 2 - 140,000/-
6. Palizi 2 - 60,000/-
7. Kuweka mbolea - 30,000/-
8. Kuvuna/kupukuchua/mifuko - 100,0000/-

Jumla ya gharama huwa ni 550,000/- ~ 600,000/-

Mavuno
Mara nyingi mavuno hutegemea ubora wa ardhi na matunzo ya mazuri ya mazao, lakini mara nyingi ekari moja ya mahindi hutoa gunia 15 ~ 25, sasa ukipata kiwango cha chini gunia 15 ukauza kwa bei ya sasa 80,000/- unapata Tsh 1,200,000/- faida ya Tsh 600,000 kwa ekari.
Hesabu za mkoa gani
 
Wacha kutisha watu.Ekari 10 zinakupa faida nzuri,hapo ni gunia minimum 250 *50,000=12,500,000 ambapo gharama zote sio zaidi ya 5,500,000.

Unavyolima ekari nyingi ndivyo unit cost inapungua
Siyo kutishana, hiyo breakdown iliangalia ekari moja. Ninajua pia gharama hupungua kidogo kwa Large scale farming. Ujumbe wang ulilenga uhalisia kwamba ili upate faida inabidi ulime mahindi mengi!
 
Back
Top Bottom